Chadema CUF TLP NCCR - LIVE from Urafiki Social Hall

Hivi huyu Mabere Marando ni yule ambaye alitoka NCCR na kwenda sisi M baada ya kukorofishana na Mrema ama ni mwingine? Ina maana amerudi tena upinzani?
Naomba ufafanuzi.

Kama hujui nyamaza!!!!!Marando hajawahi kuwa mwana CCM. Inaweza kukushangaza, lakini ndio ukweli huo. Na tangu alipogombana na Mrema hajajihusisha na siasa za chama kingine mbali na NCCVR-Mageuzi. Kimya chake, na baada ya Mrema kutofautiana na viongozi wenake wote (wakiwamo Bagenda, Lwekamwa, Jaffu, Ngawaiya, Tao an wengine) kimewafanya waliomsakama Marando wagundue nani alikuwa mwiba yeye au Mrema. Yule jamaa kichwa, achana naye. Hata kama humkubali, hii ni sifa yake, apewe.
 
labda jamaa waliona kwamba iwapo wangeitoa baada ya uchaguzi na iwapo itakuwa ccm imeshinda, wataambiwa wanatafuta visingizio vya kushindwa. aidha labda wamesikia kuna watu/mtu anataka kuitoa na hivyo wakichelewa wanaweza kosa sababu ya kuibeba hoja.

swali: wakuu hivi uchaguzi unashindaniwa siku ya kupiga kura? mi nilidhani ushindi unapatikana kwa kazi inayofanywa kabla ya uchaguzi. ndo maana tunasema " biashara asubuhi, jioni ni mahesabu"
 
Asante Lunyungu. Mimi nimeletewa nakala, sikujua kama Lunyungu umeshaipata na kuifikisha hapa. Kama alivyoshauri Mwanakijiji, next time nitasoma kwanza.
 
Hii kampuni ya uwakili ya IMMMA ni disaster kwa taifa!imeusishwa ni mikataba mingi yenye utata. Lakini naona anayetajwa mara kwa mara ni Ishengoma (i ya mwanzo), kumbe pia kwenye hizo triple m zilizofuatana, mojawapo ni Masha ambaye alikuwa naibu waziri madini na nishati lakini kutona na conflict of interest (kwamba ni director share holdetr wa tanzanite one) ikabidi muungwana amwamishe kule.Hizi syndicate ni muda mwafaka wa kuzianika hadharani wananchi waamue wenyewe sasa
 
Kumbuka na Balozi wenu wa UK ni mmoja kati ya IMMMA shareholders. SO yawezekana mwungwana kumpa ubalozi ni kulipa fadhila. Vile vile na mtoto wa JK anafanya kazi IMMMA
 
Watanzania kama akili zetu ndo hizi za kuishabikia CCM iendelee kushinda kwa gharama yeyote ile, basi tuna halali ya kuibiwa pesa zetu.Unapomjua huyu mtu ni jambazi na unamkabidhi safe ya fedha,una akili kweli?
Kwangu haya siyo mapya labda data ndo kitu kipya.Lakini wizi wa CCM umeanza siku nyingi. Walikula THB,SUKITA,NBC,NIC na sasa BENKI KUU vyote ni kugharimia uchaguzi ila wengine ndo wananufaikia humo.Na bado.
Naanza kuwa na wasiwasi na theory ya DNA inawezekana ni sahihi.
 
Kwa Mwendo Huu kama CCM itapita tena kwa kishindo ni bora kuomba Uraia wa Malawi.Hainiingii akilini kuona kuwa Hatuna Huduma muhimu kwa jamii kumbe pesa zinatumiwa visivyo na wapenda Madaraka?Tuliwasaidia kupata uhuru Msumbiji,Angola,Botswana na hata Namibia hao wote leo wana maisha yenye nafuu kuliko sisi tuliowaonyesha njia!Hivi tuna laana? Hapana WATANGANYIKA imefika wakati sasa CCM Lazima waondoke!!!
 
Very frustrating indeed! Sasa kama tunaambiwa wapinzani wameshinda viti viwili tu, hii kama sio disaster ni nini? Tuna kazi kubwa sana ya kufanya katika ile nchi nayo ni kuhusisha shida za wananchi wanazopata na aina ya uongozi walio nao. Hatuna short cut, we have to work hard collectively as a people and a nation, otherwise we are doomed!
 
CCM kula nchi baba kwani wenye nchi wenyewe wanaridhika na kazi yako na kukupa ushindi wa kishindo.Kwani hawajui kuwa wewe ni jambazi na uhai na ushindi wako unategemea sana kuendelea kuwepo kwako madarakani??Ukishamaliza benki kuu tunazo zingine tumezificha kibindoni uje uchukue.
 
naomba nirudie tena, ukichukua na kile kiti cha Chunya, basi wapinzani tayari wanavyo vitatu. Sasa bado matokeo yote hayajatangazwa. Wakipata viti angalau vitano kati ya 16 vinavyoshindaniwa itakuwa ni 1/3 ya viti vyote. Wakipata zaidi ya hapo itakuwa ni karibu nusu ya viti vyote. So, tusubiri matokeo yote, ila kwa chama ambacho kina mtandao, nyenzo na fedha toka BoT kushindwa viti vitatu ni pigo kubwa na la kutia aibu!! na kama watapoteza viti vingine basi ni kama tsunami!!
 
Asante Lunyungu kwa habari hizo.Sintoshangaa nispoziona kwenye website ya gazeti lolote la kesho.It happened before,after mkutano wa kutangaza orodha ya mafisadi.Na pengine ndo maana Mwananchi hawaja-update website yao hadi muda huu.

Wazo la kuunda tume huru ni zuri lakini haliwezekani kwa sababu hakuna jambazi active (kwa maana anaendelea na ujambazi) ambaye yuko tayari kuwakaribisha CID nyumbani kwake.So,what's next?

1.Tuwaombee dua za aina mbili hawa mafisadi.Dua ya aina ya kwanza ni wapatwe na uchungu wa nchi yao.Dua la pili ni wapate adhabu ya ufisadi wao hapahapa duniani.Wazinzi wafumaniwe au wateseke kwa ukimwi,walevi wapate ajali,na balaa zozote zile zitakazokujia akilini wakati unasoma dua hiyo...

2.Kwa sie wenye nyenzo kama mtandao,tujitahidi kusambaza taarifa (kama hii ya leo)kwa wenzetu ambao kwa namna moja au nyingine hawajui kinachoendelea huko nyumbani.Iwapo kila mwana-JF mmoja atasambaza kwa marafiki zake wa5 au 10 basi in long run ujumbe unaweza kufika kwa watu wengi zaidi.On top of that,wenye uwezo wa kutafsiri taarifa hiyo kwa kimombo wanaweza ku-submit kwenye vyombo mbalimbali (including international media,etc) ambavyo kwa namna moja au nyingine vinaweza kushinikiza serikali zao zinazotumia fedha za taxpayers wao kutupa misaada (kwa nia nzuri kabisa) lakini zinaishia mifukoni mwa mafisadi.Hapa hoja sio kuomba wasitishe misaada bali kuwalazimisha mafisadi hao wawajibike.

Tukiendelea kutofanya chochote ipo siku tutafukuzwa Tanzania baada ya nchi kuwa imeshauzwa yote,na wanunuzi wanataka kuhamia kwenye eneo lao jipya.So far mafisadi wamekuwa wanauza nchi kwa rejareja,lakini kwa vile wengine hawana uhakika sana na afya zao (as well as adhabu za hapahapa duniani eg ajali) wanaweza kabisa kuiuza nchi kwa bei poa ya jumla.Kila mmoja wetu ajaribu kutu,ia nynzo aliyonayo kuwadhibiti wanaharamu hawa.

As to hao wenye mtindio wa uwezo wa kutambua wezi,maharamia,mafisadi,majambazi,mabaradhuli,etc ambao pamoja na kufafanuliwa namna gani nchi yetu inatafunwa na mafisadi lakini bado wanaleta habari kuwa "hizo ni porojo za wapinzani" au "wapinzani walipaswa kusimamia uchaguzi badala ya kwenda Urafiki Hall kutupa news hizi",cha kufanya ni kuwaacha wabwabwaje.Nadhani tatizo lao kubwa ni huo mtindio na wala sio mapenzi na CCM.Tukiwapuuza,badala ya kupoteza muda kubishana nao,wanaweza kupata nafuu ya "maradhi" yanayowakabili.
 
Kwa Mwendo Huu kama CCM itapita tena kwa kishindo ni bora kuomba Uraia wa Malawi.Hainiingii akilini kuona kuwa Hatuna Huduma muhimu kwa jamii kumbe pesa zinatumiwa visivyo na wapenda Madaraka?Tuliwasaidia kupata uhuru Msumbiji,Angola,Botswana na hata Namibia hao wote leo wana maisha yenye nafuu kuliko sisi tuliowaonyesha njia!Hivi tuna laana? Hapana WATANGANYIKA imefika wakati sasa CCM Lazima waondoke!!!

Mwawado:
Kuhamia Malawi si suluhisho, utaendelea kuumia kila siku kwa kuwaona babu/baba/dada zako wakiendelea kuumia chini ya himaya ya CCM na serikali zake. Huko Malawi maisha yako hayatakuwa ya amani hata kidogo.

Washindani wasiwe na papara, inabidi wawe na subira wakati huu hata kama matokeo ya uchaguzi wa leo yatakuwa sio ya kuridhisha. Matokeo haya sio kipimo cha kupendwa kwa watawala hawa, ila yachukuliwe kwamba ujumbe haujawafikia wananchi huko waliko vijijini. Kumbuka kuwa mambo haya yanayosemwa na washindani hayatangazwi kwa mapana na marefu yake na vyombo vya habari vinavyowafikia wananchi. Usichukulie tunavyopata habari humu JF ndivyo ukadhani na wananchi nao habari hizo zinawafikia kiurahisi hivyo. Ni mhimu sana kulitambua hili haraka kabla hata ya viongozi wategemewa kama akina Kitila kuanza kujiuliza na kutoa hisia za kukata tamaa kama zilizotolewa hapo juu.

Njia pekee na ya uhakika kabisa ya kuwafikia wananchi na kuwapelekea ujumbe wa mambo yanavyotokea nchini mwao ni kwa hawa viongozi kuwafikia hao wananchi kwa kila njia inayowezekana kati ya sasa na kabla ya 2010.

Ujumbe wangu ni kwamba, msiwaharakishe wananchi. Wapeni ukweli wa mambo yalivyo, na sababu za wao kutoa uamzi wao wa kutowachagua tena CCM. Sababu hizo sasa zipo nyingi tu, ni namna ya kuzifikisha tu huko zinakotakiwa ndiko bado hakujapatiwa msukumo unaostahili.

Itasikitisha sana kama nafasi hii itawaponyoka tena washindani.
 
Kitila Mkumbo
Perfomance mbaya ya opposition kenye chaguzi hapa Tanzania, kama wewe hii unayoita social disaster inaonekana kama imepangwa. Unajua kama ukitaka kuwatawala watu kwa muda mrefu ni kwanza uwafanye wajinga, ukiangalia Tanzania utagundua kuwa graduates kama wewe ni wachache sana, wengi wa wapiga kura bado hawanauelewa mkubwa. Ndio maana strong hold ya CCM sio mijini kwenye watu wenye uelewa, ila ni vijijini ambako mpaka sasa hata ukiwaambia watu kuwa kuna ufisadi Tanzania hawaelewi kitu, kwanza akienda Malecela akawaambia ahhhhhh ni uongo tu, wanaweza kumuamini. Nakumbuka kuna siku Profesa Baregu aliambiwa kuwa kama ukitaka kugombea nafasi ya ubunge au uwakilishi, inatakiwa wapiga kura wawe kama mlimamni community, la sivyo unaweza kushangaa mtu kama John Komba anashinda nafasi ya uchaguzi halafu Baregu anatupwa, hili ndio tatizo. KWa hiyo zinahitajika juhudi zaidi kufikia huko. Mimi nadhani viti vitatu ni success, pamoja na kuwa juhudi zaidi zinatakiwa.
 
Hii inasikitisha mno especially ninapoendelea kusikia viongozi wa CCM wakijibu hoja za shida za wananchi kwa kisingizio kwamba serikali haina fedha. Hivi kweli serikali inayokusudia kuanza kukusanya kodi hadi kufikia shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi, kweli inashindwa kumlipa mwalimu wa shule ya msingi angalau shilingi laki moja?? Wanashindwa kuwalipa madaktari angalau lake nane??

Na kinachonisikitisha zaidi ni pale ninaposikia mtu mzima na akili zako unatunga hoja za kipumbavu ili kutetea uozo wa CCM. This is really sad. Where is your dignity? I feel like weeping simply from reading these about these allegation and feeling sorry for the poor Tanzanians ambao kama kondoo tunachungwa na kuongozwa kwenye kiama huku tukiambiwa tudumisha amani.
 
Kitila Mkumbo
Perfomance mbaya ya opposition kenye chaguzi hapa Tanzania, kama wewe hii unayoita social disaster inaonekana kama imepangwa. Unajua kama ukitaka kuwatawala watu kwa muda mrefu ni kwanza uwafanye wajinga, ukiangalia Tanzania utagundua kuwa graduates kama wewe ni wachache sana, wengi wa wapiga kura bado hawanauelewa mkubwa. Ndio maana strong hold ya CCM sio mijini kwenye watu wenye uelewa, ila ni vijijini ambako mpaka sasa hata ukiwaambia watu kuwa kuna ufisadi Tanzania hawaelewi kitu, kwanza akienda Malecela akawaambia ahhhhhh ni uongo tu, wanaweza kumuamini. Nakumbuka kuna siku Profesa Baregu aliambiwa kuwa kama ukitaka kugombea nafasi ya ubunge au uwakilishi, inatakiwa wapiga kura wawe kama mlimamni community, la sivyo unaweza kushangaa mtu kama John Komba anashinda nafasi ya uchaguzi halafu Baregu anatupwa, hili ndio tatizo. KWa hiyo zinahitajika juhudi zaidi kufikia huko. Mimi nadhani viti vitatu ni success, pamoja na kuwa juhudi zaidi zinatakiwa.

nilihadharisha mapema kuhusu haya ya kuwaona wananchi wajinga, na hapa ndipo vyama vya ushindani vinapoangukia pua.

wananchi kote wengi wanauelewa mzuri tu pengine kuliko hata huo wako, uelewa kipimo chake si kuchagua upinzani tu.
 
Back
Top Bottom