Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,003
- Thread starter
- #41
Naomba niupeleke mjadala huu mbele zaidi:
Chama lengo lake ni kushinda uchaguzi na kutawala.
Vyama vya kisiasa vinaweza kuwa na malengo mbalimbali ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, n.k Lakini lengo la kwanza kabisa la kuweza kutekeleza malengo hayo mengine yote ni kushinda uchaguzi ili iweze kupata nafasi ya kutawala au kuongoza. Vyama vingine hata hivyo vina malengo ya kuleta issues mbalimbali to the forefront of public discussion ili vyama vikubwa viweze kujadili na kuadopt positions zake.
CCM imejiwekea lengo la kushinda uchaguzi kwenye Katiba yake tena ni lengo la kwanza, Chadema haina lengo hilo ingawa is presumed. Sasa kama lengo lake (chadema) ni kuleta mjadala wa ufisadi na mabaya ya CCM mbele ya wananchi basi ishiriki kila uchaguzi bila kujali matokeo yake. Mkakati wa namna hiyo una gharama kubwa sana kwani unaassume watu hawajui mabaya ya CCM.
Kukijenga Chama
Ninaamini Chadema imepoteza nafasi nyingi sana za kukijenga chama hicho; nafasi ambazo ingekuwa katika nchi nyingine wanasiasa wangekuwa wanazivujia udenda! Baada ya Tunduru, Chadema walifanya nini kuandikisha wanachama wapya Tunduru na kufungua matawi? Baada ya Kiteto walirudi lini na kufungua matawi na kujenga kada ya wanachama? Baada ya Mbeya Vijijini je? Vipi kuhusu Tarime? Na sasa Busanda?
Chadema lazima ijue inataka nini; kushinda uchaguzi au kufanya watu waichukie CCM ili wao washinde uchaguzi? Kushiriki Biharamulo ili kujaribisha ni kupoteza muda, raslimali na nafasi.
Nimejiuliza mara ya mwisho kuona Chadema wakiandikisha wanachama wapya jijini Dar ilikuwa lini? Mara ya mwisho wao kufungua matawi mapya au kuyaimarisha ya zamani ilikuwa lini?
Je ni kwa kiasi gani wanachama wa chini wanajua viongozi wao wamejitoa mhanga kweli katika kukijenga chama? Niwakumbushe vitu viwili ambavyo wengine kwenye historia yetu hawavikumbuki sana, Nyerere alipoamua kujiuzulu Uongozi wa serikali na kurudi kwenye TANU na kuanza ziara za vijijini mnafikiri alikuwa anafanya nini kule vijijini, kuelezea mabaya ya ukoloni?
Na baadaye 1971 alipoanza ziara za vijijini tena na kuzungumza na wananchi moja kwa moja alifanya vile kwa sababu gani?
Viongozi wa Chadema wanahitaji kuachana na siasa za magazeti bali kurudi moja kwa moja kwa wananchi. Ni matumaini yangu kuwa baada ya uchaguzi wao Mkuu wiki chache zijazo, wataaamua kujipanga kwenda vijijini siyo tena kwa Operesheni Sangara bali operesheni ya kujenga chama.
Wasipofanya hivyo, wasubiri kuona jinsi CCM ilivyo na uwezo wa kujijenga tena vijijini, kwani CCM ikitaka inaweza kuconcede majimbo ya miji michache (Moshi, Arusha, Mwanza, Dar, Mbeya na Tanga) na kuchukua majimbo mengine yote na hali haitabadilika isipokuwa nyongeza ya ruzuku kwa wapinzani.
So far CCM haijashindwa kwa hoja, itashindwa kwa mkakati. Subiri "Cheche" ya Ijumaa nitalifunua hili vizuri zaidi.