Chloroquine
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 217
- 112
Baada ya kusumbuka kwa takribani wiki tatu sasa, afya yangu ikiharibika kwa kasi huku mimi binafsi,vipimo na ushauri wa madoctor ukionyesha ni uchovu tu au tatizo la kawaida Jana nimekuja kufanya vipimo hapa Nairobi na inaonyesha nina cancer katika figo langu.
Ninarudi nyumbani kesho, nitajitahidi kuendelea na maisha yangu kama kawaida, lakini huu ni ukweli mbaya sana, cancer is haunting my life.
Pole sana mkuu nakubaliana nawe kabisa ni ukweli mbaya ila naamini kama vipimo vilifanyika vizuri na wakaweza kufanya diagnosis kujua ni stage ipi huo ugonjwa upo kwa sasa ni rahisi kupata tiba appropriate hivyo shaka ondoa kwani tiba zipo na utapona kabisa mkuu. Uwe na tumaini tu na pia mwamini Mungu yeye ni mponyaji wakati sie tunatibu.