Biashara ya Kuuza Nyama (Butcher's Shop): Mambo Mbalimbali ya Kujifunza

Habari wadau!

Kabla ya kuingia kwenye hii biashara ningeomba kufahamu mambo kadhaa kutoka ka wadau ambao wana uzoefu katika hii biashara.

Mambo ambayo ningependa kufahamu ni:
  1. Usimamizi, hasa kama unamuweka mtu wa kuuza.
  2. Manunuzi na kufikisha mzigo kwenye duka.
  3. Ushindani katika soko.
  4. Faida na hasara.
  5. Changamoto nyiginezo.
Karibu wadau tuelimishane hasa katika sekta hii.
 
1.Nikupe hongera kwanza kwa kutaka kujiajiri ila nikupe dokezo na Tahadhari hapo kwa usimamizi lazima mwenyewe uwepo nikimaanisha uwe na usimamizi wa karibu zaidi.

2. Kuhusu nyama nunua tu vingunguti ama ukonga km unaishi Dar es salaam kg machinjion 4,500 mpaka 5,000 unaweza pata connection na gari yaan wasambazaji nyama kwa gari wakakuletea mpaka ulipo.

Kwa upande wa samaki nenda ubungo River side sato kg 8,000 na sangara 4,500 kwa kg km ukizoea utapata connection ya wauzaji wanaoleta mojakwamoja huwa wanauza

Sato 5,500 sangara 4,000 note hizi bei ni za jumla rejareja Sato 10,000 kwa kg na Sangara 8,000 nyama rejareja 6,000 sehemu zengine 7,000

3. Ushindani sio mkubwa ila vyema ukawa na Machine ya kukatia nyama, ofisi layout iwe nzuri, Muuzaji awe mchangamfu hapo utakuwa umewapa pigo washindani wako.

4. Faida nafikiri ushajua kwa nyama faida 1,000 kwa kg kwa samaki Sato ni 2,000 km unanunua riverside sangara 3,500 kwa kg Hasara zipo nazinakuja kutokana na miundo mbinu ukikatika umeme jua nimaafa

5. Changamoto zipo nyingi sana kwanza ukikosea kuchagua eneo yaani ukifail kuchagua location ya ofisi yahiyo butcher basi jua ni hasara kwenda mbele, Pili wauzaji sipendi kuongelea vibaya watani wangu wagogo ila usije kumueka Mgogo buchani kwako kama huna usimamizi wa karibu atakufilisi nasema tena atakufilisi kuepuka hilo tafuta machine unaweza weka yoyote akauza. Usinambie kama nafanya lahasha namuona Kaka angu anavoendesha

Kama wewe ni mgogo utanisemehe jamani
 
Nimesikia magogo marufuku je kama ni kweli mbadala wake utakuwa ni nini
Fungua mkuu inalipa vizuri tu ila inahitaji usimamizi mzuri na usafi wa hali ya juu
 
fakalava,

Nimeanza biashara hiyo mwez uliopita,mm nipo mkoani huku unachinja Ng 'ombe mzima peke yako kikubwa unakua na bucha zaidi ya moja za kuuzia,unatundika kiasi kiasi unatunza kwny friza mapema kabla haijakaa muda mrefu, unamalizia siku ya pili kuuza nyama inakua km ya leo.kikubwa usikosee kwny bei ya kununulia mnyama. Faida laki au 80 baada ya siku mbili ni kawaida
 
Nimeanza biashara hiyo mwez uliopita,mm nipo mkoani huku unachinja Ng 'ombe mzima peke yako kikubwa unakua na bucha zaidi ya moja za kuuzia,unatundika kiasi kiasi unatunza kwny friza mapema kabla haijakaa muda mrefu, unamalizia siku ya pili kuuza nyama inakua km ya leo.kikubwa usikosee kwny bei ya kununulia mnyama. Faida laki au 80 baada ya siku mbili ni kawaida
Asante Mkuu! Nitakutafuta kwa msaada zaidi.
 
Back
Top Bottom