Chadema CUF TLP NCCR - LIVE from Urafiki Social Hall

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Sasa ni saa 10:20 toka katika Ukumbi wa Urafiki Social Hall . Viongozi wa Vyama vyote wapo nje ya Ukumbi wanafanya maongezi na wana Habari . Mrema yupo, Slaa yupo,Marando Mabere yupo na CUF sijamuona mwakilishi wao ila nangoja. Kwa upenda wa NCCR na CUF sijajjua nani mwakilishi wao ila niko hewani nitawapa yanayuo jiri .Wana habari wamejaa hapa sasa sijui kama watasema yatakayosemwa hapa kama yalivyo ama watakaa kama last time pia .
 
Mkutano umeanza kwa kutoa hii statement. Mambi yanaendelea


TAARIFA KWA WANANCHI WA TANZANIA

MABILIONI ZAIDI YALIIBIWA BOT WAKATI WA UCHAGUZI MKUU 2005!

Ndugu wananchi,

Tarehe 15 Septemba 2007 tulitoa Orodha ya Mafisadi yenye kuonyesha ufisadi, wizi na/au ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma unaowahusisha viongozi na watendaji wa juu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano na watu wengine walio kwenye uongozi wa umma. Hadi sasa Serikali haijatoa majibu ya kuridhisha kuhusiana na tuhuma hizi nzito licha ya madai ya kufanya hivyo kutoka kwa wananchi, taasisi zisizo za kiserikali, viongozi mbali mbali ndani na nje ya Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) na hata wawakilishi wa nchi wafadhili walioko Tanzania.

Leo tunaomba kuwajulisha wananchi wa Tanzania kupitia Mkutano huu Maalum na Wananchi wa Dar es Salaam juu ya taarifa zinazoonyesha kuwepo kwa ufisadi na/au wizi wa mabilioni mengine ya fedha za umma uliofanyika wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2005. Nyaraka mbali mbali ambazo tumezipata hivi karibuni zinaonyesha kwamba makampuni hewa (shell companies) kadhaa yalianzishwa katika vipindi tofauti kabla ya Uchaguzi Mkuu kwa lengo mahsusi la kupitishia fedha zilizoibiwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Nyaraka hizi vile vile zinaonyesha jinsi ambavyo fedha hizo ziliibiwa na kwa wakati gani kama ifuatavyo:

1. DEEP GREEN FINANCE COMPANY LIMITED

Mnamo tarehe 18 Machi 2004 ilianzishwa kampuni iitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. kwa madhumuni ya, pamoja na mengine, kufanya biashara kama ‘mabepari’ na wakopeshaji fedha! Kufuatana na taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakurugenzi wa Deep Green Finance walikuwa ni mabwana Mark Ross Weston wa New Zealand; Anton Taljaard wa Afrika Kusini; na Rudolph van Schalkwyk pia wa Afrika Kusini. Wote watatu ni wakazi wa Afrika Kusini na wanaelekea kuwa ni maafisa na/au wafanyakazi wa Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini. Kufuatana na taarifa za BRELA, wanahisa wa awali wa Deep Green Finance walikuwa ni mawakili Protase R.G. Ishengoma na Stella Ndikimi wa kampuni ya mawakili ya IMMMA Advocates; Nedbank Ltd., Nedbank Africa Investments Ltd. na SBM Nedcor Holdings Ltd. Tarehe 15 Aprili 2005 mawakili Ishengoma na Ndikimi walihamisha hisa zao kwa Nedbank Ltd. na Nedbank Africa Investments Ltd. IMMMA Advocates vile vile ni mawakili wa Tangold Ltd. ambayo imehusishwa na ufisadi tuliouelezea katika Orodha ya Mafisadi.

Taarifa za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba tarehe 1 Mei 2004, Deep Green Finance ilifungua Akaunti Na. 011103024840 katika tawi la Corporate la Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Dar es Salaam. Kitu cha kwanza cha kushangaza ni kwamba siku hiyo ilikuwa ni Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) na ilikuwa siku ya mapumziko. Kitu cha pili cha kushangaza ni kwamba kampuni hii iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti hiyo bila ya kuingiza wala kutoa fedha yoyote kwa zaidi ya mwaka mmoja kuanzia tarehe 1 Mei 2004 hadi tarehe 31 Julai 2005. Kitu cha tatu cha kushangaza ni kwamba pamoja jina la Deep Green ‘Finance’ kuashiria kwamba kampuni hii ni taasisi ya kifedha, orodha ya taasisi za kifedha iliyotolewa na BOT tarehe 21 Agosti 2007 haionyeshi kwamba kampuni hii imewahi kusajiliwa na BOT kama taasisi ya kifedha!

Hata hivyo, kwa kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 na Desemba 1, 2005 kampuni hii ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 kutoka Wizara ya Fedha na/au BOT. Fedha hizo zilitolewa kwa utaratibu ufuatao:

(a) Tarehe 1 Agosti 2005 BOT, kwa kutumia hundi Na. 241740, ilihamisha dola za Marekani 1,354,167.26 au shilingi za Tanzania 1,546,778,770.92 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku hiyo hiyo fedha hizo zote zilichukuliwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwa utaratibu maalum wa haraka (special clearance) na kupelekwa mahali kusikojulikana na kwa madhumuni yasiyofahamika;

(b) Tarehe 1 Septemba 2005 BOT, kwa kutumia hundi Na. 015558, ilihamisha dola za Marekani 1,827,137.44 au shilingi za Tanzania 2,083,255,881.60 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku hiyo hiyo jumla ya shilingi 2,083,333,333.33 zilichukuliwa kwa mara nyingine tena kwa kutumia utaratibu huo huo maalum wa haraka na kupelekwa kusikojulikana;

(c) Tarehe 8 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha dola za Marekani 100,256.62 au shilingi za Tanzania 114,611,746.80 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Itakumbukwa kwamba Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni iliyoandikishwa nchini Mauritius tarehe 5 Aprili 2005 na kupewa Cheti cha Kutimiza masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006. Hata hivyo, mawaziri kadhaa wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wameendelea kudai kuwa kampuni hiyo inamilikiwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Tanzania. Wakurugenzi wa Tangold Ltd. ni Gavana Daudi Balali, Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge, Katibu Mkuu (Fedha) Gray Mgonja, Katibu Mkuu (Maji) Patrick Rutabanzibwa na Katibu Mkuu (Ofisi ya Waziri Mkuu) Vincent Mrisho. Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa BOT ya tarehe 21 Desemba 2006, Tangold Ltd. ililipwa na BOT dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kupitia akaunti isiyojulikana ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini na kwa madhumuni yasiyojulikana;

(d) Tarehe 16 Septemba 2005 jumla ya shilingi 129,000,000.00 zilitolewa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance na kuwekwa kwenye akaunti ya muda maalum (FDR);

(e) Tarehe 3 Oktoba 2005 jumla ya shilingi 2,083,333,333.33 za Wizara ya Fedha zililipwa kwa utaratibu maalum wa haraka kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Inaelekea fedha hizo zililipwa kabla BOT haijaingiza fedha yoyote kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwa vile tarehe 4 Oktoba 2005 BOT ilihamisha dola za Marekani 1,789,075.89 au shilingi 2,083,891,765.35 kwenda kwenye akaunti hiyo;

(f) Tarehe 8 Oktoba 2005 jumla ya shilingi 39,761,397.98 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda Tangold Ltd.;

(g) Tarehe 31 Oktoba 2005 jumla ya shilingi za Tanzania 2,083,333,333.33 fedha za Wizara ya Fedha zilihamishiwa kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(h) Tarehe 2 Novemba 2005 dola za Marekani 1,821,095.57 au shilingi za Tanzania 2,083,653,279.68 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(i) Tarehe 30 Novemba 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 2,083,333,333.33 zikiwa fedha za Wizara ya Fedha kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku moja baadaye, dola za Marekani 1,817,199.52 au shilingi za Tanzania 2,184,610,383.04 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(j) Tarehe 10 Desemba 2005 shilingi 100,940,489.71 zilihamishwa kutoka Tangold Ltd. kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Hii ilikuwa ni siku nne tu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 14, 2005 kufanyika nchini kote;

(k) Tarehe 19 Desemba 2005, siku tano baada ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, dola za Marekani 88,722.17 au shilingi za Tanzania 104,755,554.09 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(l) Tarehe 9 Februari 2006 shilingi 3,836,800.00 zilihamishwa kwenda akaunti ya mawakili wa Deep Green Finance, IMMMA Advocates, iliyoko benki ya Standard Chartered. Haijulikani kama fedha hizi zilikuwa ni kwa ajili ya malipo ya mawakili hao au la;

(m) Malipo ya mwisho kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance yalifanywa tarehe 22 Novemba 2006 ambapo jumla ya shilingi 14,465,000.00 zilihamishiwa katika akaunti isiyojulikana ya benki ya Standard Chartered na kwa matumizi yasiyojulikana;

Kutokana na rekodi za kibenki zilizoonyeshwa hapo juu, jumla ya shilingi 10,484,005.39 ziliingizwa katika akaunti ya Deep Green Finance katika kipindi cha miezi minne tu kati ya tarehe 1 Agosti na 10 Desemba 2005. Hiki kilikuwa ni kipindi cha mchakato na/au kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 14 Desemba 2005. Aidha, kuanzia tarehe 11 Desemba 2005 hakuna fedha yoyote iliyoingizwa katika akaunti hiyo hadi tarehe 27 Februari 2007 kampuni hiyo ilipovunjwa ‘kwa hiari’ ya wanahisa wake. Ni muhimu kurudia kwamba, kwa ushahidi huu wa nyaraka za kibenki, kampuni ya Deep Green Finance haikuwa na hata senti moja kabla ya tarehe 1 Agosti 2005 na wala haikupokea hata thumni mara baada ya tarehe 10 Desemba 2005 na mara baada ya Uchaguzi Mkuu.

Kwa taarifa za sasa hivi, inafahamika kwamba faili la Deep Green Finance lililotakiwa kuwa BRELA limetoweka. Tuna kila sababu ya kuamini kwamba hii ilikuwa ni kampuni hewa (shell company) iliyoundwa kwa ajili tu ya kupitishia fedha za umma kutoka Benki Kuu kwenda kusikojulikana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2005. Ndio maana kampuni hiyo haikuwa na fedha zozote benki kutokea tarehe 1 Mei 2004 hadi tarehe 1 Agosti 2005, wiki tatu kabla ya kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu. Na ndio maana mabilioni iliyolipwa na Benki Kuu yalilipwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na mara baada ya Uchaguzi Mkuu kupita malipo hayo ya fedha za umma yalikoma.

2. TANGOLD LIMITED

Kama Orodha ya Mafisadi inavyoonyesha, Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni inayomilikiwa na baadhi ya Mafisadi tuliowataja katika Orodha hiyo. Kuna utata mkubwa zaidi ambao umeigubika kampuni ya Tangold Ltd. Kwanza, licha ya nyaraka kuonyesha kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006, nyaraka za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba Tangold Ltd. ilifungua akaunti ya shilingi Na. 011103024852 NBC Corporate Branch tarehe 1 Januari 2003. Kama ilivyokuwa kwa Deep Green Finance, siku ya Tangold Ltd. kufungua akaunti yake NBC ilikuwa ni Siku ya Mwaka Mpya na siku ya mapumziko kote nchini! Aidha taratibu za kibenki za ufunguaji wa akaunti za makampuni zinalazimu kampuni husika kuwasilisha benki nakala ya usajili wa kampuni, Katiba yake, leseni ya biashara na hati ya mlipa kodi ya TRA (TIN Registration Certificate) kabla ya kuruhusiwa kufungua akaunti. Swali la kujibiwa na NBC pamoja na Serikali ni je, ilikuwaje Tangold Ltd. iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti ya benki kabla hata haijaandikishwa nchini Mauritius achilia mbali kupata hati ya kutimiza masharti ya Tanzania?

Pili, kampuni ya Tangold Ltd. iliendesha akaunti hiyo bila kuweka au kutoa fedha yoyote ile kati ya tarehe 1 Januari 2003 hadi tarehe 1 Agosti 2005 ilipoanza kunyeshewa mvua ya neema ya mabilioni ya fedha za walipa kodi wa Tanzania kutoka BOT! Mvua hiyo ni nje ya mvua ya dola za Marekani 13,340,168.37 zilizohojiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali na iliinyeshea Tangold Ltd. kama ifuatavyo:

(a) Tarehe 1 Agosti 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 4,703,221,229.08 kwenda kwenye akaunti ya Tangold Ltd. Tarehe hii ni muhimu sana kwani ndiyo siku ambayo BOT ilifanya pia malipo ya kwanza kwa Deep Green Finance kama ilivyoelezewa katika Taarifa hii;

(b) Tarehe 2 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 244,428,386.15 kutoka akaunti yake hiyo kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Kama tuliyoelezea katika Taarifa hii, tarehe 1 Septemba 2005 Deep Green Finance ililipwa pia shilingi 2,083,255,881.60 na BOT;
(c) Tarehe 8 Oktoba 2005 shilingi za Tanzania 39,761,397.98 zilihamishiwa kwenye akaunti ya Tangold Ltd. kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(d) Tarehe 12 Oktoba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 1,690,500,000.00 kwenda Meremeta Limited;

(e) Tarehe 23 Novemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 555,300,048.00 kwenda Meremeta Ltd.;

(f) Tarehe 10 Desemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 100,940,489.71 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(g) Tarehe 12 Desemba 2005, siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu, Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 551,060,000.00 kwenda kwenye akaunti ya Meremeta Ltd.

Baada ya hapo Tangold Ltd. haikupokea wala kuingiza fedha zozote kwenye akaunti yake hadi tarehe 6 Juni 2006 ilipohamisha shilingi za Tanzania 220,980,370.00 kwenda ‘TISS.’ TISS ni kifupi cha Tanzania Intelligence and Security Service ambalo ni jina la Kiingereza la Idara ya Usalama wa Taifa! Tangu tarehe hiyo hadi leo hii Tangold Ltd. haijaweka wala kutoa fedha nyingine yoyote katika akaunti hiyo. Kwa maana hiyo, katika kipindi cha miezi minne Tangold Ltd. iliingiziwa na BOT jumla ya shilingi za Tanzania 4,742,982,627.06 na ilifanya malipo kwa Deep Green Finance na Meremeta Ltd. ya jumla ya shilingi za Tanzania 3,363,531,259.67.

Maswali muhimu ya kujiuliza kuhusiana na Tangold Ltd. ni haya yafuatayo. Kwanza, ilikuwaje kampuni ambayo haikuwa hata imeandikishwa kisheria ikalipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi na/au ya umma na bila maelezo yoyote? Pili, ilikuwaje Serikali, kwa kupitia Waziri Karamagi, itoe taarifa ya uongo Bungeni kwamba Tangold Ltd. ni kampuni mpya na imeanzishwa ili kurithi mali na madeni ya Meremeta Ltd. wakati makampuni yote mawili yalikuwa yakipeana mabilioni ya fedha za umma wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu katika mazingira ya kutatanisha? Tatu, kwa nini malipo ya mabilioni haya yalikoma mara baada ya Uchaguzi Mkuu? Nne, kama Tangold Ltd. ni kampuni inayomilikiwa na Serikali je ofisi zake ziko wapi? Watendaji wake wakuu ni kina nani? Fedha za kigeni dola za Marekani 13,340,168.37 zilizolipwa na BOT tarehe 29 Desemba 2005 zilikuwa ni kwa ajili gani na kwa nini zimeendelea kuwa katika akaunti ya Tangold Ltd. hadi wakati huu?

Hivi karibuni baadhi ya wanachama wa CCM wameanza kuhoji matumizi makubwa ya fedha wakati wa mchakato wa kumpata mgombea Urais wa CCM wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita. Kama mnavyokumbuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku ametoa hadharani barua aliyomwandikia Mwenyekiti wa CCM aliyepita Bwana Benjamin Mkapa akidai kuwepo kwa ushahidi kuwa “fedha nyingi zinatumiwa katika uchaguzi huu.” Na kama alivyohoji Mzee Butiku katika barua yake kwamba “fedha hizo zinatoka wapi na ni za nani”, nasi tunawaomba wananchi wa Tanzania waidai Serikali iwaeleze mabilioni haya ya fedha za umma yalilipwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2005 kwa ajili gani.

Ili kupata majibu sahihi ya maswali yote haya, Serikali haina budi kuridhia kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi wa tuhuma zote hizi na zile zilizotolewa katika Orodha ya Mafisadi. Ni tume huru pekee itakayoweza kuchunguza ufisadi huu bila woga, upendeleo au hila. Na ni ripoti ya tume huru pekee ndiyo itakayotumika kuwawajibisha wale wote watakaobainika kushiriki kulisababishia taifa letu hasara kubwa namna hii.

Tunatambua kwamba Serikali imeteua wakaguzi wa mahesabu kutoka kampuni ya Ernst Young LLP ili kufanya uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma katika akaunti ya malipo ya nje inayoendeshwa na BOT (EPA) kwa niaba ya Serikali. Tunaomba kuweka wazi msimamo wetu kuhusiana na uchunguzi huo kuwa hauhusu ubadhirifu, wizi na/au ufisadi ndani ya BOT tuliouelezea katika Orodha ya Mafisadi na katika Taarifa hii. Vile vile uchunguzi huo hauhusu ufisadi unaohusu kusainiwa kwa mikataba mibovu na ambayo imeliingizia na italiingizia taifa letu hasara ya mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa maana hiyo, tunatoa taarifa mapema kwamba ripoti ya wakaguzi wa Ernst Young LLP haiwezi na isije ikachukuliwa kuwa ndio majibu ya Serikali kwa tuhuma za ufisadi, wizi na/au ubadhirifu wa fedha za umma zilizotolewa katika Orodha ya Mafisadi na katika Taarifa hii. Tunapenda kusisitiza kwamba tuhuma hizi zinaweza kujibiwa tu na tume huru ya uchunguzi.

Kutokana na uzito wa masuala tuliyoyaeleza katika Taarifa hii, tunapenda kuwataarifu wananchi wa Tanzania kwamba iwapo Serikali itashindwa na/au kukataa kuridhia kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi wa tuhuma hizi hadi kufikia 25 Novemba mwaka huu, vyama vyetu vitatoa maelekezo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla juu ya hatua za kuchukuliwa nao ili kuondokana na ufisadi, wizi na/au ubadhirifu wa mali ya wananchi tuliouelezea katika Taarifa hii na katika Orodha ya Mafisadi.

Asanteni sana

-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI, CHADEMA
---------------------------------------------
AUGUSTINO L. MREMA
MWENYEKITI, TLP

--------------------------------------------
PROF. IBRAHIM H. LIPUMBA
MWENYEKITI, CUF

-----------------------------------------
JAMES F. MBATIA
MWENYEKITI, NCCR-MAGEUZI
 
Sasa anaongea Ndugu Mrema katika ufunguzi .Wakati anaongea namuona Lissu na John Mnyika wanaingia . Lissu kama mwanasheria yupo kuangalia utaratibu mzima wa kisheria .
 
Mafisadi mwaka huu wameshikwa pabaya ndio sababu wanakigugumizi, jambo jema ni kuwataja mabaradhuli na kuwaanika mchana kweupe ili wafilisiwe na kwenda Keko kutimiza wajibu wao. Hatuwezi kukubali watu wachache wafuje pesa ya walipa kodi na wawe huru kuitumia.
 
Sasa Slaa amejibu tuhuma rasmi juu ya mke wa mzungu na pesa za vilema . Hili naacha waandishi wengine walisemee.

Kaelezea habari za safari yake na sasa anachomoa hadharani mkataba wa Richmond. Sijaupata ila nikiupata nitaurusha .
 
Mmmhhhhhh, hapa kuna tatizo kubwa mno. Hivi hawa jamaa kweli wana huruma hata na nchi?

Inasikitisha sana, mambo kama haya ndiyo yanawafanya watu nchi zingine wachukue silaha.

Umaskini mkubwa wa Tanzani, watu wanajichotea pesa kiasi hicho?

KInachotakiwa ni kumfikisha Gavana Balali mahakamani, atakuja kusema tu hizo pesa zilienda wapi. Maana siku ya kufa hata mafisadi husalitiana.
 
Nimekubali mzee!

Nafikiri sasa kitendawili cha hujuma wakati wa uchaguzi kimetenguliwa!

Nafikiri sasa tumejua kwa nini JK anaonekana kuwa na wasiwasi sana.

Yeye mwenyewe yuko nyuma ya hila chafu kabisa.

Suluhisho yalifanyika usiku yameonekana mchana kweupe.

Hivyo walihusika hawana budi kubwaga manyanga. Afadhali Dr. Balali tayali amekimbia hila tutaomba marekani wamurudishe nchini ashitakiwe.
 
Dr.Slaa amesema wazi wazi kwamba hajapata barua ya kuitwa Mahakamani wala toka kwa wakili na amesisitiza kwamba waende Mahakamani.Ameombwa watuhumiwa waende Mahakamani . Amesema serikali ya US inaujua Ufisadi mkubwa na ina ushahidi mkubwa zaidi ya ule alio nao yeye .Naye kabaki kushangaa wazungu kujua zaidi ya sisi Watanzania .
 
Dr.Slaa amesema wazi wazi kwamba hajapata barua ya kuitwa Mahakamani wala toka kwa wakili na amesisitiza kwamba waende Mahakamani.Ameombwa watuhumiwa waende Mahakamani . Amesema serikali ya US inaujua Ufisadi mkubwa na ina ushahidi mkubwa zaidi ya ule alio nao yeye .Naye kabaki kushangaa wazungu kujua zaidi ya sisi Watanzania .

Jk aliingia madarakani kwa kishindo anaweza kungatuka pia kwa kishindo.

Nina uhakika asiposhughulikia haya maswala yatamshugulikia mwenyewe.

Kunahitajika soln au bunge linatakiwa kufanya kazi yake.

Otherwise hiki kiama.
 
Thanks Lunyungu kwa updates, endelea kutupa zaidi. Unajua tena yanayojiri huko hatuwezi kuyapata kwenye baadhi ya magazeti ya Bongo
 
Dr.Slaa amesema wazi wazi kwamba hajapata barua ya kuitwa Mahakamani wala toka kwa wakili na amesisitiza kwamba waende Mahakamani.Ameombwa watuhumiwa waende Mahakamani . Amesema serikali ya US inaujua Ufisadi mkubwa na ina ushahidi mkubwa zaidi ya ule alio nao yeye .Naye kabaki kushangaa wazungu kujua zaidi ya sisi Watanzania .

Wazungu wa West wanajua yote yanayotokea Afrika ila wananyamaza, wao ni washiriki kwenye huu ufisadi. Laiti wangeamua kuweka wazi kila wanachokijua, ufisadi Afrika ungepungua.

Lakini wao wanakaa kimya kwasababu hizo pesa nyingi zinaenda kwao ku create jobs, huku ndugu zetu Mbulu wanakufa njaa.

Yaani, mimi kichwa kinauma kusoma baadhi ya haya mambo. Hii ni laana tupu.
 
Haha
No doubt kuwa US wanafahamu zaidi kuliko tunavyofahamu wabongo, lakini ukweli unakuja palepale there is not much that they care, as long as they kiss their..., kama wakifanya hivyo bila shaka watawaunga mkono na kuwasifu kuwa mnafanya vizuri. Lakini kama wakienda kinyume na US wish wanatumia scandle hizo kama leverage ya kuwabomoa, kwa hiyo sio US au EU watakaosafisha nyumba yetu, ni sisi wenyewe. La muhimu ni kuwa wanaweza kutusaidia kutupa mwanga zaidi ya namna ya kudeal na hizo issue.
 
Jamani nashindwa niandike lipi na niache lipi maana kuna mengi sana yanayo jiri hapa . Slaa anasema kwamba TISS wamepewa 250m toka Tangold swali ni kwa nini pesa ziende huko ?
 
Jamani nashindwa niandike lipi na niache lipi maana kuna mengi sana yanayo jiri hapa . Slaa anasema kwamba TISS wamepewa 250m toka Tangold swali ni kwa nini pesa ziende huko ?

Hiyo ni scandal tayari, nafikiri RO anahusika kwani enzi hizo alikuwa DAP.
 
Jamani nashindwa niandike lipi na niache lipi maana kuna mengi sana yanayo jiri hapa . Slaa anasema kwamba TISS wamepewa 250m toka Tangold swali ni kwa nini pesa ziende huko ?
Tangold ina utata sana, TISS haiwezi kushindwa kujua suala kama hili, mimi naona hii ni bakishishi.
 
At least watu wanaanza kuongea wazi what happened. Ipo siku watu wataanza kuchukua hatua madhubuti. no moja ikiwa ni kutowapigia kura kwa maneno matamu aya mmbwembwe. wazomeeni wakiwa majukwaani. Zomeazomea ni fimbo ya mnyonge. God bless wazalendo wa Tanzania.
 
Nimechoka hata siwezi kunyanyua miguu, thanks Lunyungu! Lakini tusiishie hapa hii ni hatari kwa nchi maskini kama tz inayotegemea zaidi ya 40% ya budget kwa misaada.
 
Ndio inayoweza kusafisha uchafu huu. Kuendelea kukataa tuhuma nzito kama hizi bila ya kuzichunguza haisaidii kitu.

Wakubali tume ichunguze,hata kama baada ya uchunguzi hiyo ripoti iwekwe kabatini; kwani sidhani kamwe kuwa ripoti inaweza kutolewa hadharani kama inatishia kutia mchanga andazi.

Jambo mhimu la kujiuliza ni: Ni nani 'mastermind' wa mipango hii katika CCM na serikali yake?

1. Mkapa? Kwa manufaa yepi wakati anamaliza ngwe yake? Hata kama hakuwa na 'interest' ni kwa vipi aruhusu mambo haya ambayo dhahiri yanaweka doa zaidi katika 'legacy' yake?

2. Mtandao? na kwa maana hiyo Kikwete mwenyewe?

Lakini? Ninazidi kujiuliza: mbona tumekuwa mabingwa sana siku hizi kuwaiga wakenya karibu kila kitu? Mpango huu hautofautiani sana na ule wa "Anglo Leasing;" na hata katika mipango mbalimbali ya kimaendeleo inayopendekezwa na serikali, kama yale 'mabillion ya Kikwete,' na mengineyo mengi hasa yanayohusu ufisadi. Hata kuiga kwenyewe hatuigi vizuri, na matokeo yanakuwa ......kupasuka msamba!
 
Nimechoka hata siwezi kunyanyua miguu, thanks Lunyungu! Lakini tusiishie hapa hii ni hatari kwa nchi maskini kama tz inayotegemea zaidi ya 40% ya budget kwa misaada.

Kunahitajika mawazo ya way forward baada ya kutoa uchafu huu hawa jamaa ninavyojua watanyamaza na kuendelea kuzungumzia uzuri tu.

Kuna haja ya kutaka uchunguzi zaidi na waliohusika kutaja hizo pesa zimepelekwa wapi pia makampuni hasa yalikuwa ya nani?

Mimi nafikiri tuwapongeze sana walioweza kutufumbua macho kuhusu uchafu huu.

Pamoja na kwamba kuna wanaosema hizi kelele haziwanyimi usingizi lakini wajue wamekalia moto.
 
Back
Top Bottom