CHADEMA: Baada ya Biharamulo; Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010

Waende tu wakajaribu bahati yao ... who knows?

1995 - NCCR-Mageuzi
2000 - CUF & TLP
2005 - CUF
2010 - CHADEMA
2015 - n.k.
 
Waende tu wakajaribu bahati yao ... who knows?.

sio bahati peke yake.they must be ambitious TO WIN!
chadema wanaafadhali.kama watafanikiwa kuchukua majimbo mengi,maanake IN A VERY LONG RUN watakuwa na 'power' bungeni.wakijakufikisha over fifty percent,WATAKUWA NA NGUVU YA KUIBADILISHA KATIBA.

again narejea kauli yangu IN A LONG RUN!

kuleta maendeleo=KUIBADILI KATIBA
kubadili katiba=KUISHINDA CCM
kuishinda ccm=kupata ushindi dhidi ya ccm KUANZIA NGAZI YA UBALOZI wa mtaa

KUISHINDA CCM KWENYE LEVEL YA UBUNGE ITAKUWA NGUMU SANA!hata wakiishinda THEY CAN MUNIPULATE VOTES,kwasababu ccm wamekita mizizi kuanzia ngazi za mtaa.WE MUST TAKE THE ROOTS OFF,right at the starting level
 
Kwanza haina sababu ya kufanya hivyo. Pili, inachosha kusikia wimbo wao wa malalamishi kuhusu CCM, dola n.k lakini kubwa ni kupoteza mtaji wao wa kisiasa. Wamuunge mkono mgombea wa chama kingine wao fedha na raslimali ambayo wangeitumia huko kwanza warudi Busanda, Kiteto, Mbeya Vijijini, Tunduru n.k na majimbo mengine kama 70 tu na huko wajijenge kwa ajili ya 2010.

a. Kuandikisha wanachama wapya (kupata kura 22,000 si mchezo kwani kuna wanachama wangapi?)
b. Kufungua matawi mapya
c. Kutengeneza mtandao wa mafunzo kwa makada wake
d. Kutengeneza ajenda za mahali (hili nitalichambua baadaye)
e. Kubadilisha Katiba yake ili kilenge kushinda uchaguzi na kuunda serikali.
f. kulenga majimbo ya mjini ambako imekuwa ikikubalika kwa kufanya hayo ya a, b na c
g. Kubadili mkakati wa mahubiri yake, kuhubiri ufisadi hakuleti ushindi bali kuhubiri ujumbe wa matumaini dhidi ya ufisadi kutaleta. Wao watafanya nini. Hapa hawana budi kuradicalize their message. "tutawatafuta wale wote waliohusika na wizi wa fedha umma, tutawawajibisha, na walioficha fedha nje tutahakikisha zinarudishwa ndani ya muda x).
h. Wahamishe makazi yao toka Dar na kuamia vijijini; Dar iwe pa kuja kuchaji tu.
i. x,y

Mkuu nakubaliana na wewe sana katika hoja zako hapo juu.

Ukweli unabaki kuwa hakuna manufaa yoyote yanayoweza kupatikana kushiriki kutafuta kiti cha ubunge Biharamulo (kiti ambacho hakikuwa kikishikiliwa na CHADEMA awali) kwani ni dhahiri kuwa nguvu kubwa itahitajika kukipata na vilevile kitakuwa chao mpaka uchaguzi ujao mwakani (endapo watafanikiwa kukipata). Manufaa ya kukitafuta kiti hicho kwa sasa yakilinganishwa na hasara ya kukitafuta kiti hicho, inanifanya nione ni bora kutumia muda wa kampeni kujitangaza zaidi kwa ajili ya 2010. Ila hili liko ndani ya maamuzi ya CHADEMA kuona inachokitaka.

Vyama vingi vya siasa hupenda kujitangaza mijini (labda kwa kuwa ofisi zao ziko mijini) kuliko vijijini. Ila kwa mtazamo wangu, endapo vyama vikiweka jitihada zaidi vijijini, na vikakubalika, automatically vitakuwa vimekubalika pia mijini. Hii inatokana na information flow kuwa nzuri sana mijini kuliko vijijini. Lolote litakalofanyika vijijini, litajulikana mijini na kinyume chake ni tofauti. Ningekuwa kiongozi wa chama cha siasa chochote, ningehakikisha nafanya jitihada zote vijijini kwa sababu hizo.

Kuhusiana na sera, nadhani CHADEMA wamefanya kazi nzuri na kubwa sana katika kuonyesha mapungufu ya serikali ya CCM (hususan Ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka). Inabidi sasa waunde team ya specialists ili waweze kuandaa roadmap ya sera zao ambazo wataziuza kwa waTanzania kuanzia sasa (kwa nia ya kupata ridhaa ya waTZ kuwaongoza). Team ya specialists hao inabidi watoke ndani na/au nje ya nchi kwa kuzingatia ujuzi wao katika kuunda sera (baada ya kuelewa mazingira ya nchi).

Sera zijitosheleze. Zihusu uchumi, ulinzi na usalama, afya, elimu, miundombinu, nishati, ushirikiano wa kimataifa, katiba ya nchi, na kadhalika.

Sera ndizo zinazowafanya wananchi kujua ukweli wa nia ya chama kinachowaomba kura. Endapo sera zisipoweza kujibu maswali magumu ya hali ya Taifa hili, wananchi watabaki kuwashabikia wao na baadae kuendelea kuchagua CCM. Hatua ya kwanza ni lazima ichukuliwe mapema kama mafanikio ya kweli yanahitajika.

Vyama vingi vimepata nafasi ya kuwa na umaarufu nchini. Kilianza NCCR-Mageuzi (wakati wa Mrema), kikafuatiwa na CUF na sasa ni CHADEMA. Wananchi huwa hawana subira sana kusubiri chama kikue. Huamishia mapenzi yao kwa chama chochote kinachoonekana kutaka kuanza kujibu maswali ya mahitaji yao. CHADEMA ina nafasi hiyo sasa, isiipoteze. Inaweza kufanikiwa zaidi kama inataka, na kutaka ni lazima kuwe bayana na endelevu.
 
Pamoja na kujimarisha wanatakiwa washiriki Biharamulo kama sehemu ya kujiimarisha zaidi, hasa ukizingatia kuwa jimbo hilo lilikuwa la upinzani, na kuna nafasi ndogo sana ya TLP kuweza kulitetea. Ni sehemu ya kujiimarisha pia ndani ya majimbo yanayolizunguka.
 
- Mkuu wangu unajua kina Nchimbi wapo wanasubiri pembeni kuchukua power, hivi kweli unategemea mabadiliko karibuni? Kuna wengine tumechoshwa na hii political drama ya bongo! Tuna miaka 50 zaidi ya hii drama za kudanganyana tu progress hakuna, pande zote mbili zinatudanganya tu wananchi! wote waende tuanze upya!

Respect.

FMES!

Usife Moyo hata Roma haikujengwa kwa siku moja na pia pamoja na kujengwa haikudumu milele. Waliopo walijijenga kwa muda mrefu na sisi tuna hiyo nafasi it is possible when there is a decision to start and starting is from zero to complete the nine counting numbers. The existing opposition parties provided the zero start and may be they are in 0.1 which is in the high rank in ordinal terms; why then should we go back to 0 which is the lower rank? Kaza buti comander sterlling ha uawi akifa mchezo umekwisha.................
 
Finias Magessa aende mahakamani, Kuna wanasheria wengi wengi tu watajitole kumsimamia pamoja na mzalendo maarufu Tundu Lissu wanaweza wakawaanika CCm na wengi wakafahamu uzandiki wao .CCM wamezidi kugeuza wananchi wote ni wajinga kwanza mahakama inaweza ikatoa hata mwongozo wa kwamba ni vipi mawaziri sita wanaweza wakaweka kambi kwa muda wa mwezi mzima kwenye jimbo la uchaguzi huku nikuchezea pesa za walipa kodi
pamoja na ushindi wa Busanda hawana lakujivunia wamelowa kwa sababu jamii ya kimataifa ilikuwepo na waliona uozo wao na wala hawajatoa tamko lolote manake wanakiri kuwa CCm ni wezi na hawafai kupongezwa
Chadema waende to Biharamulo kama mkakati wa kueneza sera za chama chao na kuwajenga wananci kugombea uchaguzi wa serikali za mtaa mnamo mwezi wa kumi
 
Pamoja na kujimarisha wanatakiwa washiriki Biharamulo kama sehemu ya kujiimarisha zaidi, hasa ukizingatia kuwa jimbo hilo lilikuwa la upinzani, na kuna nafasi ndogo sana ya TLP kuweza kulitetea. Ni sehemu ya kujiimarisha pia ndani ya majimbo yanayolizunguka.

YES!thank you very much
 
Finias Magessa aende mahakamani, Kuna wanasheria wengi wengi tu watajitole kumsimamia pamoja na mzalendo maarufu Tundu Lissu wanaweza wakawaanika CCm na wengi wakafahamu uzandiki wao .CCM wamezidi kugeuza wananchi wote ni wajinga kwanza mahakama inaweza ikatoa hata mwongozo wa kwamba ni vipi mawaziri sita wanaweza wakaweka kambi kwa muda wa mwezi mzima kwenye jimbo la uchaguzi huku nikuchezea pesa za walipa kodi
pamoja na ushindi wa Busanda hawana lakujivunia wamelowa kwa sababu jamii ya kimataifa ilikuwepo na waliona uozo wao na wala hawajatoa tamko lolote manake wanakiri kuwa CCm ni wezi na hawafai kupongezwa
Chadema waende to Biharamulo kama mkakati wa kueneza sera za chama chao na kuwajenga wananci kugombea uchaguzi wa serikali za mtaa mnamo mwezi wa kumi

Nikupoteza muda na resources twende biharamlo kupeleka kesi nyingine kwenye mahakama ya raia ili hakimu aamue tena. Mahakama ya raia inatosha na haki wamesha itoa Busanda kama imekuwa presented na karani kama mahakimu walivyoitoa karani hana nguvu zaidi ya hakimu so to me karani atafanya analysis mwenyewe kama hakimu ataendelea kumwamini au ndo siku moja ataamua kumfukuza kazi na kumnyima mafao yake yote. Mchezo wa ukuti ukuti ni wa watoto, wakubwa mambo yao ni kwa busara.
 
nakubaliana na hoja hii kuhusu Chadema kujipanga upya, lakini sishauri wasishiriki biharamulo...ninachoshauri ni kwamba yale ayaliyotokea Busanda yasiachwe tuu...ukweli uwekwe wazi for the records..2010 is very near, na Chadema wafanye utafiti wao na wajifanyie assessment ya kweli kuhusu muelekeo wao...suala la wao kujistrategize halikwepeki...ushindani waliouleta kwa CCM katika hizi chaguzi zote ni sehemu moja ya kujitangaza na mwanzo wa kampeni za 2010...waweke mikakati sasa ya jinsi ya kupambana na unyang'au na uporaji wa CCM katika chaguzi hizi.
huu ni wakati muafaka wao kuendelea na mapambano kwa nia ya kufanya maandalizi ya 2010,wanaposhindwa wasikate tamaa maana kwenda 50-50 na CCM ni mafanikio makubwa kwao katika jimbo ambalo lilikuwa mikononi mwa CCM.

lingine kubwa nazani ifike hatua sasa vyama vya upinzani vianze kufikiria suala la ushirikiano...kama wote nia ni moja kuikomboa nchi mikononi mwa CCM basi ifike hatua wakubaliane pale ambapo mmoja ana nguvu zaidi aachiwe na washirikiane...uchanguzi wa busanda CUF ilikuwa ikitumiwa na CCM na walikuwa wanataka ionekane CUF ndio mpinzani mkubwa jimboni...
juzi kwenye TBC1 Mrema alisema neno moja kwamba ni wakati sasa vyama vya upinzani vi-'RETREAT' na vijipange upya maana especially kwenye suala la ushirikiano..nakubaliana nae kwa hili.....waache ubinafsi amabao matokeo yake hukusa wote...
 
[

lingine kubwa nazani ifike hatua sasa vyama vya upinzani vianze kufikiria suala la ushirikiano...kama wote nia ni moja kuikomboa nchi mikononi mwa CCM basi ifike hatua wakubaliane pale ambapo mmoja ana nguvu zaidi aachiwe na washirikiane...uchanguzi wa busanda CUF ilikuwa ikitumiwa na CCM na walikuwa wanataka ionekane CUF ndio mpinzani mkubwa jimboni...
juzi kwenye TBC1 Mrema alisema neno moja kwamba ni wakati sasa vyama vya upinzani vi-'RETREAT' na vijipange upya maana especially kwenye suala la ushirikiano..nakubaliana nae kwa hili.....waache ubinafsi amabao matokeo yake hukusa wote...[/QUOTE]

Mimi nadhani hakuna sababu ya wao kushirikiana wanatupiana lawama sana na kuchelewesha mapinduzi ya kweli washirikiana kwa sauti kama kattika maswala ya uporaji wa rasilimali na ubovu wa katiba mambo mengine iwe kwa kila chama kujijenga kwa nguvu zake ili kuwe na chama chenye nguvu pinzani
 
Suala la muungano wa vyama natilia shaka sana. Nia ya kuungana ni nini hasa? au kumtoa sisiemu madarakani kisha wao waanze kugombea fito??
Hapa ni sera sahihi na elimu kwa umma baasi.
Labda ninakosea naomba kukosolewa
 
Kwanza haina sababu ya kufanya hivyo. Pili, inachosha kusikia wimbo wao wa malalamishi kuhusu CCM, dola n.k lakini kubwa ni kupoteza mtaji wao wa kisiasa. Wamuunge mkono mgombea wa chama kingine wao fedha na raslimali ambayo wangeitumia huko kwanza warudi Busanda, Kiteto, Mbeya Vijijini, Tunduru n.k na majimbo mengine kama 70 tu na huko wajijenge kwa ajili ya 2010.

a. Kuandikisha wanachama wapya (kupata kura 22,000 si mchezo kwani kuna wanachama wangapi?)
b. Kufungua matawi mapya
c. Kutengeneza mtandao wa mafunzo kwa makada wake
d. Kutengeneza ajenda za mahali (hili nitalichambua baadaye)
e. Kubadilisha Katiba yake ili kilenge kushinda uchaguzi na kuunda serikali.
f. kulenga majimbo ya mjini ambako imekuwa ikikubalika kwa kufanya hayo ya a, b na c
g. Kubadili mkakati wa mahubiri yake, kuhubiri ufisadi hakuleti ushindi bali kuhubiri ujumbe wa matumaini dhidi ya ufisadi kutaleta. Wao watafanya nini. Hapa hawana budi kuradicalize their message. "tutawatafuta wale wote waliohusika na wizi wa fedha umma, tutawawajibisha, na walioficha fedha nje tutahakikisha zinarudishwa ndani ya muda x).
h. Wahamishe makazi yao toka Dar na kuamia vijijini; Dar iwe pa kuja kuchaji tu.
i. x,y

Mwanakijiji si CHADEMA tu, inabidi wapinzani wote wasusie ili CCM ibaki pekee ambapo itakuwa NDIYO=HAPANA kama zamani.
 
Mojawapo ya udhaifu mkubwa wa CHADEMA ni tabia waliyojijengea ya kupenda mipasho zaidi ya mikakati.
Ingekuwa hii thread inahusu kumjadili kiongozi fulani anayehusishwa na skendo, ungeona viongozi wa CHADEMA kibao wanakuja kutoa ''umbea'' walio nao.
Ikianzishwa thread ya kujadili mikakati huwaoni viongozi wa CHADEMA humo.Hawako interested na mijadala ya aina hii! Wanavutiwa zaidi na kujadili nani hajafanya kitu sahihi kuliko kujadili wao CHADEMA watafanya vipi kitu sahihi.
Hii ni kuthibitisha kuwa aidha hawawezi au hawana nia ya kufanya kilicho sahihi.
 
Hii imekaa vizuri pengine ni wakati mzuri viongozi na wapenzi wa CHADEMA mkautazama upya mkakati wa kukinusuru chama hasa kujikita zaidi katika mikakati ya muda mrefu.

Nakubaliana pia na hoja nzito za Mzee Mwanakijiji ni jambo jema kama CHADEMA itayatafakari na ikiwezekana kuyatekeleza.
 
Suala la muungano wa vyama natilia shaka sana. Nia ya kuungana ni nini hasa? au kumtoa sisiemu madarakani kisha wao waanze kugombea fito??
Hapa ni sera sahihi na elimu kwa umma baasi.
Labda ninakosea naomba kukosolewa

Mkuu Msanii sidhani kama umekosea. Uko sahihi kabisa. Kwa kuongezea tu niseme;

Kuunganisha vyama inaweza ikawa na faida na hasara pia. Kuunganisha vyama kwa makubaliano ya ku-compromise principles za chama kimoja ili kuweza kutoa nafasi kwa chama kingine inaweza ikapunguza kasi ya maendeleo ya chama chenye nguvu zaidi ya kingine (kwa maana sote tunajua vyama vina nguvu tofauti). Kinachotakiwa ni

1. busara ya vyama ambavyo dhahiri haviwezi kukua tena kuungana na vyama vyenye nguvu bila masharti yoyote. Kwa maana nyingine, vyama hafifu vijiue na wananchama wake waingie kwenye vyama vyenye nguvu ili kuendeleza ushindani kwa chama tawala.

2. Kuunganisha nguvu kwenye chaguzi ambapo chama kimoja cha upinzani kinaonyesha dhahiri kuwa kimejiandaa vyema na kina uwezo zaidi wa kushinda.

3. Kuacha kulumbana baina ya chama kimoja cha upinzani na kingine.
Nadhani wakati umefika kwa vyama vinavyoonekana kukua kuacha kujibizana na vyama vilivyochoka. Hii itavisaidia kuonekana pia kuwa vinafanya shughuli zao kwa busara na viongozi wake ni makini. Malumbano huchelewesha jitihada za kukuza vyama, na anaefaidika na malumbano ya vyama hivi ni mmoja tu.

4. Vyama vizingatie kurekebisha Katiba zao ili ziweze kuvutia wananchi wengi kujiunga navyo. Ukweli na uhakika ni kuwa, wananchi wakiona kuwa chama kinauwiano mzuri wa kiutawala, kina utawala shirikishi, kinazingatia utawala wa sheria, kinaweka kipaumbele fursa za kila mwanachama kukua katika chama, kinazingatia ustawi wa jamii nzima ya Tanzania na kwa ujumla kinajali haki za binadamu, watajiunga nacho bila kufikiria mara mbili. Kitakachowavutia zaidi ni uzingatiaji/ufuataji wa Katiba ya chama hicho kwa kila kiongozi. Ni katika maandishi ya kimkataba kama haya ndipo wananchi wataona umakini na nia njema za chama cha siasa cha upinzani.
 
Kwa sababu tu Joto linazidi duniani, watu mnapendekeza tuisimamishe dunia kujizungusha kwenye Muhili wake na kulizunguka jua ili tuanze moja???
Madhara yake ni makubwa na yenye ukaburi kuliko kuendelea kukarabati huku dunia ikiendelea kujizungusha.
Hakuna kurudi nyuma plasta ndani ya vyama iendelee kupigwa huku mwendo ukiwa ni wa kasi.
 
Kwanza haina sababu ya kufanya hivyo. Pili, inachosha kusikia wimbo wao wa malalamishi kuhusu CCM, dola n.k lakini kubwa ni kupoteza mtaji wao wa kisiasa. Wamuunge mkono mgombea wa chama kingine wao fedha na raslimali ambayo wangeitumia huko kwanza warudi Busanda, Kiteto, Mbeya Vijijini, Tunduru n.k na majimbo mengine kama 70 tu na huko wajijenge kwa ajili ya 2010.

a. Kuandikisha wanachama wapya (kupata kura 22,000 si mchezo kwani kuna wanachama wangapi?)
b. Kufungua matawi mapya
c. Kutengeneza mtandao wa mafunzo kwa makada wake
d. Kutengeneza ajenda za mahali (hili nitalichambua baadaye)
e. Kubadilisha Katiba yake ili kilenge kushinda uchaguzi na kuunda serikali.
f. kulenga majimbo ya mjini ambako imekuwa ikikubalika kwa kufanya hayo ya a, b na c
g. Kubadili mkakati wa mahubiri yake, kuhubiri ufisadi hakuleti ushindi bali kuhubiri ujumbe wa matumaini dhidi ya ufisadi kutaleta. Wao watafanya nini. Hapa hawana budi kuradicalize their message. "tutawatafuta wale wote waliohusika na wizi wa fedha umma, tutawawajibisha, na walioficha fedha nje tutahakikisha zinarudishwa ndani ya muda x).
h. Wahamishe makazi yao toka Dar na kuamia vijijini; Dar iwe pa kuja kuchaji tu. i. x,y

Mkuu nakubaliana na hoja zote ila hapo ebu fafanua watakujua Dar kuchaji nini? Huko vijijini hakuna betri ama sijaelewa bandugu
 
Kwanza haina sababu ya kufanya hivyo. Pili, inachosha kusikia wimbo wao wa malalamishi kuhusu CCM, dola n.k lakini kubwa ni kupoteza mtaji wao wa kisiasa. Wamuunge mkono mgombea wa chama kingine wao fedha na raslimali ambayo wangeitumia huko kwanza warudi Busanda, Kiteto, Mbeya Vijijini, Tunduru n.k na majimbo mengine kama 70 tu na huko wajijenge kwa ajili ya 2010.

a. Kuandikisha wanachama wapya (kupata kura 22,000 si mchezo kwani kuna wanachama wangapi?)
b. Kufungua matawi mapya
c. Kutengeneza mtandao wa mafunzo kwa makada wake
d. Kutengeneza ajenda za mahali (hili nitalichambua baadaye)
e. Kubadilisha Katiba yake ili kilenge kushinda uchaguzi na kuunda serikali.
f. kulenga majimbo ya mjini ambako imekuwa ikikubalika kwa kufanya hayo ya a, b na c
g. Kubadili mkakati wa mahubiri yake, kuhubiri ufisadi hakuleti ushindi bali kuhubiri ujumbe wa matumaini dhidi ya ufisadi kutaleta. Wao watafanya nini. Hapa hawana budi kuradicalize their message. "tutawatafuta wale wote waliohusika na wizi wa fedha umma, tutawawajibisha, na walioficha fedha nje tutahakikisha zinarudishwa ndani ya muda x).
h. Wahamishe makazi yao toka Dar na kuamia vijijini; Dar iwe pa kuja kuchaji tu.
i. x,y

Ndugu Mwanakijiji:

Sijishughulishi sana na mijadala ya vyama vya kisiasa na maendeleo yake nchini Tanzania. Lakini kwa kuangalia kutoka pembe nyingine naona project ya kuwa na multi-party system, ilitegemewa na wengi wenye kuelimika kuleta vyama viwili vikubwa vya siasa kama ilivyo Marekani au UK.

Project hii kwa Tanzania ni failure tupu. Zanzibar imewezekana kwa sababu za kihistoria tu. Na tusitegemea kuwa katika miaka ya hivi karibuni, CHADEMA inaweza kujijenga na kuwa chama mbadala kwa kutumia resources zake bila kuwepo na historical events.

Kitu kimoja ambacho kinaweza kuwa catalyst ya historical events ambazo zingeleta mabadiliko ya kisiasa ni katiba. Mpaka sasa CCM inachotakiwa kufanya ni kulinda mabadiliko ya kikatiba hili kuendelea kuwepo madarakani kama ilivyo sasa.

Katiba ikibadilika na kuruhusu wagombea huru, mabadiliko mengi ya kihistoria yatatokea. Watu wa chama kimoja au tofauti, au huru wanaweza kugombea nafasi moja ya uongozi. Project ya mabadiliko ya katiba ingekuwa na manufaa zaidi kwa taifa kuliko project ya sasa inayotaka katika kila mfuasi wa CCM basi awepo mmoja wa CHADEMA au CUF.

Matawi na viongozi wa CCM waliopo vijijini hawapo kule kwa mapenzi ya chama. Na CHADEMA isitumie resources zake kwa matumaini siku moja na wao watakuwa na matawi au wanachama wenye idadi ya ku-match ile ya CCM.

CCM ina Matawi mpaka vijijini kwa sababu watu wanapenda ulaji na watu wanapenda washindi. Na kama matawi na wanachama hao wangependa siasa, CCM isingekuwa na sababu ya kutoa pilau, khanga au T-shirt.
 
Mimi huwa najiuliza wakati mwingine, kama je ni kweli viongozi wa vyama vya siasa hasa vinavojinadi kuwa vya upinzani wapo pale kweli kwa maslahi ya nchi hii?

Wote tuna objective moja? kama ni hivyo kwa nini wanakuwa wanalumbana tena...........

Mimi nina wasi wasi na nia yao..ifike mahali hivi vyama visafishwe..viongozi waliopo ni wale wale tangu miaka hiyo....tofautiu na CCM ni nini?

ndo maana wananchi wanaona zimwi likujualo ..halikuli likakwisha...bado upinzani haujawashawishi wananchi kwa nini uwaamini na kuwapa nchi

Naunga mkono hoja Chadema wajipange upya hakuna sababu ya kwenda biharamulo..hizo fedha wakawasaidie wahanga wa mabomu mbagala
 
Back
Top Bottom