Ben Saanane kuhamia ACT - Wazalendo siku ya Ijumaa

Ben Saanane kuhamia ACT - Wazalendo siku ya Ijumaa

Status
Not open for further replies.
Acheni story za kikuda na kumlisha mtu maneno,Kamanda Ben Saanane alishakanusha huo usaliti kule FB...

Leo ndo mnamuona kamanda baada ya kutangaza nia ya kuondoka,mlimuona takataka na kumfanyie visa kibao,nyie wachaga msipoangalia na Saccos yenu atabakia King Mbowe na Mkwe wake Mtei
 
Last edited by a moderator:
Weka CV zao na ya Kikwete ujionee tofauti.

Yule hajawa Rais kwa kukisia, kama unabisha muulize Askofu Kilaini, alitangaza kuwa yule ni chaguo la Mungu, hapo sasa.
kumbe wewe dada akili ndogo kiasi hicho, tunapozungumzia cv ya mtu tunaanzia kwenye elimu yake, uzoefu wa kufanya kazi mbalimbali, kikwete ndiyo alifanya kazi wizara mbalimbali, umewahi jiuliza makubwa aliyoyafanya huko kwenye hizo wizara ? ukimlinganisha yeye na mwl. au Mkapa wamefanya mambo makubwa sana , yeye alinganishwe na mwinyi wala sio hao wawili wanamtupa mbali nisawa na kulinganisha motto wa chekechea na yule wa chuo kikuu
 
Sina hakika kama habari hizo zina ukweli, wacha niwe tomasso katika Hilo. Ninachofahamu Ni kwamba Ben anakubalika kwa viongozi WA chadema jimbo la Rombo, mkutano mkuu WA wilaya Ben Ana kura za kufa mtu. Nategemea Ben kutangaza Nia, ila kama anaenda huko wacha tusubiri. Changamoto kwa Ben Ni moja Tu, ambayo Ni kutofahamika kwa wananchi. Anaweza kumaliza Hilo tatizo kwa kushirikiana na viongozi WA chama

Mkuu una busara na hekima, nakupa Heko.
 
Umofia wana JF,

Habari nilizoponyezewa na rafiki wa karibu na Ben Saanane,ameniambia jamaa anataka kuamia ACT kwa sababu ameona kuna kila dalili ya kunyimwa jimbo la Rombo.

Mkuu King Kong III nakushauri uwaambie hao jamaa zako ambao ni marafiki wa karibu wa Ben Saanane wamtahadharishe kuwa hata kama anatamani kiasi gani kuwania nafasi ya kugombea Ubunge Rombo na ana mashaka kwamba hatapitishwa na Chadema afute wazo la kuhamia ACT kipindi hiki kwa matamanio hayo! ACT bado ina "Player" mmoja tu mwenye mamlaka na maamuzi yote i.e Zito! Kwa yaliyojitokeza wakati wa sakata lake na wenzake kina Juliana Shonza, na tuhuma dhidi yake za kukusudia kumdhuru Zito kwa sumu, itakuwa vigumu sana kwake kuaminiwa 100%! Pengine kibinadamu alishapatana binafsi na Zito, lakini kusameheana hakufuti kutiliana mashaka! Kwa kifupi sio wakati mwafaka kwake kujiunga ACT!!! Atafakari upya!
 
Mkuu King Kong, April Fools si iliishapita?, hivi inaruhusiwa kuiendeleza hadi leo?!. Kusema ukweli kuna type fulani ya uongo ukiutunga, hata msomaji anaweza kuelewa kabisa, kuwa mwandishi sio timamu!, niliwahi kusema mara nyingi humu, mtu kuwa kichaa, sio lazima hadi aokote makopo!.

Mode, vitu kama hivi kuendelea kuachwa ndivyo vinavyoshusha hadhi ya jf!.
Ben Saanane
ni memba humu, his ability, capability na misimamo yake inafahamika humu!!.

Pasco
Mkuu Pasco, Tatizo la Watanzania nikulazimisha hisia zao kuwa Uhalisia,Ukimsoma Ben saanane hapo Juu ni kuwa hajatamka kuhama Chama,Alichosema nikufanya uamuzi tu.

Huu ni Mwaka wa Uchaguzi yeye kama Mtanzania anayohaki yakugombea popote huenda anatangaza Nia.
 
Last edited by a moderator:

Nawewe je tukuite mbea!!?? maana Ben hajatamka analokusudia wewe na mbea mwenzio King kong
mmejuaje kuwa ni kuhamia ACT, mnajuaje labda anatangaza nia ya kuoa!!!
Nilikuwa namtahadhrisha Pasco. By the way, Weka akiba ya maneno.
 
Mkuu King Kong III nakushauri uwaambie hao jamaa zako ambao ni marafiki wa karibu wa Ben Saanane wamtahadharishe kuwa hata kama anatamani kiasi gani kuwania nafasi ya kugombea Ubunge Rombo na ana mashaka kwamba hatapitishwa na Chadema afute wazo la kuhamia ACT kipindi hiki kwa matamanio hayo! ACT bado ina "Player" mmoja tu mwenye mamlaka na maamuzi yote i.e Zito! Kwa yaliyojitokeza wakati wa sakata lake na wenzake kina Juliana Shonza, na tuhuma zake za kukusudia kumdhuru Zito, itakuwa vigumu sana kuaminiwa 100%! Pengine kibinadamu alishapatana binafsi na Zito, lakini kusameheana hakufuti kutiliana mashaka! Kwa kifupi sio wakati mwafaka kwake kujiunga ACT!!! Atafakari upya!

Hakuna cha kutafakari mahali sahihi kwa ben ni ACT pekee,huko chadema walimuona mavi,wakamnyanyasa sana leo vipi wanalialia eti kamanda,chadema waache unafiki na kwa style hii wataondoka wengi sana
 
Umofia wana JF,

Habari nilizoponyezewa na rafiki wa karibu na Ben Saanane,ameniambia jamaa anataka kuamia ACT kwa sababu ameona kuna kila dalili ya kunyimwa jimbo la Rombo.
Katika ujumbe wake sijaona akisema anataka kuhamia ACT
 
Ben unatoa taarifa ukiwa kama nani kwamfano go go goooooooo no one cares.
 
Mzalendo KALINZI NYUMBANI huo ndio ukweli whether you take or leave it, ACT si chama sahihi kwa mwanasiasa yeyote anayejitambua, chama chenu hakina direction ya kiitikadi, kifalsa hata kimsimamo pia, haieleweki kinapigania nini na wapi, viongozi wake wana uelewa mdogo sana wenye siasa za chuki na visasi wengi wao nawafahamu fika na baadhi yao nimewahi kuishi nao mbali tu na maisha ya kisiasa bali hata maisha ya kawaida,
Hebu angalia watu kama Msafiri Mtemelwa, Kansa Mbarouk na Shaban Mambo kweli hawa ni viongozi au utani? Sifa kuu ya hawa jamaa ni ubishi tu, tatizo wao wanadhani ubishi ni upinzani Hapana, upinzani ni hoja kinzani. Nawapa pole vijana wote walioweka matumaini kwa chama cha ACT walahi ipo siku watarudi huku wakijutia maamuzi yao. PERIOD

Mkuu una uwezo mkubwa sana, chukuwa kama ilivyo. mkuu hoja yako naiunga mkono, Binafsi namjuwa sana Habibu Mchange, uwezo wake ni Mdogo sana sana. alafu ndani ya ACT ni kiongozi! na aliutaka Uenyekiti.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu King Kong III nakushauri uwaambie hao jamaa zako ambao ni marafiki wa karibu wa Ben Saanane wamtahadharishe kuwa hata kama anatamani kiasi gani kuwania nafasi ya kugombea Ubunge Rombo na ana mashaka kwamba hatapitishwa na Chadema afute wazo la kuhamia ACT kipindi hiki kwa matamanio hayo! ACT bado ina "Player" mmoja tu mwenye mamlaka na maamuzi yote i.e Zito! Kwa yaliyojitokeza wakati wa sakata lake na wenzake kina Juliana Shonza, na tuhuma dhidi yake za kukusudia kumdhuru Zito kwa sumu, itakuwa vigumu sana kwake kuaminiwa 100%! Pengine kibinadamu alishapatana binafsi na Zito, lakini kusameheana hakufuti kutiliana mashaka! Kwa kifupi sio wakati mwafaka kwake kujiunga ACT!!! Atafakari upya!
Sidhani kama Ben saanane anaweza kuhama Chama kwa Aina yake ya Msimamo imara wa kiitkadi.

Na ikitokea akahama itakuwa ni moja kati ya Makosa Makubwa kisiasa huko Mbeleni.
 
Last edited by a moderator:
Hapo inaonekana analazimisha ubunge.

Kama ubunge sio mtamu mwambie mbowe, au lema au mnyika asigombee...

Na kama pia chadema hawapendi madaraka mwambie mbowe aachie uenyekiti kama hawajaku zitto kabwe au kukuchacha wangwe
 
31/03/2014 Ben Saanane aliwahi kukanusha taarifa zilizoandikwa kule MF kuwa anampango wa kutimkia ACT.Ngoja tusubiri tuone tena.
 
Umofia wana JF,

Habari nilizoponyezewa na rafiki wa karibu na Ben Saanane,ameniambia jamaa anataka kuamia ACT kwa sababu ameona kuna kila dalili ya kunyimwa jimbo la Rombo.

Kwani yerico nyerere yeye bado hajatangaza nia ya kwenda act maana hawa wote zito ndo aliyewapeleka cdm
 
Ben Saanane ni kijana mwerevu, ana haki zake kama Mtanzania mwingine kujiunga na chama chochote cha siasa kwa utashi wake. Naamini kama amekubaliana na mission pamoja na vission ya ACT ya uwazi, uwajibikaji, uzalendo na kutumia rasilimali za taifa kwa manufaa ya taifa zima, basi si ajabu akajiunga ACT

Siasa ni safari, Dr Slaa alikuwa CCM sasa yuko CHADEMA

Lissu alikuwa NCCR sasa yuko CHADEMA
Lema alikuwa TLP sasa yupo CHADEMA
Zitto alikuwa CHADEMA, sasa yupo ACT

Kwa hiyo si ajabu kwa Ben Saanane kuhamia chama chenye dira na muelekeo cha ACT
Hata akina Nape, Sitta na Mwakyembe walianzisha CCJ. Maalimu Seif alikuwa CCM sasa CUF, JK naye ilikuwa ajiunge na CHADEMA kama angenyimwa kugombea urais 2005 Yeyote anaweza kuhama na kujiunga na chama kingine wakati wowote anaotaka au kuanzisha chama kama walivyofanya akina Zitto na timu yake. La msingi ni kuwa katika siasa hakuna urafiki wa kudumu wala uadui wa kudumu. Ukiona wanasiasa marafiki leo usishangae kesho wakawa maadui na wale waliokuwa maadui wakawa marafiki. Mifano iko mingi! Wassira alitoka CCM akajiunga na NCCR akawa anasema CCM ina ukimwi. Baadaye alirudi CCM chama chenye Ukimwi kama alivyosema. Mrema alitoka CCM akaenda NCCR kisha TLP na kote huko alionekana mpinzani lakini sasa amerudi CCM ingawa bado kavaa shati la TLP Na hivi tunavyoelekea uchaguzi mkuu kutakuwa na uhamaji na uhamiaji mkubwa wa wanasiasa baina ya CCM, CHADEMA, CUF, ACT - Tanzania/Wazalendo, TLP nk. Subiri kimbunga cha uteuzi wa wagombea urais ndipo utaona watu watakapo ondoka na makundi yao. Tatizo mimi naliona ni kwa wanasiasa uchwala ambao huwa wanafuata mkumbo au kufuata watu badala ya sera za chama. Sasa hivi watu wanajiunga ACT kwa kumfuata Zitto siyo chama. Huo ndio ujinga mkubwa!
 
Naamini kwa akili alizo nazo kama ninavyomsoma huku mtandaoni, anafaa kuanzisha chama chake badala ya kumfuata ZZK. Asisubiri kwenda kugombea ubunge huko Rombo. Watu siku hizi ni wa karne nyingine siyo wa ile karne ya TANU.
 
Ben mchumia tumbo hana lolote acha aende kwa wanafiki wenzake waliopanga Mapinduzi bila mafanikio sasa wakajipindue
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom