Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,184
- 671
Mwawado:
Kuhamia Malawi si suluhisho, utaendelea kuumia kila siku kwa kuwaona babu/baba/dada zako wakiendelea kuumia chini ya himaya ya CCM na serikali zake. Huko Malawi maisha yako hayatakuwa ya amani hata kidogo.
Washindani wasiwe na papara, inabidi wawe na subira wakati huu hata kama matokeo ya uchaguzi wa leo yatakuwa sio ya kuridhisha. Matokeo haya sio kipimo cha kupendwa kwa watawala hawa, ila yachukuliwe kwamba ujumbe haujawafikia wananchi huko waliko vijijini. Kumbuka kuwa mambo haya yanayosemwa na washindani hayatangazwi kwa mapana na marefu yake na vyombo vya habari vinavyowafikia wananchi. Usichukulie tunavyopata habari humu JF ndivyo ukadhani na wananchi nao habari hizo zinawafikia kiurahisi hivyo. Ni mhimu sana kulitambua hili haraka kabla hata ya viongozi wategemewa kama akina Kitila kuanza kujiuliza na kutoa hisia za kukata tamaa kama zilizotolewa hapo juu.
Njia pekee na ya uhakika kabisa ya kuwafikia wananchi na kuwapelekea ujumbe wa mambo yanavyotokea nchini mwao ni kwa hawa viongozi kuwafikia hao wananchi kwa kila njia inayowezekana kati ya sasa na kabla ya 2010.
Ujumbe wangu ni kwamba, msiwaharakishe wananchi. Wapeni ukweli wa mambo yalivyo, na sababu za wao kutoa uamzi wao wa kutowachagua tena CCM. Sababu hizo sasa zipo nyingi tu, ni namna ya kuzifikisha tu huko zinakotakiwa ndiko bado hakujapatiwa msukumo unaostahili.
Itasikitisha sana kama nafasi hii itawaponyoka tena washindani.
hata matokeo bado unatoa excuse eeh. si mlisema CCM kwisha sasa mnasema ujumbe haujafikia wananchi vijijini.
kwani mliowafundisha kuzomea walikuwa wananchi wa mjini?
nyie endelezeni fitna na kuigawa nchi kwa kumbandika huyu fisadi huyu mkombozi.
sisi tuko karibu na wananchi kutatua shida zao.nyinyi ukaribu wenu na fitna na ubinafsi endeleeni na sambazeni chuki lkn mpanda shari huvuna shari