Kwanini CHADEMA watashindwa mapema kuelekea 2025 hata baada ya maandamano?

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Ndugu wanajukwaa,

Sio mara Moja au mbili maandamano kuonesha matokeo chanya huko duniani kiasi Cha kubadili kabisa hali na mfumo mzima wa maisha lakini pia yameonesha ni chaguo la mwisho la kufikisha ujumbe fulani kama machaguo mengine yameshindwa kutoa majibu.

Mahali pengine duniani ambapo maandamano yalifanikiwa au yamefanikiwa kulikuwa na hoja ya kuunganisha waandamaji, kulikuwa na sababu ya maandamano na kulikuwa na nia ya maandamano. Tofauti na kwingine duniani ambapo maandamano yalifanikiwa ,maandamano ya CHADEMA hayatakuja kufanikiwa kamwe kwa sababu kuu zilizotajwa hapo juu.

Tukianza, Kukosekana kwa hoja kuu ya maandamano. Hoja zinazosemwa zilizopelekwa maandamano ya CHADEMA ni kupanda kwa vitu na kupigia miswada ya Sheria za uchaguzi na upatikanaji wa katiba mpya. Mpaka hapo watu wanashindwa kuelewa ,hoja kuu ni ipi? Kwa mfano, kupanda kwa vitu kama sukari ni suala la muda na muda si mrefu litakwisha hivyo hoja ya kupanda kwa vitu itakosa mashiko. Hoja ya upatikanaji wa katiba mpya hili suala limetolewa ufafanuzi sana kwamba kutengeneza katiba mpya sio suala la kisiasa ila ni la utashi, weledi na utaalamu zaidi hivyo suala hili linaweza kuchukua muda mrefu kuliko inavyofikirika.

Hivyo mpaka sasa waandamaji hawaelewi zaidi ya kusukumwa na upepo unapovuma. Hawafahamu lengo kuu la maandamano na Kwa kuwa watanzania wana tabia ya kushiriki mambo hata yasiyowahusu basi yawezekana wengi wa waandamaji ni washiriki tu wasiojua wanachoshiriki.

Kama kukiwa na hoja kuu ya maandamano itasaidia kuvuta hisia na mitazamo ya waandamaji wengi na kupeleka ujumbe wa maandamano mahali pakubwa zaidi na lengo la maandamano kutumia.

Jambo lingine ni kukosekana Kwa sababu ya maandamano. Waandamaji na waandaa maandamano wana mitazamo tofauti juu ya maandamano lakini ukiangalia juu juu utafikiri wanaelewana na wapo pamoja kwenye sababu.

Kwa jicho lango la mtazamo, sababu ya waandamaji ambayo wanaamini kwenye maandamano ni kujaribu kushawishi Serikali juu ya changamoto za Sasa kama kukatika Kwa umeme na upatikanaji wa bidhaa Kwa Bei nafuu lakini hoja ya waandaaji wanaamini wanatakiwa kuingia madarakani wao na vyovyote iwavyo lazima waingie. Hapa inakosekana sababu kuu ,ya je sababu ya maandamano ni kuiondoa Serikali au kuishawishi Serikali?

Lengo la wananchi na waandamaji si kuiondoa Serikali bali ni kuishawishi Serikali na ndio maana yanapotatuliwa ya wananchi maandamano yanakuwa hayana maana.

Kingine ambacho CHADEMA wanashindwa kutambua ni kwamba vitendo vina nguvu na nguvu ya vitendo vya MAMA ni kubwa. Mama ni mtatuzi, msikivu na mjenzi Kwa sifa hizo sidhani kama maandamano ya nafasi na nguvu kwenye uongozi wake

Kutokana na hoja hizo tunagundua CHADEMA wanaandaa maandamano wakiwa hawana hoja kuu bali ni wanaendeshwa na matukio yanayojitokeza. Ushiriki wa watu ni kama wanasukumwa na wanapelekwa bila kujua kusudi na sababu kuu.

Kutokana na hayo inaonesha kabisa CHADEMA kitakosa mvuto baada ya hoja ya maandamano kupoteza ushawishi na licha ya maandamano Bado wanaweza wasipate ushindi wa kuridhisha 2025.

CHADEMA kimeamua kupeleka salamu Kwa njia ya maandamano na CCM kinapeleka salamu Kwa utatuzi wa kero na changamoto na hiki ndio kipimo Cha wapigakura uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu 2024 na Uchaguzi mkuu mwakani.
 
"kutengeneza katiba mpya sio suala la kisiasa ila ni la utashi, weledi na utaalamu zaidi hivyo suala hili linaweza kuchukua muda mrefu kuliko inavyofikirika". Kama uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo basi wewe ni gwangara yaani nysngarakasha lisilo na faida kwa nchi yako, hilo bichwa lako linachojua ni katiba za nchi zipo kwa ajili ya siasa tu! Wewe si ridhiki.
 
Jibu maswali yafuatayo
Hapo ulipo sukari ipo? Nusu kilo shilingi ngapi?
Nauli kutoka ulipo kwenda kwenye shughuli zako shilingi ngapi?
Umeme upo hapo ulipo?
Maji je yapo?
Una kazi maalum au unashinda mtaani ukinywa vismart na double kiki?
Maswali ni mengi
 
Cdm watashindwa 2025, kwani Tanzania Kuna uchaguzi au ni maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura?
 
CHADEMA haiwezi kuishinda CCM ila wanachotakiwa kufanya kuepuka kushindwa na njia Moja mojawapo ni kujichosha mapema maana siasa ni kama mpira mara nyingine inabidi ujilinde kuliko kushambulia
 
Jibu maswali yafuatayo
Hapo ulipo sukari ipo? Nusu kilo shilingi ngapi?
Nauli kutoka ulipo kwenda kwenye shughuli zako shilingi ngapi?
Umeme upo hapo ulipo?
Maji je yapo?
Una kazi maalum au unashinda mtaani ukinywa vismart na double kiki?
Maswali ni mengi
Maswali ni mengi kweli lakini jibu ni Moja katika uchumi wa soko" market economy" Bei ya bidhaa zinatokana na "forces of demand and supply" , demand ikiwa kubwa supply ikawa ndogo hapo Moja Kwa Moja kutakuwa na ongezeko pa Bei na kinyume chake ni sahihi na kupanda Kwa Bei ni hali ya soko na kanuni zake.

Ukielewa hivyo utagundua kupanda Kwa Bei kwa bidhaa ni hali ya mpito tu
 
"kutengeneza katiba mpya sio suala la kisiasa ila ni la utashi, weledi na utaalamu zaidi hivyo suala hili linaweza kuchukua muda mrefu kuliko inavyofikirika". Kama uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo basi wewe ni gwangara yaani nysngarakasha lisilo na faida kwa nchi yako, hilo bichwa lako linachojua ni katiba za nchi zipo kwa ajili ya siasa tu! Wewe si ridhiki.
Kama unaamini utengenezaji wa katiba ni suala la utashi wa kitaalamu mbona unapelekwa na mihemko ya kisiasa?
 
CHADEMA haiwezi kuishinda CCM ila wanachotakiwa kufanya kuepuka kushindwa na njia Moja mojawapo ni kujichosha mapema maana siasa ni kama mpira mara nyingine inabidi ujilinde kuliko kushambulia

Cdm iishinde ccm kwani kuna uchaguzi au upuuzi kama upuuzi mwingine.
 
Jibu maswali yafuatayo
Hapo ulipo sukari ipo? Nusu kilo shilingi ngapi?
Nauli kutoka ulipo kwenda kwenye shughuli zako shilingi ngapi?
Umeme upo hapo ulipo?
Maji je yapo?
Una kazi maalum au unashinda mtaani ukinywa vismart na double kiki?
Maswali ni mengi
Maswali ya msingi sana haya
 
Hii kaandika binadamu anaepumuq au msukule wa lumumba??
Maana sijui kala magarage ya wapi
 
Marekani wanaandamana baada ya mafuta kupanda ndani ya week1 vipi sukari miezi6 now uiite mpito we kenge maji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom