The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,064
- 14,079
Nimeipa heshima Tanzania - Richard
2007-11-13 09:33:15
By Fred Ogot, Johannesburg
Richard Bizubenhout ameeleza anafurahia kuipa heshima Tanzania katika medani ya kimataifa baada ya kuibuka kidedea kwenye shindano la televisheni la Big Brother Africa 2 lililomalizika hapa, juzi usiku.
Akizungumza na waandishi wa habari, Richard alisema ushindi huo haukuwa wake pekee bali sifa ilikuwa inapaswa kwenda kwa Watanzania wote.
Kwa ushindi huo aliweza kuondoka na kitita cha Dola 100,000 (zaidi ya Sh. milioni 100). Aliweza kuwapiku mshiriki kutoka Nigeria, Ofuneka na mrembo kutoka Angola, Tatiana waliofanikiwa kuingia fainali.
Ofuneka ndio alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda na kuambulia nafasi ya pili na Tatiana anayesadikika kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Richard, alikamata nafasi ya tatu.
``Kwa kweli ninajivunia sana ushindi na hasa Watanzania waliochangia kura za ushindi wangu,`` alisema Richard kwenye mkutano na waandishi.
Pia aliomba radhi kama kuna watu wowote aliowakosea katika kipindi chote alipokuwa akishiriki kwenye Big Brother.
Watu wengi walifika kwa ajili ya kumshangilia Richard, akiwamo Dada yake, Linda na Kaka Louis.
Alipoulizwa kuhusiana na uhusiano na mpenzi wake Tatiana alijibu; ``Ninampenda na nitamwoa ikiwa nitavunja ndoa na mke wangu. Ninasikia amerejea kwao Canada, sijui kitu gani kimetoa,`` alieleza.
Kuhusiana na milioni 120, alizopata alidai kuwa anajipanga kuanzisha kampuni ya kutengeneza filamu.
Alisema pia atatafuta watu wa kumshauri kuweza kutumia fedha hizo.
Washiriki wengine walikuwa Max (Zambia), Kwaku (Ghana), Jeff (Kenya), Justine (Botswana), Moureen (Uganda), Code (Malawi) na Bartha (Zimbabwe).
Wakati huo huo, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Richard kwa kufanikiwa kulivaa taji la Big Brother.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati ilisema kuwa ushindi huo ulitokana na malezi mazuri wanayopata vijana wa Kitanzania na hasa kwa kuzingatia sera nzuri za CCM.
SOURCE: Nipashe