Ben Saanane kuhamia ACT - Wazalendo siku ya Ijumaa

Ben Saanane kuhamia ACT - Wazalendo siku ya Ijumaa

Status
Not open for further replies.
''Nitawaomba mniunge mkono katika maamuzi MAGUMU, ni MAKINI na SAHIHI''

Well, umakini na usahihi wa maamuzi upo kwenye ubongo wa kila anayemua kufanya maamuzi hayo. Tumtakie kila la kheri tu katika safari yake. Labda ameskuti na kuona career yake kisiasa ndani ya CHADEMA haitofika mbali.
 
Uzuri wa Zitto tofauti na viongozi wengine wa Chadema hana visasi, na haogopi kuwa na watu wenye uwezo na anawatia moyo waperform zaidi.

Kama ataenda huko, tegemea Zitto kumuunga mkono kwa moyo mweupe, kama anavyosema YA NYUMA TAMEPITA, TUSONGE MBELE.
mkuu inawezekana akafanya udukuzi na kuupeleka cdm. Binafsi simkubali zitto kwenye harakati zake kisiasa. Lakini kama binadamu bado nampenda saana tu. Ni vizur akawa makini na huyu kijana.
 
Unakumbuka sakata la watu kutaka kulishana sumu kule CHADEMA miaka hiyo.
 
Ishu hii inaweza kuwa kweli ama isiwe kweli ila kwangu mimi sijawahi kumuamini Ben Saanane.
Ishu yake na Zitto inawezekana ni movie iliyopangwa kitaalam ili chadema wavurugane na hatimaye waanzishe ACT.
Anaonekana ni mwenye akili lakini ametawaliwa na ulafi wa madaraka,kwa hili sioni tofauti yake na Zitto.
Kama anaenda huko ninamtakia kila la heri maana atakuwa amekidhi haja ya moyo wake japo kisiasa chadema haitapoteza chochote na pengine atakuwa ameondosha siasa za makundi ndani ya ubunge jimbo la Rombo.
 
Ben Saanane ni kijana mwerevu, ana haki zake kama Mtanzania mwingine kujiunga na chama chochote cha siasa kwa utashi wake. Naamini kama amekubaliana na mission pamoja na vission ya ACT ya uwazi, uwajibikaji, uzalendo na kutumia rasilimali za taifa kwa manufaa ya taifa zima, basi si ajabu akajiunga ACT

Siasa ni safari, Dr Slaa alikuwa CCM sasa yuko CHADEMA

Lissu alikuwa NCCR sasa yuko CHADEMA
Lema alikuwa TLP sasa yupo CHADEMA
Zitto alikuwa CHADEMA, sasa yupo ACT

Kwa hiyo si ajabu kwa Ben Saanane kuhamia chama chenye dira na muelekeo cha ACT
Mbona humtolei mfano stephen wasira alihama wapi na wapi na kuhamia wapi!,inaonekana mrengo wako na saatisa hauna tofauti
 
Leo ndo mnamuona kamanda baada ya kutangaza nia ya kuondoka,mlimuona takataka na kumfanyie visa kibao,nyie wachaga msipoangalia na Saccos yenu atabakia King Mbowe na Mkwe wake Mtei
We mbulula umejaa ukabila mwili mzima tena ujinga useekuwa hata na elimu ya uraia poyoyo wewe
 
Hadi Wakati huu bado nafurahia utulivu wa Ben Saanane naona watu wameporomosha yao ya moyoni na jamaa katulia tu. Hayo masaa aliyoyasema yakifika na atakachokitolea hayo maamuzi mazito yatawaacha wazi wengi hapa, hasa ambao hawakuweka akiba ya maneno.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna Mwanasiasa Tanzania hii aliyekuwa Rais mwenye CV kama ya Kikwete. Hiyo ndiyo tofauti kati yake na makanjanja wa kabla yake.

Hivi vikanjanja vya JF unavipa hadhi hata ya kuvifananisha na Kikwete? ni kama kufananisha tone la maji na bahari.
haa haa haya yanaitwa mahaba niueg
 
Hadi Wakati huu bado nafurahia utulivu wa Ben Saanane naona watu wameporomosha yao ya moyoni na jamaa katulia tu. Hayo masaa aliyoyasema yakifika na atakachokitolea hayo maamuzi mazito yatawaacha wazi wengi hapa, hasa ambao hawakuweka akiba ya maneno.

Endelea kupambana na hisia za wasaliti awana jipya maamzi yao yanajulikana
 
Last edited by a moderator:
Umofia wana JF,

Habari nilizoponyezewa na rafiki wa karibu na Ben Saanane,ameniambia jamaa anataka kuamia ACT kwa sababu ameona kuna kila dalili ya kunyimwa jimbo la Rombo.
Kuanzia Leo nimezidisha imani yangu kwa Chadema wako makini sana. Huyu jamaa yuko kwenye hile list walio kuwa wanatumiwa 200,000 wakati Zitto anavuta 400m. Alitaka kujipenyeza Bavicha watu wakashutuka. Kweli Chadema wako makini wapewe nchi.
 
Namshauri aende ACT Tanzania kwa sababu ACT Wazalendo kumeshawaka moto, hakutoshi, Ayatollah kachafua hali ya hewa.
 
pamoja na madhaifu ya Ben lakini ana akili kuliko Bavicha wote na hili nalisema wazi.Ben ni mtu ambaye mnaweza mkajadili nae jambo bila kuweka matusi na mihemko tofauti na Bavicha wengine kama CHADEMA KWANZA Mungi na Crashwise.

Ben hata asipohama Chadema lakini hampamfai pale pana wafaa wale wa matusi na wa ndio mzee,Ben anawazidi akili Bavicha wengi hawawezi kumpa nafasi.....
 
Last edited by a moderator:
Umofia wana JF,

Habari nilizoponyezewa na rafiki wa karibu na Ben Saanane,ameniambia jamaa anataka kuamia ACT kwa sababu ameona kuna kila dalili ya kunyimwa jimbo la Rombo.

Hivi hiki chama cha Sweet/ACT ni chama Social Media?
Watz kwa sasa hatutaki too much Bla! Bla! au siasa za maji taka au kujenga chama, TUNATAKA MABADILIKO OCTOBER 2015 NA HATA SIYO KUWA CHAMA KIKUU PINZANI.

Hebu vijana tuje na mawazo chanya sasa na kuacha kutumika na wasaka Tonge au Ruzuku.
 
Nina ujumbe mmoja tu kwa vijana wote bila kujari chama chako, Siasa za Facebook zinawaharibu sana mpaka wanadhani kura zinapigwa na followers wa Facebook.

Lowasa ana wafuasi wengi na anajurikana na wananchi lakini anaitegemea Ccm ndio impe Urais, kama vijana mna akili jiulizeni kwa makini ni kwa nini pamoja na mizengwe yote Lowasa ahami Ccm?

Ally Choki ni mwanamuzi bora kabisa lakini nje ya Twanga pepeta hana lolote, mwenye akili timamu atakuwa amenielewa.

Cc; Pasco
umesema ukweli mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom