BBA 2010: Big Brother Africa All Stars | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BBA 2010: Big Brother Africa All Stars

Discussion in 'Entertainment' started by Keil, Jul 16, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. K

  Keil JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  =============
  Housemates evicted so far:

  1. Hannington
  2. Sammi
  3. Lerato
  4. Tatiana
  5. Yakob
  6. Sheila
  7. Code
  8. Paloma
  9. Jen
  10. Meryl
  =============

  Jumapili ya 18/7/2010 ile show maarufu ya Big Brother Africa itazinduliwa rasmi. Maandalizi yamekamilika na washiriki tayari wanajifahamu.

  Washiriki watakuwa ni wawakilishi wa nchi shiriki ambazo ni 13 na Rest of Africa ambayo haina mwakilishi lakini ina haki ya kupiga kura. Tutawaona baadhi ya nyota walio shiriki kwenye seasons nne zilizotangulia kuanzia BBA I mpaka BBA IV.

  Nina hisia tofauti kidogo kuhusu show ya mwaka huu. Kuna uwezekano mkubwa show ikakosa msisimko kwa kuwa washiriki watakuwa wanafahamiana strategies zao. Tayari kuna watu wanajulikana kwa sifa ya kuwa snakes, wengine walitumia mahusiano kama strategy, na wengine walitumia ukimya ama kutokuongea kabisa na hivyo wanasahaulika kama wapo.

  Mtu kama Richird akirudi na akamtokea demu, hakuna demu atamwamini tena kutokana na kile tulichokiona kwa RICHIANA. Mtu kama Sheila (Kenya, BBA III) akirudi hakuna mwanaume atamwamini, maana siku Sheila anatoka, TK (Zambia, BBA III) alilia kama mtoto mdogo, kumbe Sheila alikuwa anamtumia tu ili aendelee kubaki ndani ya jumba.

  Mtu kama Kwaku a.k.a Kwaku-T (Ghana, BBA II) ambaye alikuwa anabadilisha wasichana pindi gf anapotolewa. Au mtu kama Code (Malawi, BBA II) ambaye alikuwa anamsalendia Maurine (Uganda) kumbe nje ya Jumba ameacha gf mjamzito. Kuna washiriki walitumia ukimya na kazi za jikoni + usafi wa jumba kama strategy na iliwasaidia kufika mbali, mfano: Hazel (Malawi, BBA III), Geraldine (Nigeria, BBA IV), Cherise (Zambia BBA I) na Ofuneka (Nigeria BBA II).

  Kwenye show kama hizi inapendeza zaidi wakiletwa washiriki ambao hawajuani kabisa na kila mtu anakuwa na strategy yake moyoni na hata kama ataitoa kwa wengine ni kwa malengo ya alliance. Lakini kwa show ya mwaka huu, already washiriki watakuwa wanajua true colors za washiriki wenzao.

  Katika BBA seasons zilizotangulia the top 3 walikuwa ni hawa:

  BBA I: Cherise (Zambia, winner); Mwisho Mwampamba (Tanzania); na Tapuwa (Zimbabwe).

  BBA II: Richard (Tanzania, winner); Ofuneka (Nigeria); Tatiana (Angola).

  BBA III: Ricco (Angola, winner); Hazel (Malawi); Munya (Zimbabwe).

  BBA IV: Kevin (Nigeria, winner); Emma (Angola); Eddie (Namibia).

  Washiriki wengi wa season ya kwanza kabisa kwa sasa watakuwa na maisha ya tofauti kabisa na inawezekana umri umeenda, kwa hiyo uwezekano wa kuwaona ma-star wa BBA I ni mdogo.

  Ambao ningependa kuwaona tena ni pamoja na hawa wafuatao: Kwaku-T (Ghana, BBA II), Sheila (Kenya, BBA III), LaToya (TZ, BBA III), Phil (Uganda, BBA IV), Liziwe (South Africa, BBA IV), Uti (Nigeria, BBA III), Munya (Zimbabwe, BBA III), Bertha (Zimbabwe, BBA II), Meryl (Namibia, BBA II); Maxwell (Zambia, BBA II), Lerato (South Africa, BBA II); Emma (Angola, BBA IV)

  Jumapili saa mbili usiku kwa saa za hapa kwetu siyo mbali sana, tutawaona hao nyota waliowahi kuwika kwenye seasons zilizopita ili tuone watakuja na kipya kipi katika show ya mwaka huu.

  Wapenzi na mashabiki wa BBA karibuni tena kwenye kijiwe chetu, maana kuna wengine walishapotea kabisa, mfano Kelelee sijawahi kumuona tena. Nemesis na Mbogela najua wao ni permanent members wa vijingine.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Jul 17, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mkuu Keil,

  Nadhani Tanzania itawakilishwa na Mwisho Mwampamba (ni ubashiri tu)
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yeah.... kile kipindi cha akina mama kusepa hata habri ya saa mbili kimewadia...

  nahofia wanangu tu!!!
   
 4. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Duu mwisho alivyo choka...dah...kweli nike nike...tumwombee
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jul 17, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kama watashiriki wale waliopita kweli mashindano ya mwaka huu yatakosa msisimko!
   
 6. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wakati wa mimi kubadili Signature umefika, ha ha ha

  Hata mimi naona kama BBA ya mwaka huu itakosa msisimko, pia naona watu wanaweza kuendelea kupiga kura kutokana na record za nyuma, maana watu walioboa kipindi cha nyuma wanaweza wakajikuta sio favourite wa wapiga kura.

  Nabashiri washindi wote 4 kuwa ndani ya nyumba na wote watakosa mshiko, watatolewa mapema, Ningependa kuona Tanzania inawakilishwa na Latoya, nadhani anaweza kufanya vizuri zaidi hasa baada strategy ya Elizabeth ya kugoma mahusiano kugonga ukuta na pia katika washiriki wetu wote Latoya hafahamiki sana, inaweza kuwa advantage.

  Ningependa mtangazaji wa BBA abadilishwe, Jamaa wa mwaka jana alishindwa kumudu kipindi.
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Na avanta pia!
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  It's now live!
   
 9. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #9
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Sadly IK ndiye presenter tena!

  Sean Paul kamaliza ku-perform
   
 10. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  ndio nini?
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  I said it... Mwisho Mwampamba ndiye mwakilishi wa Tanzania!
   
 12. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Jamaa sijui kama kaacha kuvuta sigara maana ile mwaka BBAII alifika mahali kavuta mpaka majani ya chai kitu kilichofanya watazamaji wammind sana, lakini alikuwa entertainer.

  Mwaka huu ulikuwa wa TZ kupeleka mwanaume, tumeshapeleka wanawake 2X mfululizo na kwa vile Richard tayari alikuwa mshindi basi nafasi ilibaki kwa Mwisho.

  ALL The Best Wa KUKAJA
   
 13. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #13
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  I thank myself... Nilibashiri Shein kuwa mgombea wa CCM kwa Zanzibar (ikawa), Nikabashiri Bilal kuwa mgombea mwenza ikawa... Then Sheikh Yahya aanze kujiandaa, namnyang'anya kiti chake ha ha ha

  Jane again... LoL ... 2nd Housemate to enter the house

  [​IMG]
  [​IMG]
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  I love African Music lol
   
 15. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli Inv, hapo nimeboreka sana, Anyway, naona kama Multichoice wamekaa kibiashara zaidi, sasa hivi wanalifukuzia soko linalokua kwa kasi la Nigeria, so presenter atoke huko, na mshindi mwaka jana kutoka Nigeria kumesaidia sana, so watahitaji kumaintain at least kwa mtazamo wangu
   
 16. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #16
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Munya anaiwakilisha Zimbabwe, anakuwa housemate wa nne kuingia
   
 17. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Haha lakini Inv. Sheikh Yahaya alishanyang√°nywa na Pweza Paul, kwa hiyo sasa mpambano wako ni dhidi ya pweza Paul aliyetangaza nia ya kustaafu
   
 18. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #18
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Malawi inawakilishwa na Code, Ethiopia inawakilishwa na Yacob.

  Mbona wanaume wengi???
   
 19. K

  Keil JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu Jane ni wa intake gani? Maana wala simkumbuki. Mkuu Invisible wengine tuko mbali na runinga, endelea kutupatia list ya hao ma ma-star.

  Pia hongera kwa utabiri mzuri kuhusu Mwisho, na mimi niliwaza hilo, but tangu zama zile walipoanza kusema ame-lost nilihisi maisha yanaweza kuwa yamemwendea kombo sana. Lakini kwa kuwa time taker nina imani anaweza kufika mbali.
   
 20. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #20
  Jul 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mkuu huyu ndiye Jennifer...

  Sheila ameingia sasa, anaiwakilisha Kenya. Jennifer anaiwakilisha Mozambique
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...