Uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu: Je vyama vya siasa vimechakata taarifa ya sensa ya watu na makazi ili kufanya siasa kisayansi?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,002
20,662
Taarifa ya sensa ya watu na makazi, kwa kiasi kikubwa, inatoa taarifa za "saiti" kukoje. Kaya, mtaa, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa. Mwanasiasa akifanikiwa kuzichimba na kuzishika takwimu za sensa, akienda mahali akapiga siasa. Anakuwa na uelewa wa eneo husika kiuchumi, kijamii na hata kisiasa.

Atajua huduma za maji, umeme, afya, barabara, elimu, na kadhalika. Mi kwa kiasi gani vyama vinajiandaa kwa uchaguzi kwa kuzingatia taarifa mbalimbali za kiutafiti?

Hii itasaidia kuondoa wanasiasa wanaodhani siasa ni kazi ya kupiga mudomo ti na maneno mengi. Wanasiasa wangapi wanafuatilia tafiti za kisomi zilizofanywa kuhusu majimbo wanayowania?.

Kwa upande wa CDM, mwanasiasa anayetumia takwimu na tafiti ni Lissu, kea upande wa CCM ni viongozi wote wa kitaifa.

Anayetaka uenyekiti wa kijiji/mtaa amepitia taarifa ya sensa kujua ajenge hoja katika engo ipi ambayo taarifa ya sensa imeonyesha mapungufu au mafanikio. Katika ngazi ya Kata, wanaoutaka udiwani pia wamepitia taarifa ya sensa ya eneo lake na kuipa tafsiri ya kisiasa?

Viongozi wa vyama kitaifa na mawilayami, wana uwezo wa kuchakata data hizo ili kuwajenga wagombea wao kupambana jukwaani ?

Vyama vina idara za tafiti au vina fedha ya kuitisha washauri (consultants) ambao watafanya uchambuzi wa tafiti na taarifa mbalimbali na kuzipa engo ya kisiasa, na kisha kuzivunja vunja ngazi ya mkoa na wilaya/jimbo zikatumiwe na wagombea kujenga hoja.

Je vyama vinafanya tafiti ya ya ya tabia za watanzania kimaeneo na jinsi ya kuwa-approach kisiasa? Hotuba ya Tarime na Rufiji haziwezi kufanana.

Vyama vinafanya tafiti za kisomi(acha vitaarifa vya makada) kuhusu nguvu yao katila matawi/misingi na nini kinawaathiri?

Wangapi wanaisoma dira ya maendeleo ya taifa na kuipa tafsiri kisiasa kwa eneo husika la uchaguzi?

Wangapi wanahudhuria makongamano, mijadala ya kisomi ili kujijengea uelewa wa mambo mbalimbali ya kijamii? Mnyika alikuwa mzuri sana katika kuhudhuria na ilimjenga sana kisiasa na kujiamini.

Tukifikia hatua hiyo, tutaondoa wanasiasa njaa, wanaodhani siasa ni kuropoka tu kama Mdude Nyagali.

N.B: Najua mkuu wa idara ya utafiti CCM ni Paul Makonda
 
Unapata wapi taarifa za kina za sensa kwa eneo lako? Labda mtaa au kata ili uzipitie, sio tu kwa lengo la kugombea uongozi wa kisiasa, bali hata kwa uelewa tu kama mkazi. Mfano taarifa za kata ya Mbezi, zinapatikana wapi?
 
Mamlaka inayohusika na sensa na takwimu (NBS)
 
Back
Top Bottom