Hivi ben hajajitokeza kukanusha ama kuthibitisha habari hii?Yaaaa..........umuofia kwako.......tunaomba ututajie msiri wako mkuu aliyekupenyezea. Najua hawezi kwenda ACT kwa sababu alibumbulua mipango ya zitto....enzi zile wakati wanatumiwa hela.
Haiwezeka kwa mtu makini kama ben akafanya ujinga kama huu!
Kama ni kweli BEN amejitambua
Mkuu King Kong, April Fools si iliishapita?, hivi inaruhusiwa kuiendeleza hadi leo?!. Kusema ukweli kuna type fulani ya uongo ukiutunga, hata msomaji anaweza kuelewa kabisa, kuwa mwandishi sio timamu!, niliwahi kusema mara nyingi humu, mtu kuwa kichaa, sio lazima hadi aokote makopo!.
Mode, vitu kama hivi kuendelea kuachwa ndivyo vinavyoshusha hadhi ya jf!.
Ben Saanane
ni memba humu, his ability, capability na misimamo yake inafahamika humu!!.
Pasco
Familia yangu ya Facebook,Marafiki wa
karibu na wa mbali kwenye mitandao na nje ya
mitandao,Salaaam! Kwa rehema na mapenzi yake Mwenyezi
Mungu na kwa dhamira ya kweli,moyo usiotetereka katika hali
yoyote kimapambano,Ndani ya masaa 72 nitatangaza
Maamuzi. Nitawaomba mniunge mkono katika maamuzi
hayo.Ni makini na sahihi.Yatakua matamu na machungu kwa
baadhi ya watu.Nimedhamiria...! The storm will pass,the
spring will come. Let the nature of patience be an
encouragement as you continue to wait. Aluta Continua,Victor
y Ascerta.... Ben
Saanane ni Jemedari wa Ukweli, bonge la Strategist, hana tamaa za kijinga, hupanga karata zake kwa umakini mkubwa ... Kamwe hawezi kuhama CHADEMA ...
Ben kuhamia chama kingine ni haki yake ya msingi, silisemei hilo. lakini hicho unachosema kinamhamisha "mission" za chama , hayo ni maneno tuu hata kwenye khanga yapo.
kwa hii sheria mpya ya mitandao sasa hivi unatakiwa uwe jela!
BEN SAANANE nakuomba uje mkuu utoe huu ukakasi.
sema neno moja tu na roho zetu zitapona
Umenielewa lakini nilichokiongelea au umekulupuka tu?nimezungumzia uongozi wa chama siyo ubunge!CHADEMA mkiendelea na huu ubishi wenu mtakiua hiki chama.Mjifunze kusikiliza na kuelewa, that groupthink you are creating will be the downfall of CHADEMA.
Amini usiamini mkuuu, ni pigo kubwa sana kumpoteza kijana makini kama Ben Saanane hapa ni lazima tujitafakari.
Bila Shaka Mtoa Mada Unatumia Pombe Kali, Mpaka Imepelekea Kuharibu Ubongo.
Aceni uoga BEN hawezi kuhamia chama cha wasaliti hata siku moja.Itakua ni maamuzi ya kutangaza nia ya kuliwania jimbo la Rombo
Nilishaleta uzi hapa kuhusu Ben Saanane kuhamia ACT Wazalendo mods wakaufuta, ni kweli ben anahamia ACT. Ben anapata upinzani sana ndani ya Chadema tena kutoka Chadema kanda ya Kaskazini Arusha. ACT ndio chama sahihi kwa Ben kuweza kutimiza ndoto zake za kuwa mbunge wa Rombo
Acheni story za kikuda na kumlisha mtu maneno,Kamanda Ben Saanane alishakanusha huo usaliti kule FB...
Aisee, ngoja tuone.
Nilikuwa namtahadhrisha Pasco. By the way, Weka akiba ya maneno.
Sitashangaa!!!!!!
Wekeni akiba ya maneno.
Mnayajua ya Ben?
Asipoenda ACT,nyie mliomtukana na kumbeza mtafanyaje?
Ben ni mtu makini nalisema hili baada ya kutafakari kwa kina, na katu awezi kukiama chama makini kama CHADEMA.
Rumours kama hizi whether true or not zinasaidia mlengwa kujitathmini mwenyewe (his strengths and weaknesses) na kutathmini nafasi na mchango wake ndani ya chadema. How does chadema fans/jf public perceives him. Namshauri Ben Saanane atulie watu wajimwage.
Acheni kupiga ramli chonganishi, nani kakuambia ana hamia ACT
Mpaka sasa Ben Saanane hajatokeza kwenye uzi huu? Hivi kweli ameamua kuharibu CV yake? ...
Naamini Ben Saanane anaupeo mkubwa zaidi ya Zitto, ni Mwanaharakati na Mwanamapinduzi zaidi ya Zitto, ni kiongozi zaidi ya Zitto. siamini kama ataweza kujiunga na ACT na kuwa chini ya Zitto.
You have talked my thoughts! Ben Saanane namkubali sana, akiondoka CHADEMA itakuwa ni huzuni sana kwangu pia even though mi pia ni vigumu sana kuhama hiki chama, nina miaka 6 tangu nimejiunga CHADEMA na sijaona ubaya wa hiki chama bali ni chama sahihi kwa mwanamageuzi yeyote yule hata kama zipo challenges za ndani kwa ndani lakini haziwezi kuondoa uhalisia kuwa CHADEMA ndio chama cha ukombozi nchini, vijana wa bodaboda, mama ntilie, wakulima, wafanyakazi, wanafunzi na kila aina ya watu matumaini yao yote ni CHADEMA hivyo hatuwezi kusaliti fikra za wanyonge hawa kwa kuiacha CHADEMA.
Sitakuwa wa mwisho kuondoka CHADEMA bali nitaipigana na kuilinda CHADEMA hata kama all the commanders will left the party, sababu naamini CHADEMA ni Tanzania, huwezi kuipenda na kuilinda Tanzania bila kwanza kuipenda na kuilinda CHADEMA.
CHADEMA AND TANZANIA ARE INSEPARABLE
labda kama anataka kumaliza deal lake la kumpa sumu ZZK ,maana nasikia dogo huwa anatembea na sumu mfukoni
Kwani Ben shida yake ubunge? Na kama ubunge tunachukua inchi october, si atapewa viti vya Rais viko 10 anaogopa nini? Eti mimo kwetu Iringa, kwahiyo nitake ubunge Ismani ambako najua Dada Mh Chiku anautaka na yeye ana privalage kubwa kuliko mimi, ndio nihame chama? Basi kuna lingine lakini kama nimapenzi ya Mungu yatakuwa, ila kama nishetani asithubutu.
I see! kumbe tusio na vyama hatujui siasa? sasa ni kwa nini mnataka tuwapigie kura vyama vyenu?
Naamini Ben Saanane anaupeo mkubwa zaidi ya Zitto, ni Mwanaharakati na Mwanamapinduzi zaidi ya Zitto, ni kiongozi zaidi ya Zitto. siamini kama ataweza kujiunga na ACT na kuwa chini ya Zitto.
Mkuu tuko pamoja sana....Kwangu mimi CHADEMA ni zaidi ya Mpenzi wangu...Naipenda sana....Na ninahuzunika sana pale mabaya yanapoikuta CHADEMA.Ninafurahi sana pale ninapoona chama changu kinazidi kupata mafanikio.
Nitakipigania chama hiki kwa moyo wangu wote na nguvu zangu zote...Nitajitoa kwa hali na Mali...Mungu anisaidie
Nimejiunga na CHADEMA mwaka 2004.....Nikiwa bado mdogo tu....Nimekuwa muumini wa chama...Chama ni kama pumzi yangu...
Hata waondoke watu wote...I will be the Last Man standing.
Kwangu mimi CHADEMA ni nchi yangu.....Nikihitajika kutoa damu yangu kwa ajili yake nitafanya hivyo.
Nitaungana na makamanda wenzangu kuhakikisha nia ya pamoja ya chama inafikiwa....
Hata kama itatokea leo kuna changamoto za ndani....hiyo ni nafasi ya kuimarisha chama changu....
Kamwe sitakimbia matatizo yoyote yale ndani ya chama changu bali nitakabiliana nayo.....MUNGU ANISAIDIE
Jamani kulikoni uzi umefikia mpaka ukurasa wa 16 bado Ben hajajitokeza tu kuthibitisha au kukanusha? Hapa anaongelewa Ben yule yule anayefahamika hapa Jukwaani au mwingine? Au ndo namna kupima upepo unakoelekea?
Acha kujikana we pro-chadema. Nani asiyekujua hapa na kelele zako za ki-bavicha? Au unakikana chama lako chadema baada ya kuona limeanza kufulia?
akili ndogo kama Sugu,lema, msigwa eti ni wabunge lakini ben mnambania ubunge rombo kisa uchaguzi wa Bavicha, ben ondoka huko chadema ni wanafiki
Jamani kulikoni uzi umefikia mpaka ukurasa wa 16 bado Ben hajajitokeza tu kuthibitisha au kukanusha? Hapa anaongelewa Ben yule yule anayefahamika hapa Jukwaani au mwingine? Au ndo namna kupima upepo unakoelekea?