mkabasia
JF-Expert Member
- Mar 11, 2014
- 2,817
- 2,379
Samahani mkuu kama hutojali.Hao Samaki Kwa bei ya jumla ni river side maeneo gani!wanauza kuanzia kg ngapi mi nataka Kwa matumizi ya nyumbani.1.Nikupe hongera kwanza kwa kutaka kujiajiri ila nikupe dokezo na Tahadhari hapo kwa usimamizi lazima mwenyewe uwepo nikimaanisha uwe na usimamizi wa karibu zaidi.
2. Kuhusu nyama nunua tu vingunguti ama ukonga km unaishi Dar es salaam kg machinjion 4,500 mpaka 5,000 unaweza pata connection na gari yaan wasambazaji nyama kwa gari wakakuletea mpaka ulipo.
Kwa upande wa samaki nenda ubungo River side sato kg 8,000 na sangara 4,500 kwa kg km ukizoea utapata connection ya wauzaji wanaoleta mojakwamoja huwa wanauza Sato 5,500 sangara 4,000 note hizi bei ni za jumla rejareja Sato 10,000 kwa kg na Sangara 8,000 nyama rejareja 6,000 sehemu zengine 7,000
3. Ushindani sio mkubwa ila vyema ukawa na Machine ya kukatia nyama, ofisi layout iwe nzuri, Muuzaji awe mchangamfu hapo utakuwa umewapa pigo washindani wako
4. Faida nafikiri ushajua kwa nyama faida 1,000 kwa kg kwa samaki Sato ni 2,000 km unanunua riverside sangara 3,500 kwa kg Hasara zipo nazinakuja kutokana na miundo mbinu ukikatika umeme jua nimaafa
5. Changamoto zipo nyingi sana kwanza ukikosea kuchagua eneo yaani ukifail kuchagua location ya ofisi yahiyo butcher basi jua ni hasara kwenda mbele, Pili wauzaji sipendi kuongelea vibaya watani wangu wagogo ila usije kumueka Mgogo buchani kwako kama huna usimamizi wa karibu atakufilisi nasema tena atakufilisi kuepuka hilo tafuta machine unaweza weka yoyote akauza. Usinambie kama nafanya lahasha namuona Kaka angu anavoendesha
Kama wewe ni mgogo utanisemehe jamani