Najibu hoja za wadau kuhusu biashara ya kunenepesha ng'ombe Tanzania

Mfugaji123

Member
Apr 3, 2020
10
18
Baada ya kuandika article kuhusiana na biashara ya kunenepesha ng’ombe nimepata maswali mengi kuhusiana na biashara hii. Wengi wanahoji inafanyikaje, ukubwa wa mtaji, vihatarishi vyake, unaweza kukosa wateja na wengine mtu anaweza kuanza akiwa na mtaji kiasi gani?.

Sasa biashara yoyote kitu cha muhimu ni lazima ufahamu mbinu za kufanya biashara hiyo , suala la mtaji huwa na la mwisho kabisa. Maana biashara haifanywi kwa mtaji tu japo ni muhimu. Tuanze hivi

Biashara ya kunenepesha ng’ombe wa kienyeji inaweza kufanyika kwa namna mbili kuu;

1: Kufanya uzalishaji na kunenepesha mifugo shambani kwako. Yaani hapa unaweza kuboresha ng’ombe wa kienyeji kwa kutumia mbegu za koo bora za ng’ombe ( Ng’ombe wa kisasa). Baadaye kabla hujawauza unawanenepesha ili kuongeza thamani katika soko. Kama nilivyotangulia kusema kwenye chapisho lililopita msingi wa kunenepesha upo katika mambo mawili, kuongeza uzani wa ng’ombe na kuboresha nyama yake.

Kwa mfano ng’ombe mwenye kg 150 anaweza kunenepeshwa akafikisha kg 200-220 ndani siku 90. Hizi kg
zinazoongeza ndiyo faida yake . Na pia huwa na mwonekano mzuri unaovutia. Wanunuzi wengi wa ng’ombe huangalia mwonekano ( umbo la ng’ombe) kwa nje katika kufanya maamuzi wa kununua ng’ombe.

Kwa wataalam wa nyama, wao wanajua nyama ya ng’ombe alieyenenepeshwa huwa na sifa nzuri za nyama; mfano huwa imara (nyama isiyotepeta), isiyokonda (nyama nene iliyoshiba), nyama yenye wekundu mkali (isiyopauka), nyama laini ( yenye mwonekano laini kila mahali) na yenye kiwango kizuri cha mafuta. Nyama ya namna hii huweza kuuzwa katika masoko ya kimataifa na ikiuzwa katika masoko ya ndani inaweza kuuzwa kwa bei juu kuliko nyama ya kawaida

2: Kununua ng’ombe , kunenepesha na kuuza. Kulingana na ripoti za wizara ya mifugo kwa msimu wa mwaka
2022/2023, Tanzania ilikuwa na ng’ombe milioni 36.6. Ng’ombe hawa ni wengi katika kufanya nao biashara. Unachofanya ni kununua ng’ombe wakati bei ipo chini. Baada ya kuwanunua unawanenepesha kisha kuwauza. Muda wa kunepesha unaweza kuwa siku 50, 75, 90 au zaidi kulingana na target yako sokoni.

Suala la masoko, kwanza ng’ombe hana stress kabisa hata ukiona wateja hakuna au hakuna anayeweza kufikia soko unaweza kuamua kumuacha shambani na kusubiri bei nzuri. Hata hivyo ni muhimu kulenga msimu mzuri wa kuuuza ng’ombe ili kuepuka gharama kubwa za uendeshaji. Uzuri ni kama soko la ng’ombe kubwa sana Tanzania. Biashara za ng’ombe hufanyika kila siku shida ni kuwa ng’ombe bora wa kuchinja bado ni changamoto. Ng’ombe wengi wanaochinjwa katika machinjio yetu hawa sifa zozote za kuchinja lakini ndo tulio nao.
Fursa za masoko ya nyama ya ng’ombe ni kama ifuatavyo;
1:Kuuza nyama nje ya nchi ndani ya bara la Afrika: Mahitaji ya nyama ya ng’ombe ni makubwa katika
nchi zingine za bara la Afrika. Mathalani, nchi zinazohitaji kwa wingi nyama ya ng’ombe ni Misri, Algeria,
Libya, Senegal, Ghana na Nigeria. Afrika ya Kusini hufanya vizuri katika soko hili; huuza nyama Misri,
Zimbabwe, Nigeria, Lesotho n.k.

2:Kuuza nyama nje ya bara la Afrika: Kuna ongezeko la soko la nyama nje ya nchi hasa katika nchi za
China, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain, Kuwait, Oman, Comoro, Hong Kong, Jordan na
Saudi Arabia. Mathalani, Saudi Arabia zaidi ya tani 700,000 na Tanzania ina nafasi nzuri ya kuhudumia soko hilo

2.Fursa ya Ndani ya Nchi. Kwa makadirio ya 2022 , ulaji wa nyama kwa Tanzania kwa mtu mmoja ni kg 12 kwa mwaka chini ya kiwango cha kg 50 kinachopendekezwa na FAO. Kwa takwimu hizi, Tanzania hula tani zaidi ya 700,000kwa mwaka huku mahitaji kamili yakiwa tani takribani milioni 3. Kulingana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), mahitaji ya ndani ya nchi ya nyama kwa ujumla ni tani milioni 2.90 kwa mwaka na kufikia mwaka 2030, yanaweza kufikia takribani tani milioni 4.80.

Dar Es Salaam: Mkoa wa Dar Es Salaam ni mlaji mkubwa wa nyama ya ng’ombe nchini. Zaidi ya nyama tani 70,000 huliwa na Dar Es Salaam pekee, wakati mahitaji yakiwa ni tani 300,000 kwa mwaka.

Dodoma: Dodoma hutumia tani tani 36,000 za nyama kwa mwaka lakini mahitaji kamili ni tani 150,000 kwa mwaka. Pia, Kuna machinjio yenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 300 na mbuzi na kondoo 200 kwa siku. Uwepo wa machinjio hayo umesababisha kuwepo kwa mahitaji makubwa ya mifugo bora kwa ajili ya nyama na mazo mengine yatokanayo na mifugo. Hii inatoa fursa katika kuanzisha mashamba ya uzalishaji na kunenepesha mifugo.
Morogoro: Morogoro pia hutumia zaidi ya tani 36,000 za nyama lakini mahitaji yake halisi ni takribani tani 150,000 Mkoa wa Morogoro una idadi ya ng’ombe takribani milioni 1.1. Mkoa una manchinjio 19. Kuna kiwanda cha Nguru cha nyama ambacho kina uwezo wa kuchinja ng’ombe 100 na mbuzi 1000 kila siku. Kiwanda hiki kinatoa fursa ya kunenepesha na kuuza mifugo kiwandani.
Arusha: Arusha hutumia zaidi ya tani 27,000 kwa mwaka lakini mahitaji yake halisi ni takribani 115,000.
Mwanza : hutumia zaidi tani 43,000 kwa mwaka wakati mahitaji halisi kwa mwaka ni takribani tani 180,000 kwa mwaka.
Kwa ujumla, kuna mahitaji nyama ni makubwa katika mikoa yote Tanzania na kwa kuwa nyama ya ng’ombe huchukuwa takribani asilimia 70 ya nyama zote zinazozalishwa na kuliwa nchini, hivyo basi ina tija ya kubwa ya kibiashara.

Kwa yule anayependa kujua kwa undani juu ya biashara za unenepesha tumekuandalia ripoti ya Upembuzi yakinifu ya Unenepeshaji ng’ombe Tanzania (Feasibility Study Report of Cattle Fattening Project Tanzania, 2024), humu utaona upembuzi wa mambo yote muhimu ikiwemo Project rationale, operational feasibility, market feasibility, Technical feasibility na Financial Feasibility.

Pia kuna mwongozo wa unenepeshaji wa ng’ombe utakaokusaidia hatua kwa hatua kujifunza na kutekeleza program ya unenepeshaji shambani kwako. Pia tutakusaidia kuandika business plan kwa aajili ya mkopo au mpango binafsi wa biashara.

Tupigie simu/Whatsapp: 0621106923
images (18).jpeg
 

Attachments

  • mock-00496-12383.png
    mock-00496-12383.png
    1.3 MB · Views: 6
Back
Top Bottom