Cancer inachukua maisha yangu

Cancer inachukua maisha yangu

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
Baada ya kusumbuka kwa takribani wiki tatu sasa, afya yangu ikiharibika kwa kasi huku mimi binafsi, vipimo na ushauri wa madoctor ukionyesha ni uchovu tu au tatizo la kawaida. Jana nimekuja kufanya vipimo hapa Nairobi na inaonyesha nina cancer katika figo langu.

Ninarudi nyumbani kesho, nitajitahidi kuendelea na maisha yangu kama kawaida, lakini huu ni ukweli mbaya sana, cancer is haunting my life.
 
Poleee mi pia huwa najiskia kuchoka sana sijui tayari??????
 
Pole sana. Ila usiishie hapo, pamoja na maombi fanya vipimo zaidi ili kujua kama ni cancer kweli na imefikia hatua gani na nini kifanyike. Pia anza kufuatilia natural therapies for cancers.
 
Pole mkuu.

You may want to get a second opinion and verify the stage and what your options are.

I am not encouraging self diagnosis, false hope or doubting doctors, but it is worth getting as much information as you can and verification of the information given by doctors.

Kidney Cancer Symptoms, Causes, Treatment - How is kidney cancer staging determined? - MedicineNet

Thanks Kiranga, I am forced to go through critical analysis and verification of these results,I went to the best hospital in DAR the whole of last week but nothing nearing this problem came into their sight.
 
Kuna tiba asilia imekuwa ikizungumzwa sana mitandaoni. I cant vouch for it but it can be real. Naomba nitoe dokezo wanaojua waendeleze: kutumia tunda, majani na/au magome ya mstaferi (soursop). Google it and try it. Katika 100 mimi binafsi naipa 85.
Pole ndugu yangu
 
Pole sana, ila kuwa na imani kwa mwenyezi Mungu kwani yeye ndo ajuae undani wa maisha yetu.
 
Nimeumia jamani nimeumia sana Specialist mkubwa muhimbili proffessor Mkony he is the best lakini hujasema imefikia stage gani????i hope its early stage
 
Pole sana, ila kuwa na imani kwa mwenyezi Mungu kwani yeye ndo ajuae undani wa maisha yetu.

Hapa panaitajika God's intervention. Mlilie sana Mungu, nae atafanya, kwani wewe si wa kwanza na unaweza kuwa shuhuda mzuri sana hapa JF.
 
daaa pole sana mkuu bila shaka unatakiwa kuwaona wataalam wa kansa ili wakwambie cha kufanya.

usikate tamaa God is with you.
pole sana.
 
Nimeumia jamani nimeumia sana Specialist mkubwa muhimbili proffessor Mkony he is the best lakini hujasema imefikia stage gani????i hope its early stage

Kesho ndo nitapata detailed report, but I know it is complicated already. Nitaenda hapo Muhimbili pia.
 
Dah, pole sana ndugu! Ushauri uliotolewa na waliotangua hapa hasa wa kupima tena kwa mara ya pili ni muhimu sana na kuweza kuhakikisha ukubwa wa tatizo na namna ya kulikabili! Lakini yote kwa yote cancer ni ugonjwa mbaya ila kuna baadhi ya mitishamba inaponya ugonjwa huu kama una bahati!

Mzazi wangu alionesha dalili za tatizo hilo kabla hazijathibitishwa tukaelekezwa kwa mtaalam wa mitishamba akampatia dawa, sasa anaendelea na uzee wake kama kawaida dalili zile zilitoweka na maumivu makali yaliyokuwa yanaambatana na dalili hizo yalikwisha leo ni zaidi ya miaka 8 au 9!

Pole sana.
 
Kama unaamini dawa za tiba mbadala i know the guy unaweza kuni pm then nitakutafutia namba yake nikupe umtafute ujaribu

au unaweza kwenda kwa wale jamaa wa celagerm

au
dynapharm
nenda J Mall wapo pale hata kama hautapata XYZ ila angalau utakuwa umepata ABC
 
Back
Top Bottom