Biashara ya Kuuza Nyama (Butcher's Shop): Mambo Mbalimbali ya Kujifunza

Nataka kufunga baadhi ya biashara nilizo nazo kwa sababu zimekuwa zikijiendesha kihasara kwa mda Sasa, nikafikiria kuanza biashara ya nyama.

Nafikiria kujenga mabucha ya kisasa, natafta eneo najenga zizi kwa ajili ya kuhifadhia ng'ombe ambao nitaajiri watu wa kwenda kununua mnadani na watahifadhiwa humo kabla ya kuchinjwa, nataka nianze na ng'ombe zaidi ya 60 kwa kuanzia.

Then ng'ombe watakaochinjwa watapelekwa kwenye mabucha yangu na pia nitakuwa nachakata nyama kwa ajili ya kusambaza kwenye masupermarket.. japo bado sijajua kiundani soko na changamoto ya biashara hii, naombeni wajuzi wa biashara hizi mnifahamishe na mkoa gani ambao biashara hii inafanyika vizuri zaidi.

Napenda kujua pia Kama biashara hii itanilipa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa, but napenda ungenifahamisha changamoto zake na namna ya kuifanya
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni biashara nzuri kama una mtaji mzuri wa kuwekeza kisasa hususani kwenye miundombinu hasa Abbattoirs "Machinjio", magari ya usambazaji "Nyama tu" na rasilimali watu kama EHOs, Afisa mifugo na vifaa vya kuchinjia.

Dodoma kuna machinjio nzuri na za kisasa, unaweza kuzitembelea ukajifunza.

Bila kusahau watu wa TFDA, NEMC, Meat Board na Afisa Afya watakuwa karibu nawe kila wakijisikia.
 
Ni biashara nzuri kama una mtaji mzuri wa kuwekeza kisasa hususani kwenye miundombinu hasa Abbattoirs "Machinjio", magari ya usambazaji "Nyama tu" na rasilimali watu kama EHOs, Afisa mifugo na vifaa vya kuchinjia.

Dodoma kuna machinjio nzuri na za kisasa, unaweza kuzitembelea ukajifunza.

Bila kusahau watu wa TFDA, NEMC, Meat Board na Afisa Afya watakuwa karibu nawe kila wakijisikia.
Vipi Kuhusu faida yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi Kuhusu faida yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hapa unepewa mwanga tu, si unajua mfumo mfumo wetu wa machinjio dar ni maeneo maalum tu, hii yako itakuwa mpya.

Ila siamini kama haiwezekani. Kwa kuanza anza na watu wa manispaa,usikie wanasema nini kuhusu eneo jipua kwa ajiri ya machinjio. The rest ni mteremko.
 
Mkuu hiyo biashara ni nzuri sana tatizo linokuja kudhoofisha biashara ni suala la Parking ya nyama

Changamoto kubwa hiko hapo bado wa Tz hatuwezi ku design parking nzuri ya product kama ya nyama ndio maana katika Supermarket zetu wanauza sana nyama ya Nje kwasababu ina kidhi viwango vya kimataifa

Ushauri wangu

1. Jenga banda sehemu yenye ardhi ya kutosha ambayo pia kuwe na Majani ya kutosha ( ranch kidogo hivi unakipiga na fensi)

2. Jenga Machinjio madogo ya kisasa

3. Tafuta alternative source of energy usitegemee umeme wa tanesco kwa sababu bucha za kisasa zinatumia mashine kukatia nyama na sio vigogo na hizo mashine zinatumia umeme kwaiyo ukitegemea umeme wa Tanesco unaweza ukakaa siku bila kufanya kazi

4. Kuusu Parking nenda TFDA kuna wataalam watakupa ushauri wa jinsi gani unaweza kufanya parking ya International standard

5. Usikope hela bank kwaajili ya kuanzisha biashara hii inaweza ikakugharimu biashara ikawa ngumu mwanzoni alafu jamaa wakaanza kukuchachamalia mwishowe ukamwaga manyanga

6. Fanya Study tour nakushauri nenda pale SUA (Moro) yuko Professor mmoja Ana mradi mkubwa wa hii kitu na anapiga hela ndefu sana atakupa muongozo wa kila kitu usitegemee ushauri wa hapa JF tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Witmak255,

Kama unaweza kufanya kila kitu kinachohitajika kwenye biashara hii kikamilifu, ni biashara nzuri. Unapaswa kuwa na mabucha yako, machinjio, maduka au wateja kama supermarkets. Pia unapaswa kuweza kukata nyama kitaalamu kwa kutumia machine na kuzipaki vizuri. Pia usisahau kwamba utahitaji freezers kubwa kuweza kuhifadhi nyama kabla ya kuuza.

Biashara hii inahitaji uwe na gari/magari yako, moja la kubeba ng'ombe na jingine kusafirisha nyama kwa wateja. Vyote hivi vinahitaji uwekezaji mkubwa.

Sikushauri uanze na ng'ombe 60 ni wengi mno kama huna miundombinu na nyenzo nyingine utapata shida na pengine hasara.
 
Back
Top Bottom