Chadema CUF TLP NCCR - LIVE from Urafiki Social Hall

Patamu hapo!!! sasa huo ni upande mmoja, nina hamu kusikia upande wa pili ukijibu objectively.

Nachukia mtu mmoja mmoja au taasisi ya aina yoyote inayojibu mambo ya msingi kijumla jumla tu, especially pale muuliza swali au mshutumu anapokuwa amelenga mambo specific.

NB: Ninachoweza kusema huenda ni kamchezo ka muda mrefu sana, sasa kamefikia mwisho wake!
 
Hapa sasa ni patamu sana kwani mkutano wao mkuu ni hapo kesho kutwa sasa naona hili kombora la pili limelenga pale panapostahili .

Ila tatizo ni pale unapokuta kuwa hata usalama wa taifa wamelipwa pesa za ufisadi .

Naona hapa wanaweza sasa kujitokeza na kusema kama ni kweli aqma laa ila kama ilivyuo kuwa wanazo hata cheki zilizotumika hakuna jinsi.
 
kilitime,

sina uhakika kama upande wa pili utaweza kutoa majibu ya hizo tuhuma/shutuma, labda ambacho wanachoweza kufanya ni kutoa blanket statement itakayo-cover yote. jibu lililo rahisi kwao ni kusema kwamba walishatoa ufafanuzi bungeni au walijibu wakati ule wa list ya mafisadi na huo ndiyo utakuwa mwisho wa mchezo.

Ni kweli unaweza kuwa mchezo wa muda mrefu na inawezekana siri hizo zimevuja kutokana na mambo tunayoyaona sasa yakitokea na hivyo kuna watu wamevujisha siri za namna ambavyo mchezo mchafu huwa unafanyika.

Swali langu ni moja, hizo details za kibenki wapinzani wanawezaje kuzi-access wakati huwa ni siri kati ya benki na mteja wake? Nadhani mambo yamekuwa magumu na kwanini hizo account zote ziende kufunguliwa NBC? Kwanini wasifungue kwenye benki nyingine?

Kama wapinzani wanahisi kwamba fedha hizo zilitumika kwa ajili ya kampeni, je, JK na vyombo vyake vya dola vitakubali kufanyia kazi hizo tuhuma? Bado ninaona kuna utete wa aina fulani kwenye hili swala na liko complicated kwa kiasi fulani. Hao waliotoa tuhuma hizo bado wana kazi ya ziada nadhani wanahitaji kwenda mbali zaidi ili kuweza kupata majibu yanayoeleweka, vinginevyo tutasikia blanket statement na huo ndiyo utakuwa mwisho.
 
Inasikitisha sana, Naomba kila mpenda Tanzania ajitahidi kufikisha ujumbe huo hapo juu kwa kila anayemfaham, yaani mimi sasa niko busy na email nawa-forwardia Wa-TZ wenzangu popote walipo duniani waone jinsi tunavyonyogwa mchana kweupeee.

naomba tujiulize maswali yafuatayo
1. ikiwa maskini wa mtaani akiiba pesa kidogo tu kama elfu kumi anapigwa na wananchi wenye hasira, je hawa wanaoiba mabilion ya walipa kodi tuwafanyeje? hawaoni huruma?

2. je hivi watanzania wanafaham kama pesa za umma ni zao na inatakiwa ziwahudumie wao na si vinginevyo, mi nafikiri inatakiwa ifanyike kampeni rasmi kuwaelimisha watanzania wote nini maana ya pesa za umma na nini chanzo chake, ninasema hivyo kwa sababu ninawasiwasi watu hawajui pesa za umma ni zao na wanapaswa kuwa na hasira sawa na pale wanapoingiliwa na wezi

thanks, ila nimekasirika sana duuu, mtu unapata kamshahara kadogo bado ushuru wanakata kibao, ok, basi huo ushuru utusaidie kwenye shughuri za kijamii na sio kuneemesha wachache ambao tayari ni matajiri???!!!
 
Mungu anapaswa sasa kuingilia klati.

Kuhusu ufunguzi wa account zote NBC nafikiri ni kutokana na jinsi benk husika ilivyobinafsishwa na pia benki nyingine ni ya huko afrikia ya kusini hivyo kuwa rahisi kufanya transactions zao.

Kuna haja ya kufuatilia kwa kina juu ya hii benki ya NEDBANK kwani huenda inafanya biashara chafu sana hapa afrika .
 
Inasikitisha sana, Naomba kila mpenda Tanzania ajitahidi kufikisha ujumbe huo hapo juu kwa kila anayemfaham, yaani mimi sasa niko busy na email nawa-forwardia Wa-TZ wenzangu popote walipo duniani waone jinsi tunavyonyogwa mchana kweupeee.

naomba tujiulize maswali yafuatayo
1. ikiwa maskini wa mtaani akiiba pesa kidogo tu kama elfu kumi anapigwa na wananchi wenye hasira, je hawa wanaoiba mabilion ya walipa kodi tuwafanyeje? hawaoni huruma?

2. je hivi watanzania wanafaham kama pesa za umma ni zao na inatakiwa ziwahudumie wao na si vinginevyo, mi nafikiri inatakiwa ifanyike kampeni rasmi kuwaelimisha watanzania wote nini maana ya pesa za umma na nini chanzo chake, ninasema hivyo kwa sababu ninawasiwasi watu hawajui pesa za umma ni zao na wanapaswa kuwa na hasira sawa na pale wanapoingiliwa na wezi

thanks, ila nimekasirika sana duuu, mtu unapata kamshahara kadogo bado ushuru wanakata kibao, ok, basi huo ushuru utusaidie kwenye shughuri za kijamii na sio kuneemesha wachache ambao tayari ni matajiri???!!!

Na pia waeleze watanzania wote kuhusu JF. Hii itakuwa faida pia kwa JF na watanzania Wote
 
Hapo ndipo hawa viongozi wa upinzani wanapokosa mwelekeo, siku ya leo ambayo ni siku ya uchaguzi wa kata 16 za udiwani sehemu mbalimbali za nchi, badala ya wao kuwa huko wapo busy na sera za kutupisha "makombora" it sound they have got their priorities up-side down.

Kesho ikitangazwa CCM imeshinda kata zote wataibuka na kusema ooh tumeibiwa kura! upuuzi kama huu ndio unaowafanya credibility yao kwa wananchi iupungue na ku-resort kwenye sera za kuzomea.

Walianza vizuri kwa kupanga kuachia kata vyama mbalimbali, na wakasema watafanya kampeni ya pamoja kuelekea chaguzi hizi, sasa cha ajabu wakati wote wa kampeni wote wapo Dar busy na kurusha makombora ya mafisadi. Mzee wangu aliwahi kuni hadithia zamani kuwa ukiona mtu ana kukimbiza muda mrefu na mara anaanza kurusha matusi na vitisho basi ujue kishaishiwa pumzi huyo sasa anatapatapa, katika hili nadhani wapinzani ni sawa na huyo mkimbizaji alieishiwa pumzi..

Haya endeleni kusubiri yatakayojiri huko urafiki mimi nasubiri matokea ya chaguzi za Majengo-Songea, Katazi, Kabwe, Namanyere nk.
 
Kwani umeambiwa kuwa ni lazima slaa aende huko?
Hapa unaonekana kama hujui maana ya mgawanyo wa madaraka .

Kwa taarifa tuu ni kuwa Zitto yupo ARusha akisimamia zoezi husika.

Rukwa yupo Said Arf mbunge pamoja na msafiri mtemelwa afisa mwanadamizi kampeni na uchaguzi.

Na Songea kapangiwa Edson Mbogoro ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema sasa sijui wewe unataka iweje kwenye jambo hilo.

Naambiwa pia kuwa wametuma timu za makao makuu kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za uchaguzi.

Cuf naambiwa pia wametuma timu za makao makuu, lwakatare,mwanza,mmasi tunduru akiwa na mazee Rajabu n.k

Tlp naambiwa kuwa wao wametuma timu pia kule arusha n.k.

Masatu no research, no data no right to speak.
 
mie nimeshawaambia hawana chao, na weshalijua hilo, hawa kazi yao kumwaga sumu tu, lkn wananchi wa tanzania wako macho sana hadi masaa ya usiku.

na safari hii watajua nani washenga wa mabibi zao
 
Kwani umeambiwa kuwa ni lazima slaa aende huko?
Hapa unaonekana kama hujui maana ya mgawanyo wa madaraka .

Kwa taarifa tuu ni kuwa Zitto yupo ARusha akisimamia zoezi husika.

Rukwa yupo Said Arf mbunge pamoja na msafiri mtemelwa afisa mwanadamizi kampeni na uchaguzi.

Na Songea kapangiwa Edson Mbogoro ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema sasa sijui wewe unataka iweje kwenye jambo hilo.

Naambiwa pia kuwa wametuma timu za makao makuu kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za uchaguzi.

Cuf naambiwa pia wametuma timu za makao makuu, lwakatare,mwanza,mmasi tunduru akiwa na mazee Rajabu n.k

Tlp naambiwa kuwa wao wametuma timu pia kule arusha n.k.

Masatu no research, no data no right to speak.

Mpaka Kieleweke,

Mlipoanza kuzunguka nchi nzima kunadi ufisadi wa CCM mliktuahidi kuwa kwa mwendo huo huo ndio mtafanya kampeni za udiwani.

Sasa kwa mujibu wa posts za awali za Lunyungu top brass lote la vyama vya "ushindani" wakiingia ukumbini urafiki wakiwo Slaa, Mnyika, Lissu etc.

Sasa tunapozungumza kuweka vipa umbele kisengele nyuma ndio huko, wakati leo ndio siku ya uchaguzi badala ya nguvu zote kuzielekeza huko mnapiga soga kwenye mkutano wa "ndani" ambao mngeweza kufanya next week end, MkapaKieleweke siasa halisi zipo on the ground na sio urafiki wekeni vipa umbele vyenu vizuri.
 
Masatu na wenzio nadhani kuna mahali unatakiwa ufike uwaze vyema.Hivi Chama ni hawa akina Slaa pekee ? Huu nadhani ni ugonjwa pekee uko CCM ambao wapinzani wanapashwa kubadilika na kudhani kwamba wasipo kuwepo wao kazi haitafanyika .
Now tuendelee na mjadala wa maana .Mbona hujagusia haya yaliyo wekwa hapa ?Mkataba wa Richmond nitauweka hapa baadaye .
 
Lunyungu sijasema Dr Slaa pekee ndio chama, unapotosha kwa makusudi. Rejea post yangu ya awali na soma btw the lines upate ujumbe mpana uliomo kwenye post.

Nasisitiza kipi muhimu kugawa mkataba wa Richmond (ambao already mlishagawa b4 na upo mitandaoni) na kwenda ku fight kupata viti vya udiwani? Haoni kama mnaanza kuishiwa gesi? ule moto mlioanza nao wa kuzunguka na helikopta kutangaza ufisadi nchi nzima kwani Slaa alikuwemo? je hamuoni nusu tu ya nguvu ile mngeitia where it matters most ( kwenye chaguzi kama hizi) si walau mngeambulia walau kiti kimoja?

Hivi kweli mko makini na siasa au mnacheza?
 
kobole kobole, mliojificha tunawaona.

lunyungu tusaidie matokeo mwisho yatakuwa ngapi ngapi?

bwana zitto alianza moja sufuri na sasa yako 1 kwenu na 2 mbili CCm

jee at the end ngapi ? au mshashinda vyote ndio mmeamua kuja furaha kurelax?

au mnapanga kuja kutueleza ufisadi uliotokea kwenye uchaguzi? maana si hasha mkatujia hapa uchaguzi haukuwa fair na free ila tunakusubirini tukusuteni, tena kwa masinzi mwaka huu

MAFISADI WA KUUZA UHURU WA NCHI YETU>

MAFISADI WA KUDUMAZA MAENDELEO YA TAIFA>

BAADA KUKAA NA KUTAFAKARI TUFANYE NN TUSONGE MBELE NYIE DAIMA MNAWAZA NI JINSI GANI KUINGIZA NCHI KWENYE BALAA
 
Lunyungu sijasema Dr Slaa pekee ndio chama, unapotosha kwa makusudi. Rejea post yangu ya awali na soma btw the lines upate ujumbe mpana uliomo kwenye post.

Nasisitiza kipi muhimu kugawa mkataba wa Richmond (ambao already mlishagawa b4 na upo mitandaoni) na kwenda ku fight kupata viti vya udiwani? Haoni kama mnaanza kuishiwa gesi? ule moto mlioanza nao wa kuzunguka na helikopta kutangaza ufisadi nchi nzima kwani Slaa alikuwemo? je hamuoni nusu tu ya nguvu ile mngeitia where it matters most ( kwenye chaguzi kama hizi) si walau mngeambulia walau kiti kimoja?

Hivi kweli mko makini na siasa au mnacheza?

Masatu

Wewe uliingiziwa ngapi kwenye account yako?

Suala waliloongelea hapa ni suala kubwa sana kuliko hata diwani sijui wa kata ya kabale ambaye hata hivyo bila kuondoa kigingi kinachosumbua ambao ni mafisadi hawezi kuleta maendeleo Tanzania.

Lazima zitengeneze njia mhafaka wa kuleta maendeleo, wakati watu wanapigwa jua kuomba kula watu wana download pesa BoT mithili ya files kutoka internet.

Lazima tumalizane na MAFISADI kabla ya mengine.
 
Kakindomaster,

Wewe Chadema wamekuingizia ngapi?

Sijakataa linaloongolewa ni jambo kubwa, unahitaji EC 100 kujua kuwa kupanga priorities kwa Scale of preferences, sasa huo hayo yanayofanyika Urafiki mngeyafanya wiki ijayo au wiki iliyopita ili leo muelekeze nguvu kwenye chaguzi hizi.

Unaposema udiwani sio muhimu unakosea sana huko mkuu ndio kwenye grassroot na foundation ya siasa kama kukilegea huko huwezi kupata ubunge na halafu urais na hilo ndio kosa mnalo fanya kila siku.

Badala ya kurekebisha mko na mambo ya name calling sijui umeingiziwa ngapi, umenunuliwa, umetumwa .... haya sie yetu macho!
 
Kama matumizi ya amani na utulivu wa watanzania ndio haya, kigogo gani ataacha kuhubiri hii amani?
 
Kwani umeambiwa kuwa ni lazima slaa aende huko?
Hapa unaonekana kama hujui maana ya mgawanyo wa madaraka .

Kwa taarifa tuu ni kuwa Zitto yupo ARusha akisimamia zoezi husika.

Rukwa yupo Said Arf mbunge pamoja na msafiri mtemelwa afisa mwanadamizi kampeni na uchaguzi.

Na Songea kapangiwa Edson Mbogoro ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema sasa sijui wewe unataka iweje kwenye jambo hilo.

Naambiwa pia kuwa wametuma timu za makao makuu kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za uchaguzi.

Cuf naambiwa pia wametuma timu za makao makuu, lwakatare,mwanza,mmasi tunduru akiwa na mazee Rajabu n.k

Tlp naambiwa kuwa wao wametuma timu pia kule arusha n.k.

Masatu no research, no data no right to speak.

Great; toa shule mwanangu! Good work, keep it up!
 
Back
Top Bottom