CHADEMA: Baada ya Biharamulo; Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010

Naomba niupeleke mjadala huu mbele zaidi:

Chama lengo lake ni kushinda uchaguzi na kutawala.
Vyama vya kisiasa vinaweza kuwa na malengo mbalimbali ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, n.k Lakini lengo la kwanza kabisa la kuweza kutekeleza malengo hayo mengine yote ni kushinda uchaguzi ili iweze kupata nafasi ya kutawala au kuongoza. Vyama vingine hata hivyo vina malengo ya kuleta issues mbalimbali to the forefront of public discussion ili vyama vikubwa viweze kujadili na kuadopt positions zake.

CCM imejiwekea lengo la kushinda uchaguzi kwenye Katiba yake tena ni lengo la kwanza, Chadema haina lengo hilo ingawa is presumed. Sasa kama lengo lake (chadema) ni kuleta mjadala wa ufisadi na mabaya ya CCM mbele ya wananchi basi ishiriki kila uchaguzi bila kujali matokeo yake. Mkakati wa namna hiyo una gharama kubwa sana kwani unaassume watu hawajui mabaya ya CCM.

Kukijenga Chama
Ninaamini Chadema imepoteza nafasi nyingi sana za kukijenga chama hicho; nafasi ambazo ingekuwa katika nchi nyingine wanasiasa wangekuwa wanazivujia udenda! Baada ya Tunduru, Chadema walifanya nini kuandikisha wanachama wapya Tunduru na kufungua matawi? Baada ya Kiteto walirudi lini na kufungua matawi na kujenga kada ya wanachama? Baada ya Mbeya Vijijini je? Vipi kuhusu Tarime? Na sasa Busanda?

Chadema lazima ijue inataka nini; kushinda uchaguzi au kufanya watu waichukie CCM ili wao washinde uchaguzi? Kushiriki Biharamulo ili kujaribisha ni kupoteza muda, raslimali na nafasi.

Nimejiuliza mara ya mwisho kuona Chadema wakiandikisha wanachama wapya jijini Dar ilikuwa lini? Mara ya mwisho wao kufungua matawi mapya au kuyaimarisha ya zamani ilikuwa lini?

Je ni kwa kiasi gani wanachama wa chini wanajua viongozi wao wamejitoa mhanga kweli katika kukijenga chama? Niwakumbushe vitu viwili ambavyo wengine kwenye historia yetu hawavikumbuki sana, Nyerere alipoamua kujiuzulu Uongozi wa serikali na kurudi kwenye TANU na kuanza ziara za vijijini mnafikiri alikuwa anafanya nini kule vijijini, kuelezea mabaya ya ukoloni?

Na baadaye 1971 alipoanza ziara za vijijini tena na kuzungumza na wananchi moja kwa moja alifanya vile kwa sababu gani?

Viongozi wa Chadema wanahitaji kuachana na siasa za magazeti bali kurudi moja kwa moja kwa wananchi. Ni matumaini yangu kuwa baada ya uchaguzi wao Mkuu wiki chache zijazo, wataaamua kujipanga kwenda vijijini siyo tena kwa Operesheni Sangara bali operesheni ya kujenga chama.

Wasipofanya hivyo, wasubiri kuona jinsi CCM ilivyo na uwezo wa kujijenga tena vijijini, kwani CCM ikitaka inaweza kuconcede majimbo ya miji michache (Moshi, Arusha, Mwanza, Dar, Mbeya na Tanga) na kuchukua majimbo mengine yote na hali haitabadilika isipokuwa nyongeza ya ruzuku kwa wapinzani.

So far CCM haijashindwa kwa hoja, itashindwa kwa mkakati. Subiri "Cheche" ya Ijumaa nitalifunua hili vizuri zaidi.
 
Wasipoenda Biharamulo wapinzani wetu (CCM) watasema wameogopa kushindwa na itaonekana hivyo kwa sababu in politics perception is more effective than reality. It will be too damaging politically for CHADEMA not participate in Biharamulo.

Cha kufanya hapa wale wote wenye kiu ya mabadiliko ya kisiasa nchini na wanaoamini kwamba chadema ni agent wa mabadiliko hayo tuwachangie ili tuongezee nguvu za ushindani wao huko Biharamulo. Ningeshauri kwamba mtu mmoja afungue thread ya harambee hapa ili watu waanze kuchanga!
 
Suala la kuchangia ni muhimu ila wananchi waliisha tishwa kuwachangia wapinzani, hasa upande wa wafanyabiashara. wakikugundua tu wanakufilisi kwa ku-over estimate Tax liability. Muulize Askofu wa Merelani Arusha na NCCR au Dr. Aziz pale Tabora alikuwa na hospital binafsi kwa kuwasapoti CUF wakamfilisi karudi CCM hivi sasa, SM Said pale Tabora alikuwa na duka la jumla nafikiri lilikuwa ni best pale Tabora miaka hiyo nipo pale alikuwa CUF wakamfilisi na mifano mingi tu.

Sasa ili wapinzani wapate support wanatakiwa kuuhakikishia umma kuwa wao si miongoni mwa branch za CCM ambazo ukiwachangia tu wanawaambia watu wa system na kuanza kuandamwa. Kuna watu wengi wangependa kuchangia bila kutaka kujulikana lakini je wapinzani wanaweza kuwastahi?. Jibu ni hapana kwani vyama vyote vya upinzani vina vinzi vya Othman.
 
Naomba niupeleke mjadala huu mbele zaidi:

Chama lengo lake ni kushinda uchaguzi na kutawala.
Vyama vya kisiasa vinaweza kuwa na malengo mbalimbali ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, n.k Lakini lengo la kwanza kabisa la kuweza kutekeleza malengo hayo mengine yote ni kushinda uchaguzi ili iweze kupata nafasi ya kutawala au kuongoza. Vyama vingine hata hivyo vina malengo ya kuleta issues mbalimbali to the forefront of public discussion ili vyama vikubwa viweze kujadili na kuadopt positions zake.

CCM imejiwekea lengo la kushinda uchaguzi kwenye Katiba yake tena ni lengo la kwanza, Chadema haina lengo hilo ingawa is presumed. Sasa kama lengo lake (chadema) ni kuleta mjadala wa ufisadi na mabaya ya CCM mbele ya wananchi basi ishiriki kila uchaguzi bila kujali matokeo yake. Mkakati wa namna hiyo una gharama kubwa sana kwani unaassume watu hawajui mabaya ya CCM.

Kukijenga Chama
Ninaamini Chadema imepoteza nafasi nyingi sana za kukijenga chama hicho; nafasi ambazo ingekuwa katika nchi nyingine wanasiasa wangekuwa wanazivujia udenda! Baada ya Tunduru, Chadema walifanya nini kuandikisha wanachama wapya Tunduru na kufungua matawi? Baada ya Kiteto walirudi lini na kufungua matawi na kujenga kada ya wanachama? Baada ya Mbeya Vijijini je? Vipi kuhusu Tarime? Na sasa Busanda?

Chadema lazima ijue inataka nini; kushinda uchaguzi au kufanya watu waichukie CCM ili wao washinde uchaguzi? Kushiriki Biharamulo ili kujaribisha ni kupoteza muda, raslimali na nafasi.

Nimejiuliza mara ya mwisho kuona Chadema wakiandikisha wanachama wapya jijini Dar ilikuwa lini? Mara ya mwisho wao kufungua matawi mapya au kuyaimarisha ya zamani ilikuwa lini?

Je ni kwa kiasi gani wanachama wa chini wanajua viongozi wao wamejitoa mhanga kweli katika kukijenga chama? Niwakumbushe vitu viwili ambavyo wengine kwenye historia yetu hawavikumbuki sana, Nyerere alipoamua kujiuzulu Uongozi wa serikali na kurudi kwenye TANU na kuanza ziara za vijijini mnafikiri alikuwa anafanya nini kule vijijini, kuelezea mabaya ya ukoloni?

Na baadaye 1971 alipoanza ziara za vijijini tena na kuzungumza na wananchi moja kwa moja alifanya vile kwa sababu gani?

Viongozi wa Chadema wanahitaji kuachana na siasa za magazeti bali kurudi moja kwa moja kwa wananchi. Ni matumaini yangu kuwa baada ya uchaguzi wao Mkuu wiki chache zijazo, wataaamua kujipanga kwenda vijijini siyo tena kwa Operesheni Sangara bali operesheni ya kujenga chama.

Wasipofanya hivyo, wasubiri kuona jinsi CCM ilivyo na uwezo wa kujijenga tena vijijini, kwani CCM ikitaka inaweza kuconcede majimbo ya miji michache (Moshi, Arusha, Mwanza, Dar, Mbeya na Tanga) na kuchukua majimbo mengine yote na hali haitabadilika isipokuwa nyongeza ya ruzuku kwa wapinzani.

So far CCM haijashindwa kwa hoja, itashindwa kwa mkakati. Subiri "Cheche" ya Ijumaa nitalifunua hili vizuri zaidi.
Heshima yako Mzee Mwanakijiji!
Ni hivi hata yafanywe yote yaliyoelezwa hapa bila ya Katiba mpya,tume huru ya uchaguzi,vyombo vya dola huru na mazingira sawa kwa vyama vyote, kila chaguzi yatajirudia matokeo yale yale kwa majimbo mengi.Hivi kwanini tusifikiri njia mbadala ya kuleta mageuzi mbali na vyama vya siasa?Mageuzi ambayo yatawezesha kufanyika marekebisho ya katiba,kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi,vyombo vya dola huru na uwekaji wa mazingira sawa ktk chaguzi zote kwa washiriki wote.Kwasanduku la kura na mazingira yaliyopo sasa nachelea kusema ni sawa kwa tembo kupita kwenye tundu la sindano.Itatuchukia Karne na karne kama masultani wetu hawatodhoofishana wenyewe ili kuleta mageuzi ya kweli.
 
kwa mtazamo wangu nadhani bado sana kufikia democrasia ya kweli Africa ikiwemo Tanzania! Wanaothani CCm watakubali katiba mpya wasahau kwani ni lini ukasikia samaki akijikaanga mwenyewe! Kumbukeni madaraka matamu africa! Nchi ambazo 80% ya population ni wajinga! 80% masikini ambao ukiwatrigger kidogo tu umewapata. 70% ya viongozi ni miungu mtu! Wanakaa madarakani mpaka wanazeeka! Hivi ni kweli kuwa jimbo la Mtera (kwa mzee tingatinga) tangu nchi inapata uhuru hakuna mtu aliyepatikana kugombea na kufanya hiyo kazi!
Bado safari ni ndefu hasa unapoona hata wasomi wanashabikia CCM. Tatizo kubwa ni kuwa watu hatuna utaifa! Elimu ndo silaha kubwa ya ushindi wa CCM. Hivi kwa mfano mtu wa kijijini mpaka aje ajue kuwa umeme ni muhimu ni lini kama hajawahi uona na akajua matumizi yake. Kwa wale wezangu ambao tulisoma wakati huo kwenye kitabu cha kusadikika! Majibu aliyotoa chiligati kuhusu yaliyokuwa yanafanyika Busanda si ni sawa na majibu aliyojibiwa Karama na Mfalme pale Karama aliposema tunahitaji kujenga barabara. Mfalme akasema hatuhitaji kwani miguu yetu ni futi moja sasa barabara ya nini! Mheshimiwa Chiligati kasema magazeti na na video wanasoma na kuangalia watu wa huko mjini! inamaana Chiligaiti kwa ufahamu bado anazidiwa na Shaabani Robati aliyeishi miaka kama 50 iliyopita na yeye yuko karne nyingine! Ni majibu hayohayo wanayatoa Viongozi wa CCM wakijua hakuna atayehoji kwa sababu atahoji kivipi kitu asichojua!
Tunahitaji mabadiliko hata hapa JF kuna watu bado wanamgando wa mawazo! CHADEMA leteni mabadiliko ya kifikra kwa watu! Toeni hotuba za matumaini na muoneshe kweli kuwa mnaweza! Hivi hamkusikia OBAMA hotuba zake jamani!
 
Hivi kwanini mnafikiri serikali ya CCM iliacha kutilia mkazo Elimu ya Watu Wazima hadi kufikia asilimia 30 ya watu wazima hawajui kusoma na kuandika? Kwa maneno mengine, asilimia 30 ya watu wetu wanategemea kusikia kama njia ya kwanza ya kupata habari na maelezo mbalimbali.

Swali, Je asilimia 30 ya watu wanaweza kuleta tofauti kwenye uchaguzi kama taarifa wanazozipata zinatoka kwenye radio na televisheni tu? Hawawezi kusoma magazeti, vipeperushi, mabango n.k
 
Mkuu mwanakijiji!
Mimi nadhani waliacha makusudi! Who cares! After all ukiwa na wajinga wengi si ndo unaongoza kwa raha! Karaha ya nini kuwa critisized kila wakati! Wasiwasi wangu hii siyo asilimia 30! Is more than that! Halafu hivi elimu wanayopata hawa watu inawapa uwezo wa kuhoji! Au ndo ile ya mwalimu ni biblia!
Swali jingine je hiyo asilimia 30 je wanaredio na TV?
 
- Mkuu wangu unajua kina Nchimbi wapo wanasubiri pembeni kuchukua power, hivi kweli unategemea mabadiliko karibuni? Kuna wengine tumechoshwa na hii political drama ya bongo! Tuna miaka 50 zaidi ya hii drama za kudanganyana tu progress hakuna, pande zote mbili zinatudanganya tu wananchi! wote waende tuanze upya!

Respect.

FMES!

Unachozungumzia kinatoka ndani ya moyo wako kabisa kweli? hivi unataka kuliambia jamvi kwamba Nchimbi akigombea huyu ndugu yangu JM na mwenziwe AKM hawatakwenda kuwadanganya wananchi kuwa watapata maisha bora chini ya Nchimbi? kweli hawatakwenda kumpigia kampeni kama kawaida? hii hapa tunapiga soga tu.
Jamani Chedema shiriki kila uchaguzi kushindwa ni mwanzo wa kushinda. Hakuna kukata tamaa Iko siku tutatoka tu!
Mahakamani no. Mtapigishwa kwata kule mpaka 2011 haina maana. Bado turudi kwa wananchi na wao ndio waamuzi wa kweli. Kama wanaitaji kuendelea kuishi wanavyotaka na si kama wanavyopaswa kuishi, hamna noma. Nyie hubirini kila linalowezekana. Mimi ni mavuno ya Operation Sangara. Ngoja nikawahi kuangalia Man na Baca
 
Unachozungumzia kinatoka ndani ya moyo wako kabisa kweli? hivi unataka kuliambia jamvi kwamba Nchimbi akigombea huyu ndugu yangu JM na mwenziwe AKM hawatakwenda kuwadanganya wananchi kuwa watapata maisha bora chini ya Nchimbi? kweli hawatakwenda kumpigia kampeni kama kawaida? hii hapa tunapiga soga tu.
J

- Hebu rudia tena una maana gani sijakuelewa bado? Kwamba kuna watu watakwenda kumpigia kura Nchimbi, sasa what this has to do na mawazo yangu na mimi FMES?

Respect.

FMEs!
 
Wasipoenda Biharamulo wapinzani wetu (CCM) watasema wameogopa kushindwa na itaonekana hivyo kwa sababu in politics perception is more effective than reality. It will be too damaging politically for CHADEMA not participate in Biharamulo.

Cha kufanya hapa wale wote wenye kiu ya mabadiliko ya kisiasa nchini na wanaoamini kwamba chadema ni agent wa mabadiliko hayo tuwachangie ili tuongezee nguvu za ushindani wao huko Biharamulo. Ningeshauri kwamba mtu mmoja afungue thread ya harambee hapa ili watu waanze kuchanga!

- Mkuu Kitila, with all due respect Chadema fanyeni tathmini makini sana kabla ya kwenda huko Biharamulo, wanaofahamu vizuri sana huko wanasema kwamba upepo kwenu huko sio mzuri sana, sasa basi jaribuni kuonyesha umakini na ukomavu wa kisiasa kuliko watasema au itaonekana, hapana fanyeni the right thing,

- Kama upepo hauko sawa basi saidieni mwenye upepo sawa, otherwise tupo pamoja na kujua nini mipango yenu next! Halafu eti mnahitaji hela za mchango wa nini na huku mnazo za kuchomea helikopta?

Respect.

FMES!
 
Jitihada zote zinaposhindikana lazima tukubali ukweli na kukiri kwamba tumepoteza muda. Kwa mtazamo wangu hakuna chama HATA KIMOJA, chenye uwezo thabiti wa kumkomboa Mtanzania. Nini kifanyike? Tuanze upya. Mwanzo Mpya. Sera Mpya. Nia Mpya. Mawazo Mapya. (CCM msiibe hii kaulimbiu, tumeshaisajili COSOTA!)
 
- Mkuu tupo pamoja sana hapa na ndicho ninachokisema.

Respect.

FMES!
 
Kubadili mkakati wa mahubiri yake, kuhubiri ufisadi hakuleti ushindi bali kuhubiri ujumbe wa matumaini dhidi ya ufisadi kutaleta. Wao watafanya nini. Hapa hawana budi kuradicalize their message. "tutawatafuta wale wote waliohusika na wizi wa fedha umma, tutawawajibisha, na walioficha fedha nje tutahakikisha zinarudishwa ndani ya muda.

Hongereni kwa kuliona hilo; watu wengi walishasema huu mtaji wa ufisadi usha kwisha, wapinzani tuweke mkakati mwengine ili tujiandae kwa uchaguzi mkuu ujao, ikaonekana wanaosema hayo "wana wivu dhidi ya chama chao".

Naungana nawe mdau wa mabadiliko ktk kuwatafuta na kuwaandaa wanachama madhubuti, kwa kuweka mandao mpana zaidi huko vijijini ambako chama tawala kinadai ndio mtaji wake upo huko.

Tutake tusitake; kama vyama vyetu vipo miji mikuu tu hapa nchini, tutaendelea kukokotwa daima milele na tutaendelea kulalamika tunaibiwa hadi kiyama. Mifano ipo mingi tu, tuliona enzi ya NCCR Mageuzi, CUF na sasa Chadema, tena enzi hizo tulipigwa mabo matakatifu huko huko mjini (Ubungo, Temeke, Kigamboni na Kinondoni).

TUJIPANGE UPYA
 
Mzee Mwanakijiji
Ongezea na hizi:
1. Aidha wajifunze ustaarabu, manati hazileti ushnindi
2. Kama mgombea kiti cha urais ni Mh. Mbowe, wasahau kabisa kushika dola. Bisha nikupe sababu.

Kubalini tu mmeshindwa Busanda ndiyo maana hamkutaka kutokea wakati wa kutangaza matokeo kwa kuogopa aibu. Mlikuwa na vijana wengi wa kijiweni tu ambao mliwalipa Shs. 500/- za kazi ya kuzomea lakini mkakosa wapiga kura vijijini. Ama kweli mikakati ya uchaguzi hamna kabisa.
 
hivi mpaka leo vyama vya upinzani vimeshindwa kabisa kuungana na kusimamisha mgombea mmoja kwenye kila jimbo wa chama ambacho kina nguvu zaidi kwenye jimbo hilo na kuweza kufanikiwa kupata viti zaidi bungeni au ndio kila mtu anataka kuwa kiongozi hata kama nafasi ni ndogo? kwa style yao hio hawatafika popote.wale viongozi wao wote wa kubwa wenye nguvu wagombee ubunge na waachane kung'ang'ania kiti cha uraisi na waende kufanya madiriko kwa kutumia nguvu ya bunge.
 
Mimi naamini hakuna sababu ya kuunganisha vyama. Unapofanya hivyo ccm nayo inafanya bidii kujiingiza katika huo ushirikiano ambao baadae hauwi tena ushirika mtakatifu.

Lakini vyama vikijipanga vyenyewe vyema, wananchi watachagua vyama vilivyo bora. Mfano, tizama yaliyofanyika kiteto, busanda, magogoni, tarime n.k Hii inaonyesha chama kikishakuwa na nguvu eneo husika inatosha. Na hii ndio njia pekee kupambanua vyama imara, na vilivyouchwara vitajifia vyenyewe kio cha kawaida.

Suala la msingi ni wewe kuchagua mahali sahihi na usimame na sio kuendelea kusubiri wao tu wafanye.

WAUNGE MKONO, ili mabadiliko yaotkee haraka!

Ni kuulize tu mfano rahisi, unataka CHADEMA au CUF viungane na NRA, NLD, CHAUSA, SAFINA au kitu gani sasa.

Labda ungesema CHADEMA na CUF, lakini pia hawa sidhani kama ngoma itakuwa rahisi kiasi hicho, kwani utamu wa pilau kila mmoja ashushe mkono ndani ya sinia bwana, sasa the later lazima awe Prof au maalimu tu miaka nenda rudi, si yatakuwa yale yale ya bibi aliyeko madarakani (manake keshakaa zaidi ya miaka 45, wakati watawala wa cuf washakaa zaidi ya miaka 15 ambayo ni zaidi ya 1/3 ya ccm). Sasa nadhani watu wanatofautiana katika mambo ya msingi kama haya.
 
Naunga mkono hoja Chadema wajipange upya hakuna sababu ya kwenda biharamulo..hizo fedha wakawasaidie wahanga wa mabomu mbagala
Kwa kuwa ccm wana majimbo mengi, na pia mapato makubwa kuwiko vyama vyote, kwanini usiwashauri wao wakapeleka hizo fedha Mbagala wakaacha vyama vingine viwanie hilo jimbo?, ningekuelewa zaidi kwani from the first place wao ndio waliotakiwa kuwahakikishia usalama Wanambagala na Watanzania kwa ujumla na wala sio vyama vingine visivyokuwa na serikali!
 
Nono,
Mkuu wangu siku zote tunaishi kwa mifano. Unaposema vyama pinzani havina haja ya kuungana nadhani unafikiria tu kutokana na hisia zako bila kuzingatia hali halisi.
Huu mpango wa vyama vingi tumeiga kwa wazungu ama niseme toka Ulaya kwa wale waliotutangulia na huwezi kuona nchi yoyote ktk nchi hizo zikisimamisha vyama karibu 20 katika uchaguzi mmoja tena basi vikiwa na mirengo inayofanana...

Na sababu kubwa ya kutofanya hivyo inatokana na IMANI - ni lazima chama kiundwe kwa tofauti za mrengo na sio mapenzi, makubaliano, au matakwa ya mtu/watu..Clinton sii lazima apendane na Obama wala Demokratic sii wote wanapendana ama kukubaliana kifira ila wote wanasimamia imani moja..Inapofikia swala la imani ni lazima wahusika watu wachague ni upande gani wanasimama na sii kuunda vyama 10 vyenye mrengo mmoja..

Sasa ni aidha tubadilishe kabisa mfumo wa vyama vingi na kuweka tafsiri ya imani hizi za mrengo. wale wote wanakubali upande wa kulia wakae Kulia na wale wanaoamini kushoto wajitenge kutokana na imani hiyo sio kutazama ni upande gani una sura bora zaidi ya nyingine. Ama ni swala la kuungana ili kuondoa mfumo uliopo ambao hautazami mrengo wa chama bali ahadi na sura za wahusika. Mwanasiasa nchi za wenzetu ni yule anayesimamia mrengo fulani, usipokuwa na imani ya mrengo wewe huwezi kuwa mwanasiasa ni sawa mtu asokuwa na dini..

Nimewahi kusema Chadema na CUF inawabidi waondoe tofauti zao hata kama ni vyama viwili vyenye mrengo tofauti kwa sababu hakuna Mtanzania hata mmoja anayetazama mrengo wa chama.. Ukweli ni kwamba hakuna mwananchi anayefahamu Conservative anasimama kulia kwa sababu gani na nini tofauti yake na Progressive au Liberal. Ndio maana ndani ya CCM wapo Conservative na Progressive na wamefanikiwa hadi ktk chgauzi mbali mbali. CCM hadi leo wana sera za mchanganyiko wa Kikommunist, Kijamaa, Kibepari, na hasa ufujaji mkubwa wa pato la Tiafa ktk vitu ambavyo hawizalishi uchumi wa nchi wala kuongeza kazi kwa wananchi na hakuna mtu anayetazama uipande huoi isipokuwa kulaumu mtu mmoja iwe Kikwetye au Mkapa lakini sii chama.

Iweje leo Chadema, CUF, NCCR na TLP wahofie kujiunga kwao kutokana na mrengo wa vyama hivi wakati CCM inashinda chaguzi hizi wakiwa mseto wa kila kitu unachoweza kufikiria..Mkuu wangu CCM ni kama dini, dini moja ya Wakristu au Waislaam wanaokubalika ktk imani na hawajali madhehebu ndani yake maadam wanajulikana ni dini gani..
Vyama vya Upinzani vinajaribu kuunda dini zao kwa imani tofauti tofauti bila kukubali kwamba wao ni Wakristu au Waislaam, hivyo ni shida kubwa kwa Chadema kujitangaza na kukubalika na wengi hata kama wana make sense ktk mengi wanayosimamia.. Ni sawa na Dalai Lama anataka kuwabatiza Watanzania kuwa Monks..
Mkuu Lengo kubwa la CCM kama chama ni - Kushinda chaguzi zote - Na wanashinda na wataendelea kushinda kama vyama vya Upinzani havitaweka kusoma alama za wakati..
Kuogopa Unafiki ktk jamii maskini ni kujiganganya pia, kwani Unafiki ni maisha yetu ya kila siku, usiyaogope! tunazungukana hadi ktk familia zetu, wachawi hawatakwisha kwani ni moja ya desturi zetu hutakiwa kumwogopa mchawi wala kufikiria kuna wachwi, laa sivyo huwezi kuishi Tanzania wala kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom