CHADEMA: Baada ya Biharamulo; Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010

walichofanya chadema ni sahihi ni bora kujifunza kutokana na makosa na inavyoelekea wanajifunza ndio maana kila uchaguzi angalau wanakaribia ushindi hasa hii wa biharamlo
 
Kwanza haina sababu ya kufanya hivyo. Pili, inachosha kusikia wimbo wao wa malalamishi kuhusu CCM, dola n.k lakini kubwa ni kupoteza mtaji wao wa kisiasa. Wamuunge mkono mgombea wa chama kingine wao fedha na raslimali ambayo wangeitumia huko kwanza warudi Busanda, Kiteto, Mbeya Vijijini, Tunduru n.k na majimbo mengine kama 70 tu na huko wajijenge kwa ajili ya 2010.
i. x,y

ukitazama vizuri CCM inatakiwa kujipanga vizuri kuikabili CHADEMA 2010 hususani kwenye haya majimbo yaliyofanya chaguzi ndogo. sehemu zote CCM imecheza rafu kuupata ushindi na 2010 wacheza rafu watakuwa wanapambana kwenye majimbo yao with exception ya Makamba. Vile vile Chadema ni muhimu kuweka msisitizo sehemu watakazo shinda hususan huku walipopata uuungwaji mkono kwa muda mfupi walau waibuke na majimbo yakutosha kuithibiti 1/3 ya bunge

aluta continua
 
Mkuu ni kweli mtupu unayoongea, inatakiwa watuonyeshe mbinu mbadala za uhakika na zenye tija mambo ya kusema eti nitakusanya kodi hivi na vile hilo hata mtoto wa shule ya msingi ana uwezo nalo kulisema.

Ndiyo mimi nikasema jogoo ni yule yule kapwaka rangi tofauti ,mbinu za CHADEMA ukiziangalia hazina tofauti na za ccm ,ila zimepakwa rangi tuu.
Mkuu heri hizi zimepakwa rangi je; tuendelee na zile ambazo hata rangu hazina??????
 
Najua hata mwizi roho humuuma akitulia; hata akiwa selo huumia kwa vitendo vyake; vile vile hata mashabiki wale wanazi (ofcourse wengine ndio mnalipwa namna hii) roho zinawauma maana wanafanya vitendo ambavyo wakifanyiwa wao waisingependa wafanyiwe vile; ila wako juu sasa wanashindwa kushuka; ila kwa uwezo wake muumba atawashusha na kuwaumbua mbele ya haki maana anaangalia waja wake wakiteketea kwa magonjwa ( afya shida); maisha magumu;na mizongo ya kila siku; nachelea kuona na wewe ukiwa ktk kundi la waumbuliwa mbele ya haki; utajiri mtamu ila; ila mtamu zaidi kama unatoka kwa haki; Kama wafanya ushabiki na spining kwa manufaa ya dhati kujenga nchi yako-Ubarikiwe; lakini kama mtu yeyote afanya kwa manufaa ya matumbo na araruwe
 
Last edited:
Wakuu wote JF, heshima mbele sana bado tuko likizo isipokuwa kidogo tu:-

1. Tunawapa CCM hongera kwa ushindi wa Biharamulo, demokrasia sio kushinda kwa Chadema tu, tulisema toka mwanzo ile strategy ya uraia wa Oscar iloikuwa wrong number na ndiyo iliyopunguza hewa ya imani kwa upinzani huko jimboni.

2. Chadema na Upinzani wajipange upya, siku zote kuna kesho, waje hapa wakubali ku8beba responsibility ya kushindwa badala ya kulia lia kila siku, ninasema hivi it is about time sasa viongozi wote wa juu wa Upinzani wakajiondoa na kuwapa nafasi vijana wapya, CCM tunaijua na mauza uza yake, lakini Upinzani hatuyajui isipokuwa ni haya matokeo ya uchaguzi ndiyo yanajisema yenyewe kwamba viongozi huko hawana jipya zaidi ya CCM.

3. The good news ni kwamba tuna wana-JF watatu tayari ambao wameji-commit kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge mwakani katika majimbo matatu ya uchaguzi hizi ni habari njema sana, na we are working arround the clock behind the scene kuwasaidia kwa hali na mali, pia tuna wabunge wetu watano mashujaa kutoka bunge linaloisha ambao ni lazima tuwarudishe kwa anymeans necessary kwa hiyo wakuu JF sasa tunaanza pole pole kuingia kwenye action, badala ya maneno matupu,

- The bad news ni kwamba bado JF hatujawafikia wananchi wengi wanao-matter na uchaguzi, yaani wapiga kura kwa hiyo wakuu tuzidishe juhudi kufikia wananchi wapiga kura, otherwise tuko pamoja sana huku pembeni.

Respect and out!

Kamanda FMES!
 
Adui wa CCM ni CUF hili halina mpinzani wala mbadala ,na wenyewe CCM wanapokutana mazungumzo yao ni vipi wataikabili CUF 2010 maana kuzuilika bila ya kuibia haiizuiliki, vyama vingine kwa CCM ni laini na nyororo hivyo havihitaji kazi kubwa ni rahisi kuvipiga buti na vikasarenda. Au uongo ?
 
CCM wataendelea kushinda sehemu zote ambazo wananchi wamegawanyika. I mean wakati margin ya ushindi inapokuwa ndogo always itawafavour CCM kwa sababu ya wizi na utapeli kwenye kura na kuhesabu.

Kwa hiyo strategy ya CHADEMA 2010 iwe ni kutafuta majimbo 100 ambayo wanaweza kuksimamisha wagombea wenye nguvu hasa na wenye uwezo wa kupata 75%. Basi! Wasijihusihe na kingine chochote. Target iwe kupata angalau 50 ya hayo. Huo utakuwa ushindi mkubwa. CCM will be done. Kilichobaki CCM watafanya wenyewe. Urais unawezekana kwa CHADEMA 2015.
 
Unaposikia upinzani wameshinda kwa asilimia 51, ujue in real terms walishinda kwa asilimia 80. Wakipata asilimia 60, CCM wanashinda kwa asilimia 51. That's a fact!!
 
Bado ukweli utabakia kwamba Chadema pekee bila nguvu ya pamoja na vyama vingine haiwezi kumshinda CCM.
Kulingana na maneno ya Mrema, Biharamulo ilikuwa jimbo la TLP, hivyo ushindi wa wananchi wa Biharamuro ni kumwondoa TLP sii kushinda kwa Chadema wala CCM..kilichotokea huko Biharamuro ni wananchi kukiacha chama hicho na kujiunga na vyama vingine ikiwa na maana CCM wameongeza umaarufu wao baada ya kushindwa uchaguzi uliopita, na Chadema wameongeza umaarufu wao kwa kiwango kikubwa zaidi ya CCM kwa sababu hawakuwa nafasi walioshika leo.

Hivyo pamoja na kuibiwa kura ni muhimu tukubali kwamba hadi sasa hivi CCM aidha imesimama palepale pa mwaka jana kabla ya kuiba kura au imeongeza umaarufu wake kwa kuchukua asilimia ndogo ya wafuasi wa TLP.
Binafsi nitaendelea kuamini kwamba ipo haja kubwa sana ya Muafaka baina ya wapinzani hasa chama Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi..ambao kwa muda wamekuwa na matatizo baina yao.
Ni muhimu sana chama CUF na NCCR-Mageuzi wakubali dira ya Chadema ambayo inaonekana kuwavutia wananchi zaidi ya kushindana ktk uongozi..Kisha chama TLP wakubali kwamba wanapoteza umaarufu na p[engine ni wakati muafaka kwao kufanya mageuzi ya haraka iwekenavyo..
Nje ya hapo, tutakuwa tunajidanganya kufikiria kwamba Chadema imeweza kusimama na CCM wakati ushindi haukuwa wetu mahala ambapo CCM ilishindwa uchaguzi uliopita. Leo hii tukiweza kumwondoa CCM ni furaha yetu sote kuondoka kwa CCM ndiko kunatangulia zaidi ya amechukua nani kwani macho yetu wote ni kuona CCM imeanguka!
Yawezekana kabisa ndicho walichoomba wana Biharamulo - kuanguka kwa TLP.
 
Haya maneno wengine hawataki kuyasikia ,utapoteza hadhi yako hapaa ohoooooo.
wapaswa kusema CCM kwisha waiba kura kwa ma bavu na CUF kwishaaaaaaaaaa ,na chama mbadala ni chadema .kituo kikubwa.
 
Bado ukweli utabakia kwamba Chadema pekee bila nguvu ya pamoja na vyama vingine haiwezi kumshinda CCM.
Kulingana na maneno ya Mrema, Biharamulo ilikuwa jimbo la TLP, hivyo ushindi wa wananchi wa Biharamuro ni kumwondoa TLP sii kushinda kwa Chadema wala CCM..kilichotokea huko Biharamuro ni wananchi kukiacha chama hicho na kujiunga na vyama vingine ikiwa na maana CCM wameongeza umaarufu wao baada ya kushindwa uchaguzi uliopita, na Chadema wameongeza umaarufu wao kwa kiwango kikubwa zaidi ya CCM kwa sababu hawakuwa nafasi walioshika leo.

Hivyo pamoja na kuibiwa kura ni muhimu tukubali kwamba hadi sasa hivi CCM aidha imesimama palepale pa mwaka jana kabla ya kuiba kura au imeongeza umaarufu wake kwa kuchukua asilimia ndogo ya wafuasi wa TLP.
Binafsi nitaendelea kuamini kwamba ipo haja kubwa sana ya Muafaka baina ya wapinzani hasa chama Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi..ambao kwa muda wamekuwa na matatizo baina yao.
Ni muhimu sana chama CUF na NCCR-Mageuzi wakubali dira ya Chadema ambayo inaonekana kuwavutia wananchi zaidi ya kushindana ktk uongozi..Kisha chama TLP wakubali kwamba wanapoteza umaarufu na p[engine ni wakati muafaka kwao kufanya mageuzi ya haraka iwekenavyo..
Nje ya hapo, tutakuwa tunajidanganya kufikiria kwamba Chadema imeweza kusimama na CCM wakati ushindi haukuwa wetu mahala ambapo CCM ilishindwa uchaguzi uliopita. Leo hii tukiweza kumwondoa CCM ni furaha yetu sote kuondoka kwa CCM ndiko kunatangulia zaidi ya amechukua nani kwani macho yetu wote ni kuona CCM imeanguka!
Yawezekana kabisa ndicho walichoomba wana Biharamulo - kuanguka kwa TLP.

Mkandara,

Waungane vyama vipi na vipi? yaani chadema na TLP? njoo rikizo nyumbani baba ujionee huko unapata nusunusu
 
Walichofanya Chadema mpaka sasa ni sahihi, na mafanikio yameonekana. Kuongeza idadi ya wapiga kura wanaokiunga mkono sio jambo dogo.

Naelewa humu kuna wapotoshaji waliosomea, na pengine wanalipwa kwa kazi hiyo, ili ionekane Chadema imekosea njia. Mimi naamini kabisa mafanikio wanayoyapata (ukiachilia mbali kuukosa ubunge) ni makubwa na ya kujivunia.

Mkumbuke jambo moja: Upinzani Tanzania umejengwa zaidi kwa influence ya mtu mmoja mmoja, kama Seif Shariff kule Zanzibar, na Mrema huku Bara. Kudorora kwa hawa ndio imekuwa kudorora kwa vyama. Lakini kwa Chadema hali ni tofauti. Hiki ni chama-taasisi, na sio chama-mtu.
Kwa hilo tu, big up Chadema! Wasomi wengi na walalahoi watawafuateni.
 
Kwanza haina sababu ya kufanya hivyo. Pili, inachosha kusikia wimbo wao wa malalamishi kuhusu CCM, dola n.k lakini kubwa ni kupoteza mtaji wao wa kisiasa. Wamuunge mkono mgombea wa chama kingine wao fedha na raslimali ambayo wangeitumia huko kwanza warudi Busanda, Kiteto, Mbeya Vijijini, Tunduru n.k na majimbo mengine kama 70 tu na huko wajijenge kwa ajili ya 2010.

a. Kuandikisha wanachama wapya (kupata kura 22,000 si mchezo kwani kuna wanachama wangapi?)
b. Kufungua matawi mapya
c. Kutengeneza mtandao wa mafunzo kwa makada wake
d. Kutengeneza ajenda za mahali (hili nitalichambua baadaye)
e. Kubadilisha Katiba yake ili kilenge kushinda uchaguzi na kuunda serikali.
f. kulenga majimbo ya mjini ambako imekuwa ikikubalika kwa kufanya hayo ya a, b na c
g. Kubadili mkakati wa mahubiri yake, kuhubiri ufisadi hakuleti ushindi bali kuhubiri ujumbe wa matumaini dhidi ya ufisadi kutaleta. Wao watafanya nini. Hapa hawana budi kuradicalize their message. "tutawatafuta wale wote waliohusika na wizi wa fedha umma, tutawawajibisha, na walioficha fedha nje tutahakikisha zinarudishwa ndani ya muda x).
h. Wahamishe makazi yao toka Dar na kuamia vijijini; Dar iwe pa kuja kuchaji tu.
i. x,y
Sina cha kuongeza hapa mzee wangu Mwanakijiji
 
Bado ukweli utabakia kwamba Chadema pekee bila nguvu ya pamoja na vyama vingine haiwezi kumshinda CCM.
Kulingana na maneno ya Mrema, Biharamulo ilikuwa jimbo la TLP, hivyo ushindi wa wananchi wa Biharamuro ni kumwondoa TLP sii kushinda kwa Chadema wala CCM..kilichotokea huko Biharamuro ni wananchi kukiacha chama hicho na kujiunga na vyama vingine ikiwa na maana CCM wameongeza umaarufu wao baada ya kushindwa uchaguzi uliopita, na Chadema wameongeza umaarufu wao kwa kiwango kikubwa zaidi ya CCM kwa sababu hawakuwa nafasi walioshika leo.

Hivyo pamoja na kuibiwa kura ni muhimu tukubali kwamba hadi sasa hivi CCM aidha imesimama palepale pa mwaka jana kabla ya kuiba kura au imeongeza umaarufu wake kwa kuchukua asilimia ndogo ya wafuasi wa TLP.
Binafsi nitaendelea kuamini kwamba ipo haja kubwa sana ya Muafaka baina ya wapinzani hasa chama Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi..ambao kwa muda wamekuwa na matatizo baina yao.
Ni muhimu sana chama CUF na NCCR-Mageuzi wakubali dira ya Chadema ambayo inaonekana kuwavutia wananchi zaidi ya kushindana ktk uongozi..Kisha chama TLP wakubali kwamba wanapoteza umaarufu na p[engine ni wakati muafaka kwao kufanya mageuzi ya haraka iwekenavyo..
Nje ya hapo, tutakuwa tunajidanganya kufikiria kwamba Chadema imeweza kusimama na CCM wakati ushindi haukuwa wetu mahala ambapo CCM ilishindwa uchaguzi uliopita. Leo hii tukiweza kumwondoa CCM ni furaha yetu sote kuondoka kwa CCM ndiko kunatangulia zaidi ya amechukua nani kwani macho yetu wote ni kuona CCM imeanguka!
Yawezekana kabisa ndicho walichoomba wana Biharamulo - kuanguka kwa TLP.
Asante kwa mchango wako Kaka yangu, Sina cha kuongeza kwa i was thought kama wewe na michango hiyo pia
 
Walichofanya Chadema mpaka sasa ni sahihi, na mafanikio yameonekana. Kuongeza idadi ya wapiga kura wanaokiunga mkono sio jambo dogo.

Naelewa humu kuna wapotoshaji waliosomea, na pengine wanalipwa kwa kazi hiyo, ili ionekane Chadema imekosea njia. Mimi naamini kabisa mafanikio wanayoyapata (ukiachilia mbali kuukosa ubunge) ni makubwa na ya kujivunia.

Mkumbuke jambo moja: Upinzani Tanzania umejengwa zaidi kwa influence ya mtu mmoja mmoja, kama Seif Shariff kule Zanzibar, na Mrema huku Bara. Kudorora kwa hawa ndio imekuwa kudorora kwa vyama. Lakini kwa Chadema hali ni tofauti. Hiki ni chama-taasisi, na sio chama-mtu.
Kwa hilo tu, big up Chadema! Wasomi wengi na walalahoi watawafuateni.

Mkuu
Hii dhana iliyojikita miongoni mwa wachangia wengi ya kwamba kukosoa chadema basi utakuwa mpotoshaji ama unalipwa n i dhana potofu na ndio inapelekea hata kuhoji hivi ni kweli malalamiko ya wanachadema humu wengi kuhusu ubabe wa ccm ni kweli ama ni mwendelezo uleule.

Fikiri mtu humufahamu yupo wapi na ana fanya nini na yuko vipi na uhusiano na wanaoitwa mafisadi ,Ngoma inatoka huko moja kwa moja na shutuma kwamba eti wewe ni fisadi na unalipwa na mafisadi ,hivi kama wewe assume upo position hiyo ya anayeitwa ni fisadi harafu mtu anayekuita anakuja na malalamiko ya kuibiwa utamkubalia moja kwa moja hoja yake?

Harafu kingine sisi wadanganyika tunakubali kudanganywa kwa pipi kama watoto wadogo,hatukubali kukaa chini na kuhoji tulicho nacho.

Kwangu mie Vyama vyote vipo kwa masilahi ya watu wachache hakuna chama cha wanyonge hapo

Tunashindwa kuhoji na kubakia na ushabiki ule ule kwa kuwa hatuna nia thabiti tunayojaribu kuihubiri.
 
Invincible,
Mkuu nadhani umetuelewa vibaya. Mimi binafsi nawapongeza sanasana Chadmea kwa kazi kubwa waliyoifanya iwe majimbo yote ya Uchaguzi ambayo wameshikiri. Lakini hii sii dhamira ya mtazamo wangu wala mategemeo ya wananchi wengi. Tunachokitazama ni zaidfi ya hatua waliyofikia na kama kuna kwenda mbele zaidi ikiwa CCM wapo.
Mkuu CCM walishindwa na TLP wala sii muda mrefu ulopita na waliiba kura vile vile, leo hii Chadema wameingia na kuchukua kura zote za TLP lakini wameshindwa kuvuta toka CCM ndio maana CCM kaibuka mshindi iwe kaiba au hakuiba.. haya ya kuiba kura CCM hufanya chaguzi karibu zote na unatakiwa kumshinda kwa hesabu kubwa sana..Hivyo Chadema kimeweza kupiga hatua dhidi ya TLP na sii CCM (ambao wameibuka washindi) hii ndiyo reality nayojaribu kui explore..

Hivyo hivyo chaguzi za sehemu zingi zilizopita, utaona kwamba vita huanza na vita baina ya Upinzani, kisha wakagawanyika, CCM hingia kwa mlango wa nyuma wakaibuka washindi. Hii vita baina ya wapinzani ndio chanzo cha kushindwa. Wananchi hatutaki kuingia fainali wala kushiriki kwa vyama vya Upinzani tunachotaka sasa hivi ni kuonma suhindi unakuja upande huu. Hizi ahadi za Kikwete kutuhakikishia kwamba Tanzania itaingia World Cup mwaka 2010 wakati sisi wananchi hatuoni uwezo huo kuwepo ni mawazo ya kujenga tunapojadili na kuzungumzia mapungufu ya mchezo huo nchini...kamleta kocha wa nje na kadhalika hadithi ikasimama pale pale..Tanzania hakutufika hata fainali za nchi za Kiafrika..lakiuni muulize Kikwete na mawaziri wake kama alitegemea hali hii kutokea.. watakupa sababu mia kidogo na hawatakubali kwamba walifanya wao makosa hapa na pale..
Ndicho nachozungumzia mkuu wangu Waungane vichwa, chama au vyovyote vile vyama hivi vinatakiwa kusimamama pamoja (mshikamano) wakati wa uchaguzi na kuwa kitu kimoja against chama tawala..Laa sivyo CCM kila siku itaibuka mshindi kwa sababu CCM ina washabiki haina wapenzi wa nchi hii. Ndio maana tuna vazi la chama (njano na Kijani), hatuna vazi la taifa..Taifa bila CCM ni taifa lililopotea hii ndio imani ya dini inayotangazwa na huwezi kuwabadilisha kirahisi..
 
Back
Top Bottom