Cancer inachukua maisha yangu

Cancer inachukua maisha yangu

Baada ya kusumbuka kwa takribani wiki tatu sasa, afya yangu ikiharibika kwa kasi huku mimi binafsi,vipimo na ushauri wa madoctor ukionyesha ni uchovu tu au tatizo la kawaida Jana nimekuja kufanya vipimo hapa Nairobi na inaonyesha nina cancer katika figo langu.

Ninarudi nyumbani kesho, nitajitahidi kuendelea na maisha yangu kama kawaida, lakini huu ni ukweli mbaya sana, cancer is haunting my life.

pole sana ndugu yangu, nakutia moyo kuwa Mungu aliyeiumba hiyo figo anaweza kuifanya upya tena, nenda kwenye vituo vya maombezi vya walokole watakuombea, kitu kikubwa ondoa hofu maana ni kitu hatari sana kwani inaua kuliko ugonjwa
 
Sina sababu ya kukupa Pole kwa Mara ya pili bali Jina la bwana Yesu lihimidiwe maana ulikuwa umekufa naye amekuisha. Endelea kumwani Yesu nawe utakuwa salama siku zote. Asante Yesu kwa ajili ya Mtumishi wako Sangarara
 
Last edited by a moderator:
This is the best news ever. My ever famous life line : YOU ARE NEVER DEFEATED UNTIL YOU GIVE UP.
namshukuru Mungu kwa ajili yako. Akuponye, akutetee, arudishe kile ambacho mwovu amekuibia.
 
Wow! Glory to Almighty God! Namshukuru Mungu sana kwa ajili yako sangarara.Nilivyosoma thread yako kwa kweli niliumia kiasi cha kutokwa machozi.Lakini sasa nimefurahi sanaaaaa kweli Mungu ni mwema wakati wote.Nakutakia quick recovery
 
Ashukuriwe yeye muumba mbingu na ardhi na viumbe tuliomo!!!!!

Mkuu Sangarara muumba katupa somo kupitia wewe!!!

Pole kwa uliyopitia na karibu tena jukwaani
 
Sifa, nguvu na utukufu ni vyake Mwenyezi Mungu tunamshukuru kwa kukurudishia afya njema. Habari njema sana hii hongera mdau
 
Mkuu Sangarara,
Pole na changamoto.

Tafadhali zingatia haya:
1. Iwapo hujafanyiwa operation na kutolewa sample ikathibitishwa maabara si sahihi kusema una cancer. Hapo unakuwa na UVIMBE ambao biological nature yake haifahamiki, ila tu inahisiwa kuwa cancer.

2. Mgonjwa siku hizi yanageuzwa biashara. Usiingie kwenye mtego kununua products ambazo hazijawa scientifically objectively proven kutibu tatizo lako.

3. Don't jump from hospital to hospital or from doctor to doctor. Ingefaa zaidi uendelee na hospitali hiyohiyo waliyokudiagnose.

4. Don't give up. Fight on. Cancer nyingi hutibika kwa operation, radio au chemotherapy. Modern medicine inatoa options za kuboresha maisha ya wagonjwa wa cancer kwa kiwango cha juu sana.

ZeMarcopolo
Mungu ni Mwema sana, thanks for this insightful comment.
 
Pole sana ili ukitaka usiumwe tena na maradhi yoyote yale mwilini mwako fanya hivi: Kila siku unapoamka Menya punje 1 ya kitunguu saumu kisha ukimeze hicho kipunje kimoja kila siku hutawea tena kuuguwa na maradhi yoyote yale jaribu kisha uje unipe Feedback.

mkubwa naomba ufafanuzi inatakiwa KUKIMEZA BILA KUTAFUNA AU KUTAFUNA NA KUMEZA, ninangojea ufafanuzi wako ili nianze utekelezaji, aksante
 
mkubwa naomba ufafanuzi inatakiwa KUKIMEZA BILA KUTAFUNA AU KUTAFUNA NA KUMEZA, ninangojea ufafanuzi wako ili nianze utekelezaji, aksante
Kimenye kisha kitobowe toboe kidogo kitoe maji maji kidogo kisha ukimeze kwa kunywa pamoja na maji .
 
Dah, very sad, pole sana mkuu. hii inatia hofu kwamba hospitali zetu za nyumbani kuna kasoro nyingi ikiwa ni pamoja na vifaa na utaalamu. usikate tamaa mkuu, inawezekana sio cancer labda ni infection tuu, na ni vizuri imegundulika mapema hivyo ni rahisi kupata matibabu na tatizo huenda likaisha kabisa kama sio kuwa under control. Nadhani itakuwa rahisi sasa kwa wataalamu wetu wa nyumbani kwa msaada wa majibu na vipimo ulivyofanya Nairobi kukusaidia. Mtangulize mungu kwa hili na usikate tamaa na kuona your life has reach an end, hofu nayo inaweza kukusababishia tatizo lingine au kuongeza tatizo.
Thanks Kiranga, I am forced to go through critical analysis and verification of these results,I went to the best hospital in DAR the whole of last week but nothing nearing this problem came into their sight.
 
Pole mkuu.

You may want to get a second opinion and verify the stage and what your options are.

I am not encouraging self diagnosis, false hope or doubting doctors, but it is worth getting as much information as you can and verification of the information given by doctors.

Kidney Cancer Symptoms, Causes, Treatment - How is kidney cancer staging determined? - MedicineNet

Shukrani Sana kiongozi.
Hii link imenisaidia Sana Sana I'm a peripheral neuropathy patient for 4 years time.
 
Unaendeleaje Sangarara?

Feedback itatuongezea nguvu ndugu yetu ya kuendelea na maombi!

Mungu akutie nguvu akuondolee hofu na akupe faraja yake na zawadi ya inani yake kuu kwamba.... Yote yawezekana kwake aaminiye!
 
pole sana ndugu yangu, nakutia moyo kuwa Mungu aliyeiumba hiyo figo anaweza kuifanya upya tena, nenda kwenye vituo vya maombezi vya walokole watakuombea, kitu kikubwa ondoa hofu maana ni kitu hatari sana kwani inaua kuliko ugonjwa

Ni kweli nenda ukaombewe ila usiishie hapo tu umpe na Yesu maisha wish you all the best.
 
Mungu ashukuriwe sana kwa kufanikisha matibabu yako kwenda salama salmini na kuweza kurudi katika afya yako ya awali.

Hauna haja ya kutokwa machozi tena, Jitie nguvu na umtukuze Mungu, Baada ya kuishi kama mfu kwa zaidi ya wiki mbili, nimekuwa mzima tena na habari ya kansa haiko nami tena.
 
Back
Top Bottom