BBA 2: Mtanzania ashinda!

mzee FMES.. you are not implying kwamba ushindi wa Richie ni ushindi wa serikali ya Rais Kikwete na CCM? Now that is daring!!
 


Mkuu Brazameni,

Heshima mbele, kwenye maisha kuna wakati wa kila kitu kuanzia kucheka mpaka kulia, kuruka na kushuka chini, kwenye hili la Richie na ushindi, sasa ni wakati wa kushangilia na kusherehekea ushindi wake kwanza, then mengine kama yapo yatakuja baadaye,

Lakini sasa ni saaa ya kushangilia ushindi wake ambao ni wa taifa mkuu, siasa na forum baadaye.

Hongera Richie na wa-Tanzania wote kwa ushindi mnono!
 
Hongera Mheshimiwa Rich kwa kulitangaza jina Tanzania Vyema!!,Tutakusubiri ATL ili tuje kukupongeza zaidi.Hongera sana kwa kulitangaza jina Tanzania.Mchango wako huo ni Mkubwa na unakubalika na kila Mtanzania..

Can read this down:

RICHARD WINS!


That's Richard - 24yrs

Tatiana - 26yrs

Ofuneka - 29yrs
 
jamani salama hajakosea ..ametumia uhuru wake ..hamjaona kule angola kwa tatiana wawili wameongea kumsapoti rich..na kule nigeria pia wawili wakahojiwa wakamkubali rich...kenya na uganda waliomkubali rich ni kama wawili wengi wakimkubali tatiana...let speak our hearts open..na wala sio haki kumnyanyapaa salama kwa kuongea feelings zake...kama rich angepigiwa kura na wa tz pekee asingeshinda...so tusiwalaumu wa tz ambao hawakumpa kura...
 
Yaaani pole pole tu chini ya uongozi wa Muungwana, na CCM tunajikongoja, japo matatizo yapo pia lakini Mungu anatunusuru na tunaweza kuwika mbele ya Dunia,

hongera mkuu Richie, maana huu ushindi ni wa bongo nzima.

Duh, ama kweli Muungwana mwaka huu atasifiwa kwa mengi! Hata hili nalo kumbe inabidi credit yeye, haya bwana!

Hongera sana bwana Richard. Acha wenye roho za korosho hao wa west africa, lakini ndiyo hivyo tena wewe beba hizo $100,000 msebemsebe!
 

PM,

The way alivyokuwa akiongea Salama kama ulimsoma vema ni kuwa aliongea si kama kwa kutoa maoni yake tu bali kuonesha machungu yake kuikosa nafasi ile. Of-course mi nilikuwa namuunga mkono sana Salama na nilidhania angeenda huenda tungepata burudani ya kipekee. Nigeria wale waliompendekeza Richard hawakutoa mabaya ya Ofuneka, wameonesha kwanini wanapenda Richard ashinde.
 

I agree with you. Asionekane msaliti. Hiyo hasa ndiyo falsafa ya uhuru wa mawazo, tutoke kwenye ukomunisti ambapo mtu hawezi kufikiria yeye mwenyewe ila kufuata wengine wanasemaje.
 
I agree with you. Asionekane msaliti. Hiyo hasa ndiyo falsafa ya uhuru wa mawazo, tutoke kwenye ukomunisti ambapo mtu hawezi kufikiria yeye mwenyewe ila kufuata wengine wanasemaje.

Mkuu Kitila,

hapa hakuna anayebisha kuwa mtu asitoe maoni yake...hoja ni kuwa hata kama unatoa maoni, basi inategemewa utakuwa na busara za kujua athari za yale maoni yako....wakati huo huo, hapa pia tunatia maoni yetu kuwa Salama alivomponda sivyo na ushahidi ndo huo jamaa kashinda...ni uhuru pia sio?
 
Mkuu,
Salama anaponda tu mara nyingi hatumii busara kwa kile anachopondea.nakumbuka kwenye Bongo Star search alikuwa anaponda sana basi tu bila sababu za msingi.
 
I agree with you. Asionekane msaliti. Hiyo hasa ndiyo falsafa ya uhuru wa mawazo, tutoke kwenye ukomunisti ambapo mtu hawezi kufikiria yeye mwenyewe ila kufuata wengine wanasemaje.

Salama Jabir ni mmoja wa mabinti wanaojiamini na binafsi nilikuwa nampa credit kuwa angeenda huko angeleta changamoto kubwa sana. Bahati mbaya alikosa. Huyu Richie wala sikutarajia afikie kwenye 5 Bora. Mambo yamekuwa ndivyo sivyo.

Anyway, ni uhuru wa mtu kujieleza, ila kwakuwa walikuwa washindani pamoja angetumia trick ya namna ya kuponda si moja kwa moja. Ukisoma hapa utaona watu wanavyomchukulia Salama
 
Nampongeza Richard kwa ushindi kwani hicho kitita si haba kama atakuwa mwenye busara kitabadili maisha yake sana.

Upande mwingine nampongeza kwa kuitangaza Tanzania

Nawapongeza watanzania wote kwa moyo wa upendo wa kumpa shavu kwa kumpigia kura Rich hadi akaibuka kidedea.

ila sikubaliani na sipendezewi na yafuatayo:

-Michezo ile inayo endelea ndani ya jumba lile kuanikwa wazi wazi mbele ya jamii wa rika tofauti! mfano sikupendezewa zile picha walivo anikwa uchi uchi

-Sipendi tabia ya watu kumsifia JK/CCM hata wasipo husika sasa kwa hili la big Brother na mafanikio ya JK/CCM wapi na wapi?
 
ila sikubaliani na sipendezewi na yafuatayo:

-Michezo ile inayo endelea ndani ya jumba lile kuanikwa wazi wazi mbele ya jamii wa rika tofauti! mfano sikupendezewa zile picha walivo anikwa uchi uchi

Kaka/Dada Rwabugiri,

Richard hakuwa na option inapofikia suala la kuoga. Camera zilikuwa kila sehemu. Alitakiwa aishi maisha ya YEYE kama YEYE. Wa kulaumiwa hapo ni waandaaji kwa kuwaanika washiriki nyakati za kuoga. Kwa waliokuwa wanaangalia 24hrs wanaweza kukiri kuwa hata washiriki walikuwa hawapendezwi kuchukuliwa picha nyakati za kuoga ama kubadilisha mavazi.

Mchezo mgumu sana ule mkuu
 

Imvicible ,
Simlaumu Rich najua wanachukuliwa bila kupenda/kujua picha hizo! Ila ndo ukweli wangu kwamba hicho kitu sikipendi katika mchezo huu!!

Na pengine ndo maana huu mchezo haupendwi sana na watu wazima hasa wenye kujali makuzi ya vijana wao!

But well, kwa vile mtanzania mwenzetu kashinda walau kajikwamua na MKUKUBITA (Mkakati wa Kukuza Uchumi Binafsi Tanzania) Hatuna budi kujumuika naye kwa kumpongeza.
 
Hongera Richie,

Nafikiri imekuwa wakati muafaka wa kulinganmisha mafanikio wnaume walioiletea Tanzania ukilinganisha na wanawake.
Naomba mwenye kumbukumbu sahihi atusaidie, ila naamini wanaume wamewakilisha Taifa vizuri sana nje, ndio maana hata salama akashindwa.

Je kama Salama angeenda then akawa anafanyiwa na Mnigeria. na Leo akawa wapili au 3 ingekuwaje?
 
SINA HAKIKA, naomba kufahamishwa kwa kina;

1, NINI MAANA YA BIG BROTHER kwa manufaa ya MWAFRIKA/MTANZANIA?
2.. JE, MBALI YA KITITA CHA USHINDI, KUNA SIRI GANI KATIKA MCHEZO HUO, AMA KWA WAANDAAJI AU KWA WASHIRIKI?
3... JE, NI ISHARA GANI KUONA JINSI MCHEZO HUSIKA UNAVUTA HISIA ZA WATAZAMAJI WENGI, NI KITU GANI HASA KINAWAVUTA?
4.. HICHO KINACHOWAVUTIA WATAZAMAJI WENGI, HUWA KINAWAVUTA WATAZAMAJI MAENEO MENGINE AMA VIPINDI VINGINE?
5... JE, USHINDI WA RICH UTATUMIKAJE KATIKA KUITANGAZA TANZANIA HASA KATIKA UTALII?
6-- MWISHO, WANASIASA WETU WA AFRIKA NAAMINI SASA WATATAKA NAO KUMTUMIA RICH KUJITANGAZA BADALA YA KUTANGAZA UTALII..

TUSUBIRI TUONE JINSI AFRIKA KUSINI ITAKAVYOJITANGAZA KATIKA SOKO LA TANZANIA KWA KUMTUMIA RICH NA BIG BROTHERS

NAKUMBUKA MTU MMOJA ALINIAMBIA KWAMBA, BIG BROTHER NI MKAKATI WA AFRIKA KUSINI KUTANGAZA BIASHARA ZAO NA KWAMBA NCHI ZINAZOTOA WASHIRIKI NA HATA KUSHINDA NI SOKO KUU LA BIDHAA ZA AFRIKA KUSINI AMA ZA VIWANDANI AMA HUDUMA KAMA VILE TV NA BENKI ZAO NA KADHALIKA. TUJADILI NA KUTAFAKARI
 
Big brother ni ujinga mtupu. Nimeiona huku ulaya....underclass ndio mashabiki wakuu. Sasa pia kuna Idol. Sijui hii nayo imeshaingia Afrika?

Any way, hongera Richard kwa kupata dola laki nzima. Natumai zitasaidia kuboresha maisha yako.
 
Big brother ni ujinga mtupu. Nimeiona huku ulaya....underclass ndio mashabiki wakuu. Sasa pia kuna Idol. Sijui hii nayo imeshaingia Afrika?

Any way, hongera Richard kwa kupata dola laki nzima. Natumai zitasaidia kuboresha maisha yako.

Idol ipo Tanzania, lakini inaitwa 'Bongo Star Search', lakini maudhui ni yale yale, kusaka vipaji katika masuala ya muziki. Miaka michache iliyopita, wadhamini wa Big Brother Afrika walidhamini pia Tanzania Pop Idol, na mwanamuziki Banana Zorro alituwakilisha Watanzania kule Afrika Kusini ambako hakufanya vema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…