Chadema CUF TLP NCCR - LIVE from Urafiki Social Hall

Chadema CUF TLP NCCR - LIVE from Urafiki Social Hall

Mdogo wangu John Mnyika,

Naomba nikusifu kwa propaganda, Hongera sana mkuu,,, maana hizo statistics, ukizisoma kwa kweli Utaona Upinzani Umeshinda saaaana!!! Lakini Ungeweza tu kutulia ukatupatia wakati viti ni 10 hadi 20 at least ungeweza kufanya sisi wengine tulibahatika kusoma kwenye shule za kalimanzira kuwapa Hongera ya Halali Kwenu...

Ni sawa sawa na kipima Joto cha ITV kinachotoa statistics za percentage bila kusema washiriki ni wangapi!!!

Tunaomba usitulazimishe kuamini kwamba Upinzani kwa uwezo wa kufikiri, kuchambua hakuna clear differentiation other than kwamba huko ni Mnyika na kule ni Tambwe,,,, please!!!

Kilitime,

Mnyika hajui kwamba wenzake Propaganda huwa wanasomea, kama anataka kuwa propagandist mzuri aende akasome.

Naona Propaganda zake nyingi, hata mwanafunzi wa shule ya msingi anaweza kuziona.

Hizi SPIN zimewashinda hata watu makini kama akina Blair.

Mimi na SPIN mbalimbali.
 
Mtanzania

Asante kaka.

Nami naamini: STRATEGY is better than SPIN.

Nimetoa FACTS tu, na nimeahidi nikipata matokeo mengine nitayaleta.

Hakuna Kulala...

JJ
 
Mwanakijiji,

Let me put it this way, kwako wewe na mimi ni rahisi sana kuelewa, kwa Mwingine ni tatizo. Mfano ngoja ni spin hiyo taarifa yao:

"Hawa wapinzani waongo kabisa, hawa lengo lao ni kuleta machafuko hapa nchini, mmenisikia wananchi? wakataeni, wanachekesha kweli eti juzi juzi wanasema hela zimelipwa na BOT kwenda kakampuni flani halafu wana cheque namba na tarehe lakini hawajui hela zilienda wapi au zilitumikaje, jamani huu si uongo jamani?, utapataje cheque na husijue hela zimeenda wapi au zimetumikaje, hawa ni wa kupuuza kabisa, CCM hoyeee! CCM hoyeee!"

Hapo ninawahutubia watanzania walalahoi hawajui hata cheque inaonekanaje, kosa dogo tu la kutomalizia ninaweza kuli CAPITALIZE.

Watakuzomea. Watanzania wa juzi sio wa leo, wanaona, wanagusa, wananusa na wanatafakari sana. Wametoka huko kitambo. Those days are gone, trust me. Na CCM wanalijua hili ndio maana siku hizi inawawia vigumu hata kuitisha mikutano ya hadhara. Bahati kubwa walionayo wapinzani sasa hivi ni kwamba wanasikilizwa kuliko CCM!
 
Those days are gone, trust me. Na CCM wanalijua hili ndio maana siku hizi inawawia vigumu hata kuitisha mikutano ya hadhara. Bahati kubwa walionayo wapinzani sasa hivi ni kwamba wanasikilizwa kuliko CCM!

Kitila Mkumbo,

Well said!!!

Nakuaminia Kitila; ingawa nina mashaka kwamba uko on the right place at the right time!!!
 
Mtu wa Pwani,
si ndo wee ulikuja na shairi hili...

wako wapi marijali????????????????

wako wapi marijali katika hii tanzania
wanaopenda adili haki wanopigania
wanochukia madhili wanotendewa raia

-------------------------------------------

wako wapi marijali wale tulowasikia
kwa kali zao kauli bungeni wakizitoa
sioni hata kivuli wapi wametokomea
------------------------------------------

wako wapi walonena wanyonge taangalia
kwa marefu na mapana wakawa wajinadia
kumbe maana hawana kweli inapowadia
----------------------------------------------

wako wapi viongozi nchi tulowaachia
mbona hawatendi kazi ambazo walitwambia
wazishusha zao hadhi na kuondoa murua
------------------------------------------------

suala nnauliza majibu nipatieni
haya yananitatiza yananighasi moyoni
au wamepatilizwa hawasikii hawaoni

Leo

hata matokeo bado unatoa excuse eeh. si mlisema CCM kwisha sasa mnasema ujumbe haujafikia wananchi vijijini.

kwani mliowafundisha kuzomea walikuwa wananchi wa mjini?

nyie endelezeni fitna na kuigawa nchi kwa kumbandika huyu fisadi huyu mkombozi.

sisi tuko karibu na wananchi kutatua shida zao.nyinyi ukaribu wenu na fitna na ubinafsi endeleeni na sambazeni chuki lkn mpanda shari huvuna shari

Ni mie nakosea kuelewa au ushabadili mwelekeo?
Hao ulowaulizia "kwa kali zao kauli bungeni wakizitoa
sioni hata kivuli wapi wametokomea"
ndo hao wanatoa data za ufisadi!
 
Watakuzomea. Watanzania wa juzi sio wa leo, wanaona, wanagusa, wananusa na wanatafakari sana. Wametoka huko kitambo. Those days are gone, trust me. Na CCM wanalijua hili ndio maana siku hizi inawawia vigumu hata kuitisha mikutano ya hadhara. Bahati kubwa walionayo wapinzani sasa hivi ni kwamba wanasikilizwa kuliko CCM!

Kitila,

Good Observation. Ila kumbuka mimi ninapoelezea Cheque kwao ninaiweka nitakavyo, ninaielezea kuwa ni doc inayoonyesha mambo yote, kwahiyo upinzani hawajaona hiyo cheque wala nini wame spin tu. Levels kaka, Level za watu unaoongea nao ina matter sana, JF hapa Mtanizomea YES, lakini mwanerumango hawatanizomea.

Unafikiri wapiga kura wapo wapi! ni walalahoi vijijini kaka. Hao hata ukisema hela zimeibiwa hawakuelewi, unless uelezee hizo hela zina uhusiano gani na maisha yake anayoishi.

Najua unajua kuwa mimi najua unajua kuwa siasa ni Propaganda, tatizo mimi sio mzuri sana huko, ila ukimpata mwenyewe, mnashindwa!
 
Kitendo cha kuunda makampuni hewa na kula pesa za wananchi Mungu ndiye atakayeamua na ipo dalili kuwa Mungu anaingilia kati wizi huu subiri muone nyakati zinzonyesha

Waliofunuliwa wanaona lakini wasiofunuliwa haya maono hawawezi kuona watabaki kulala usingizi

Usichezee mali za wavuja jasho ndugu zanguni wote hao waliokula hizo pesa mioyoni mwao sasa hakuna amani hata kidogo; investiment, pesa zilizoko ktk mabenki hasa ya nje na madaraka waliyonayo wameyapata kwa kudhurumu mtu wa chini hawana furaha nayo na hayatawasaidia kamwe,

wanaiba ili kusomesha watoto wao nje lakaini wengi wao wanarudi wakiwa mateja, mtoto silizi, na hawana hata uwezo wa kuiendeleza miradi yao bali visu nje nje kwa wazazi wao.

Watanzania kaeni mkao wa kula saa ya ukombozi imefika ambapo hata yule mtoto wa masikini sasa ataingia BOT hata ikulu maana kura kwa pesa inakwisha

Someni nyakati Mungu akisema au hapana ndiyo hakuna atakayepinga chini ya mbingu.

Walio na ufunuo wanaona

CCM rudini mkarudie Mungu msione raha kuendesha mashangingi ya pesa za wananchi yatawamaliza. Mungu siku zote si wamchezo anaweza kukaa kimya siyo kwamba hakuoni anakuona sana ila anakupa muda ujirekebishe.

Mungu uvumilivu umemshinda sasa kaeni tayari
Laiti mngelijua mngemrudia leo maana yeye ni mema mkaenenda ktk njia zake

Umoja wa vyama vya siasa nawashauri muanze kuunda baraza la mawaziri, pelekeni wajenius bila kujali ni mtoto wa mlala hoi au la wakasome nje ili mpate wataalamu wauhakika

Vyuo vyetu vya Tz vimejaa makada na mafisadi mitaala inatengenezwa ili kufeva siasa pekee mkitaka kujua tafuteni mitaala wanayofundishwa kitivo cha Engineering pale UDSM ndiyo mtaelewa niayosema.
Mungu siku zote yuko na mtu mwenyehaki msiogope
 
hata matokeo bado unatoa excuse eeh. si mlisema CCM kwisha sasa mnasema ujumbe haujafikia wananchi vijijini.

kwani mliowafundisha kuzomea walikuwa wananchi wa mjini?

nyie endelezeni fitna na kuigawa nchi kwa kumbandika huyu fisadi huyu mkombozi.

sisi tuko karibu na wananchi kutatua shida zao.nyinyi ukaribu wenu na fitna na ubinafsi endeleeni na sambazeni chuki lkn mpanda shari huvuna shari

Sisi tuko karibu na wananchi kutatua shida zao.......

When you say this with a straight face; knowing what has become of the esterwhile 'revolutionary party' you must be heavily invested in the entire plot.
 
Kitila,

Good Observation. Ila kumbuka mimi ninapoelezea Cheque kwao ninaiweka nitakavyo, ninaielezea kuwa ni doc inayoonyesha mambo yote, kwahiyo upinzani hawajaona hiyo cheque wala nini wame spin tu. Levels kaka, Level za watu unaoongea nao ina matter sana, JF hapa Mtanizomea YES, lakini mwanerumango hawatanizomea.

Unafikiri wapiga kura wapo wapi! ni walalahoi vijijini kaka. Hao hata ukisema hela zimeibiwa hawakuelewi, unless uelezee hizo hela zina uhusiano gani na maisha yake anayoishi.

Najua unajua kuwa mimi najua unajua kuwa siasa ni Propaganda, tatizo mimi sio mzuri sana huko, ila ukimpata mwenyewe, mnashindwa!

Nakubali mkuu. Lakini hao wakulima wa vijijini si ndio waliowazomea mawaziri wetu walipoenda juzi ku-spin kuhusu Buzwagi na hizi kashafa za Bo au siyo? Ndio nikasema pengine huwa tunawa-underestimate wananchi waliopo vijijini. Mimi tangu nianze kuandika makala kwenye magazeti na kupokea maoni ya wananchi kwa njia ya simu na sms tena kutoka vijijini nimebadilisha sana mwelekeo wangu kuhusu hawa wananchi. Actually, siogopi kukuambia kwamba inapokuja swala la uelewa na ujasiri wa kisiasa wananchi wa vijijini na walala hoi wanatuzidi mbali sana ujanja sisi tunaofikiri tunajua!

Nimejifunza pia kwamba ukiongea kitu ambacho wananchi kinawahusu watakusikiliza kwa makini na kukupenda. Hiki ndicho kilichotokea kwa Zitto, Slaa na wapinzani wengine. Kwa muda mrefu wapinzani walikuwa wanaongea mambo ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moha na maisha ya wananchi. Kwa mfano uking'ang'ania tu madai ya Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi bila kuonyesha ni namna gani haya mambo yanaathiri maisha yao ya kila siku, watakusikiliza kisha wanakuacha kama ulivyo wakikuona wewe ni mwanasiasa kama walivyo wengine katika CCM. Lakini pale ambapo wapinzani wameweza kuonyesha jinsi mali zao zinavyoibwa kwa kutumia katiba na sheria mbovu, sasa wananchi wameanza kushtuka na kuwaona wapinzani kama sehemu ya wao zaidi kuliko hao CCM.

Bado safari ni ndefu huko tuendeako, lakini tusisahau pia kwamba tumetoka mbali. Hii safari tutaikamilisha kwa sisi sote kutekeleza wajibu wetu na sio kufikiri kwamba kazi ya ukombozi wa nchi yetu ni ya wapinzani pekee. Tumeshaliona tatizo, ambalo ni CCM, sasa lazima sote tushirikiane kulimaliza. Akina Mrema na akina Zitto pekee hawataweza, especially pale ambapo kuna kambezo! This is how our colleagues in Kenya managed; by coming together to fight a common enemy, KANU. They won the battle and the victory now belongs to people for ever. And the victory I am talking about here is the people's power to change the government in a ballot box. Hii ndio sisi tunakosa. Tunataka wananchi tuwe na uwezo wa kubadilisha serikali pale ambapo tunataka. Tuwe tuna uwezo wa kuwafukuza CCM madarakani na kuwaweka wengine, hawa wengine nao (wawe CHADEMA, CUF whoever), wakichemsha, tunawatoa na kuwaweka wengine. Lakini sasa ni kama vile wananchi hatuna ujanja hata kama CCM watakosea kiasi gani ni kama vile hatuna ujanja. Huu ndio ugonjwa namba moja tulio nao kama nchi, na kuushinda huu ugonjwa tunahitaji juhudi za pamoja na sio kufikiri kwamba akina Mrema pekee ndio kazi yao.

Pole nimeeda zaidi ya mada yenyewe, tatizo naandika kama naongea!
 
Kazi ni kubwa na safari ni ndefu sana . watu wa kijiji kiasi kasi ya uelewa inaanza kuwaingia lakini bado Wapinzania they should go there and talk to them .
 
Kunahitajika mawazo ya way forward baada ya kutoa uchafu huu hawa jamaa ninavyojua watanyamaza na kuendelea kuzungumzia uzuri tu.

Kwa kweli tumekwisha. Lakini nani wa kulisemea hili? Majuzi nimeona kuna baadhi ya vyombo vya habari kama ze comedy wameshapewa hela waanze kumpiga vita Slaa sasa nani ataendeleza hili la kupiga kelele?
Ila nashauri wana JF tusiishie tuu kusema kwenye hii forum totoke nje tuwaambie watu nini kinachoendelea kwa wale wenye uwezo wa kuprint vitu kama hivi ni vizuri waprint wawape watu hii ndio njia pekee ya kusambaza ujumbe. Vyombo vyote vya habari vimeshanunuliwa kwa hiyo tusivitemee sana..
 
WanaJF,

Mimi ni CCM damu damu. Ninaomba kuuliza na kuchangia.

Hizi fedha za Deep green (ita rangi ya chama) mnajuaje zilienda kwenye uchaguzi na zilitumiwa na CCM?

La pili, nikisema kuwa hizi pesa zililiwa na wajanja wachache na wala wana CCM hawajui hilo mtakataa?.

Hivi Karamagi ni mmoja wa wamiliki wa TICS au TISS? nataka kujumlisha 2 na 2 nipate NNE.

Ninachomaanisha ni kuwa tuzipe hizi habari nafasi na sisi tutafakari. Inawezekana kabisa mkurugenzi asielewe fedha zimepelekwa wapi (Tangold Ltd) kwa sababu si mmiliki wa kampuni husika. Hivyo kuwajumlisha wakurugenzi wote wa Tangold Ltd sio HAKI.

Ninawapa changamoto Wapinzani kuacha kusema uongo, huwezi kupata cheque number na tarehe ukashindwa kujua hela zilienda wapi. This is a political stunt, hela zilikoenda mnajua na inajulikana, zilivyotumika ndio tatizo.
Come up wapinzani, sio wananchi wote tunatazama upande mmoja wa sarafu.

Labda wewe uliyetazama huo upande mwingine wa shilingi unaweza kusema kuwa hizi pesa zilienda wapi! Mhh, kwako hii habari ya wizi huu ni uongo? ama kweli kazi ipo
 
Bado safari ni ndefu huko tuendeako, lakini tusisahau pia kwamba tumetoka mbali. Hii safari tutaikamilisha kwa sisi sote kutekeleza wajibu wetu na sio kufikiri kwamba kazi ya ukombozi wa nchi yetu ni ya wapinzani pekee. Tumeshaliona tatizo, ambalo ni CCM, sasa lazima sote tushirikiane kulimaliza. Akina Mrema na akina Zitto pekee hawataweza, especially pale ambapo kuna kambezo! This is how our colleagues in Kenya managed; by coming together to fight a common enemy, KANU. They won the battle and the victory now belongs to people for ever. And the victory I am talking about here is the people's power to change the government in a ballot box. Hii ndio sisi tunakosa. Tunataka wananchi tuwe na uwezo wa kubadilisha serikali pale ambapo tunataka.

Kwa mtizamo wa mwanaCHADEMA hapo uko right kabisa kwa mtizamo wa mwananchi mzalendo mwingine asiye mwanachama,,, issue sio kuitoa CCM au chama tawala,,, issue ni kuwa na mechanism ambayo itafanya chama tawala kufanya kazi yake... na hii ni rahisi katiba nzuri na idadi ya wawakilishi wa ratio ya at least 3:7, 4:6

Kwa nchi ya vyama vingi, kila siku kutakuwa na chama tawala na vyama pinzani,,, na sidhani wewe utakuwa upinzani muda wote, kuna siku mtakuwa madarakani,,, sasa sikweli kwamba wakati wote walioko madarakani si sahihi ni wale ambao hawako madarakani watoke [BIG NO] sikubaliani na hilo.

Tuwe tuna uwezo wa kuwafukuza CCM madarakani na kuwaweka wengine, hawa wengine nao (wawe CHADEMA, CUF whoever), wakichemsha, tunawatoa na kuwaweka wengine. Lakini sasa ni kama vile wananchi hatuna ujanja hata kama CCM watakosea kiasi gani ni kama vile hatuna ujanja. Huu ndio ugonjwa namba moja tulio nao kama nchi, na kuushinda huu ugonjwa tunahitaji juhudi za pamoja na sio kufikiri kwamba akina Mrema pekee ndio kazi yao.
Mimi nadhani ujanja tunao ila unakuwepo tu, tukiwa makini, kwa mfano ni viongozi wa upinzani wangapi walihakikisha Njelu Kasaka harudi CCM?,,,

Lakini wale wajanja wanaotuongoja ndio sio watu wa kuaminika,,, watu makini bado hawako upinzani and it is your responsibility ya mtu makini kama wewe kuweka mazingira wakufuate wengine... usiache wababaishaji ndio wawe mbele otherwise we will never meet those objectives...

Sasa Angalia Mheshimiwa Kitila Anaongea na Watu hapa JF ambao they have access to assess things and to make up their mind, muheshimiwa Mnjika anadhani atapata wapiga kura humu JF. wapi na wapi bwana...
 
Kwa mtizamo wa mwanaCHADEMA hapo uko right kabisa kwa mtizamo wa mwananchi mzalendo mwingine asiye mwanachama,,, issue sio kuitoa CCM au chama tawala,,, issue ni kuwa na mechanism ambayo itafanya chama tawala kufanya kazi yake... na hii ni rahisi katiba nzuri na idadi ya wawakilishi wa ratio ya at least 3:7, 4:6

Kwa nchi ya vyama vingi, kila siku kutakuwa na chama tawala na vyama pinzani,,, na sidhani wewe utakuwa upinzani muda wote, kuna siku mtakuwa madarakani,,, sasa sikweli kwamba wakati wote walioko madarakani si sahihi ni wale ambao hawako madarakani watoke [BIG NO] sikubaliani na hilo.

Mimi nadhani ujanja tunao ila unakuwepo tu, tukiwa makini, kwa mfano ni viongozi wa upinzani wangapi walihakikisha Njelu Kasaka harudi CCM?,,,

Lakini wale wajanja wanaotuongoja ndio sio watu wa kuaminika,,, watu makini bado hawako upinzani and it is your responsibility ya mtu makini kama wewe kuweka mazingira wakufuate wengine... usiache wababaishaji ndio wawe mbele otherwise we will never meet those objectives...

Sasa Angalia Mheshimiwa Kitila Anaongea na Watu hapa JF ambao they have access to assess things and to make up their mind, muheshimiwa Mnjika anadhani atapata wapiga kura humu JF. wapi na wapi bwana...

Unataka kupata things both ways!

Issue kubwa hapa ni hao watu "makini" unaosema wewe kuwa wako sisiemu wameiba mabilioni ya pesa za wananchi. Standard ipi zaidi ya umakini utaweka hapa?

Kuhusu Mnyika na Mkumbo kuwa JF, je ni makosa? these guys can be everywhere ili kutetea angalau kilichobaki kisiuzwe. Wao tayari wameanza kazi kupambana na ufisadi, na for now watanzania wako glad kuwa kuna mtu yuko msitari wa mbele kupigania maslahi yao ambayo wanaccm wanayauza kwa wakoloni kila siku!
 
Sasa Angalia Mheshimiwa Kitila Anaongea na Watu hapa JF ambao they have access to assess things and to make up their mind, muheshimiwa Mnjika anadhani atapata wapiga kura humu JF. wapi na wapi bwana...[/QUOTE]

Kilitime:

Unanikumbusha pale Kili Time sinza shekilango...a good please to be...kuna 'voters' tofauti usiku na mchana!(joke).

Anyway, siko hapa kutafuta kura-lakini nikizipata hewala. Mwenyewe umesema hapa JF kuna watu wenye kuweza kupata mambo kama wanaweza kupata mambo kwa nini huamini kama wanaweza kupeleka mambo hayo kwa watu. Na kama wapo humu wanaotoka ubungo, hata kama ingekuwa napiga kampeni kwanini hutaki kufiri kuwa watapeleka ujumbe kwa majirani zao na hatimaye kupata kura? Lakini nirudie, siko hapa kuomba kura- ukifika wakati wake nitaomba.

Niko hapa kuwasilisha fikra zangu mbadala na kupata fikra mpya! Niko hapa kupata ukweli na kusambaza ukweli. Kama nitatumia fursa hiyo vilevile kuwaomba wachangiaji na wasomaji kuunga mkono CHADEMA, ama kuunga mkono ukweli, ni sehemu tu ya kusimamia fikra mbadala ninaozoziamini.

Tuendelee kukata issues, salam toka msamvu. Nikifika matombo nitawapa salam zako pia

JJ
 
Mimi nadhani ujanja tunao ila unakuwepo tu, tukiwa makini, kwa mfano ni viongozi wa upinzani wangapi walihakikisha Njelu Kasaka harudi CCM?,,,

Lakini wale wajanja wanaotuongoja ndio sio watu wa kuaminika,,, watu makini bado hawako upinzani and it is your responsibility ya mtu makini kama wewe kuweka mazingira wakufuate wengine... usiache wababaishaji ndio wawe mbele otherwise we will never meet those objectives...

Sasa Angalia Mheshimiwa Kitila Anaongea na Watu hapa JF ambao they have access to assess things and to make up their mind, muheshimiwa Mnjika anadhani atapata wapiga kura humu JF. wapi na wapi bwana...

i) Siasa ni mapenzi ya mtu ndugu yangu. Vyama vya upinzani sio walinzi wa kuhakikisha watu hawarudi CCM. Ni jukumu la mtu mwenyewe kuamua anataka chama gani na yupo huru kuhama na kuhamia chama kimoja kwenda kingine wakati wowote. Kwa hiyo Njelu Kasaka alikuwa na hiari ya kutoka CCM na kurudi huko kama alivyofanya kwa jinsi akili yake ilivyomtuma. Kwa vyovyote vile upinzani haukupaswa kuwajibika na wala sasa hauwajibiki kumlinda Kasaka asirudi CCM. Hiyo ni juu yake.

ii) In the second issue, you are really missing the point. Binafsi sipo hapa kutafuta kura. This is not a vote fetching forum. We are exchanging views about the fate of our beloved country. Kama wewe upo hapa kukitafutia chama fulani kura, endelea lakini usifikiri na wengine tunafanya kazi hiyo.
iii) Niseme pia hili maana linajirudiarudia sana. Katika upinzani na hasa CHADEMA tunaamini katika tofauti ya mawazo, maadili na unyoofu. Hatuamini katika ghiliba. Kwa hiyo hatupo tayari kupata kura kwa ghiliba, na kama ghiliba ndio njia pekee ya kushinda uchaguzi Tanzania basi tupo tayari tubaki kuwa wapinzani milele! Tutauza mawazo yetu na wananchi watatupima kwa yale tunayoyafikiri, kusema na kuyatenda. Tunatekeleza wajibu wetu kama chama, uamuzi bado ni wananchi wenyewe.
 
Kwa mtizamo wa mwanaCHADEMA hapo uko right kabisa kwa mtizamo wa mwananchi mzalendo mwingine asiye mwanachama,,, issue sio kuitoa CCM au chama tawala,,, issue ni kuwa na mechanism ambayo itafanya chama tawala kufanya kazi yake... na hii ni rahisi katiba nzuri na idadi ya wawakilishi wa ratio ya at least 3:7, 4:6

Kwa nchi ya vyama vingi, kila siku kutakuwa na chama tawala na vyama pinzani,,, na sidhani wewe utakuwa upinzani muda wote, kuna siku mtakuwa madarakani,,, sasa sikweli kwamba wakati wote walioko madarakani si sahihi ni wale ambao hawako madarakani watoke [BIG NO] sikubaliani na hilo.

Mimi nadhani ujanja tunao ila unakuwepo tu, tukiwa makini, kwa mfano ni viongozi wa upinzani wangapi walihakikisha Njelu Kasaka harudi CCM?,,,

Lakini wale wajanja wanaotuongoja ndio sio watu wa kuaminika,,, watu makini bado hawako upinzani and it is your responsibility ya mtu makini kama wewe kuweka mazingira wakufuate wengine... usiache wababaishaji ndio wawe mbele otherwise we will never meet those objectives...

Sasa Angalia Mheshimiwa Kitila Anaongea na Watu hapa JF ambao they have access to assess things and to make up their mind, muheshimiwa Mnjika anadhani atapata wapiga kura humu JF. wapi na wapi bwana...

By far this is a very balanced opinion from kilitime. No partisan politics here.

CCM wanaelewa udhaifu uliomo katika vyama vya upinzani, ndio maana hawastuki pamoja na kuwa na mambo mazito haya yanayowakabili sasa hivi.
 
Silaha pekee wanayo jivunia CCM ni Pesa za kuhonga na FFU na wizi . Hawana la zaidi la kutegemea na huu ndiyo ukweli pekee .Hawana sera za kutekelezeka japokuwa ni safi .
 
Back
Top Bottom