Ben Saanane kuhamia ACT - Wazalendo siku ya Ijumaa

Ben Saanane kuhamia ACT - Wazalendo siku ya Ijumaa

Status
Not open for further replies.
Ben ana haki ya maamuzi yake...Lakini ni mtu ninayemkubali sana CHADEMA.

Huenda akiangalia mbele haoni mwanya wa kupenya kwenye jimbo la Rombo.

Lakini Ben ni mtu ambaye nilikua naona kuwa ni muumini wa sera na itikadi za Chama

Kama itatokea huyu kamanda akahama Chama nitaumia sana

Ila naipenda sana CHADEMA...Nitakuwa wa mwisho tena wa mwisho kabisa kwenye chama hiki......

Haijalishi niwe na madaraka au nisiwe na madaraka
 
Hii habari kama ni ya kweli itakuwa imemshushia sana hadhi Ben Saanane kwa kuungana na chama wakala na mshirika wa ccm katika kuua upinzani wa kweli. Atakuwa ameamua kuifanya kazi ya kuzuia mabadiliko na uchumi bora kwa watanzania maskini.

Hii naomba iendelee tu kubaki tetesi na isiwe kweli maana ikiwa kweli itakuwa zzk anaendelea kuangamiza vipaji vya vijana kwenye siasa. Alianza na Mwampamba, Shonza, Change etc.

Ben anatangaza rasm kugombea Ubunge jimbo la Rombo.
 
Acheni kupiga ramli chonganishi, nani kakuambia ana hamia ACT
 
Kwa mtu makini sana anayeijuwa vyema Chadema basi ni rahisi kuelewa Chadema inaingiza Mamluki ACT kipindi hiki ili kumsambaratisha kabisa Zitto Kabwe.

Inahitaji akili pana sana kuliewa hili na sijajuwa bado Chadema iliwezaje kujipenyeza mpaka idara yetu ya usalama wa Taifa na ina informers wake idarani.

Maisha ya Zitto kisiasa siku zake zinahesabika, kuna mkakati mzito ambao kwa akili ndogo za Zitto kamwe hawezi kuushtukia.

Dunia nzima ukishatumika kwenye mission za kijasusi kinachofuata wanakueliminate.
hayo ni maneno mazito sana mkuu, kama ndio hivyo basi chadema ni hatari. na hao majasusi kutoka idarani ndio watakua wamemwambia Dr. Kua kuna bomba la gesi limetandazwa tokea mtwara mpaka ulaya chini ya bahari. chadema inatisha sana kwa ujasusi, ishue ya kagenzi pia sio ndogo ujue. wapo vizuri.
 
Wacha porojo wewe.

Barabara za lami zaidi ya wote wa kabla yake, tena wachanganye pamoja.

Kila ukijibu ntakupa kimoja, mpaka utie akili.

Just a challenge; tarmac roads is a result of foreign debts which could b done by anyone. Hapo vipi
 
Nina ujumbe mmoja tu kwa vijana wote bila kujari chama chako, Siasa za Facebook zinawaharibu sana mpaka wanadhani kura zinapigwa na followers wa Facebook.

Lowasa ana wafuasi wengi na anajurikana na wananchi lakini anaitegemea Ccm ndio impe Urais, kama vijana mna akili jiulizeni kwa makini ni kwa nini pamoja na mizengwe yote Lowasa ahami Ccm?

Ally Choki ni mwanamuzi bora kabisa lakini nje ya Twanga pepeta hana lolote, mwenye akili timamu atakuwa amenielewa.

Cc; Pasco
Mawe mazito haya aisee, nilichoelewa hapa uongozi ni kama taasisi flani hivi lazima kuwe kuna chombo kinachokupa mwongozo wa nini cha kufanya zaidi ya wewe kama individual
 
Ninachojifunza hapa ni kwamba ukijiunga na chadema au ukiwa mwanachama tu utapewa sifa nyingi hata ambazo hustahili. Lakini ukitoka tu sifa zote mbaya, matusi, kejeli na zingine zinazofanana na hizo utabebeshwa. Mifano ni mingi tuliona kwenye nyuzi zinazomhusu Mdee na leo Ben saanane.

Just imagine hizi taarifa hata hazijathibitika lakini watu washamgeuka kijana huyu. Kiukweli chadema mnatoa taswira mbaya kwa jamii siasa si ugomvi wala matusi
 
ukweli ni kwamba kama ben anaenda ACT basi Zitto awe makani sana na huyu jamaa. maana ile kazi aliyotumwa na slaa hakuikamilisha. tafadhalini kama kuna yeyote kati yenu anayefahamiana na zitto amu-alert mapema.



anasimu nne + power bank tano, lazima atajazia mikono.

wanajifunza ukachero uharo

Hapo inaonekana analazimisha ubunge.

Hivi huyu jamaa yupo kweli,baada ya kupigwa chini kwenye Bavicha sijamwona kabisaa

Yaaaa..........umuofia kwako.......tunaomba ututajie msiri wako mkuu aliyekupenyezea. Najua hawezi kwenda ACT kwa sababu alibumbulua mipango ya zitto....enzi zile wakati wanatumiwa hela.

kwa kuwa ni uvumi unao "ifeva" ACT,utachwa tu na moderators.ila ungekuwa kinyume chake,ungefutwa haraka sana.mtizamo wangu tu.

Ben Saanane ni kijana mwerevu, ana haki zake kama Mtanzania mwingine kujiunga na chama chochote cha siasa kwa utashi wake. Naamini kama amekubaliana na mission pamoja na vission ya ACT ya uwazi, uwajibikaji, uzalendo na kutumia rasilimali za taifa kwa manufaa ya taifa zima, basi si ajabu akajiunga ACT

Siasa ni safari, Dr Slaa alikuwa CCM sasa yuko CHADEMA

Lissu alikuwa NCCR sasa yuko CHADEMA
Lema alikuwa TLP sasa yupo CHADEMA
Zitto alikuwa CHADEMA, sasa yupo ACT

Kwa hiyo si ajabu kwa Ben Saanane kuhamia chama chenye dira na muelekeo cha ACT

Sema machache. Wanaojua Siasa hawaweki visasi. Wenye uwezo na mbinu wanajuana!

Hapo sasa umenena. Zitto anatakiwa kuwa makini na hawa anaohama nao. Wengine wanaenda ACT kwa kazi maalum

kwa jinsi walivyombania uenyekiti wa Taifa bavicha na watu ambao alikua anawategemea sana(mbowe na slaa) ,ukiongeza na umakini wa Ben Saanane lazima atajiuliza mara mbili kubakia chdema chama ambacho hata demokrasia yake ya ndani kimefeli
 
Lisemwalo lipo, Ben Saanane kuja huku!
Si msubiri siku ifike ndio mtajua yote. Mbona wabongo wambea sana siku hizi? Na hata kama akihama kuna ajabu gani? Kuhama vyama ni desturi ya watanzania. Utakuta jamaa anataka kuongelea mambo mengine kabisa na nyie mnarukia megine.
 
Wacha porojo wewe.

Barabara za lami zaidi ya wote wa kabla yake, tena wachanganye pamoja.

Kila ukijibu ntakupa kimoja, mpaka utie akili.

jifunze kutambua net development na si gross wewe dada yangu. Angalia na madeni basi na resources alizovuna

Kwa mfano madini, tembo, mazao ya msituni n.k.
 
Mawe mazito haya aisee, nilichoelewa hapa uongozi ni kama taasisi flani hivi lazima kuwe kuna chombo kinachokupa mwongozo wa nini cha kufanya zaidi ya wewe kama individual

Exactly, Simba na Yanga hata umlete Fugerson au Morinyo kuwa kocha hamna kitu watakachofanikiwa.

Uzuri Lowasa ni mtu mzima anazijuwa vyema hesabu za kisiasa na hafanyi makosa.

Kinachoniuma Zitto anaharibu future ya vijana wengi wafuata mkumbo wakati yeye kwenye siasa akibuma ana uwezo wa kufanyakazi za kitalaam kwa malipo makubwa ila vijana wasiojitambuwa watafirika mjini.

Angalia umri wa wanakwenda ACT utapata jibu wala huitaji degree kujuwa baada ya uchaguzi mkuu kutakuwa vilio na kusaga meno, siasa za kwenye mitandao zinawaharibu sana vijana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom