Pongezi za CCM kwa Richard wa BBA 2 zimetushangaza: Kutafuta umaarufu wasiokuwa nao

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,048
Pongezi za CCM kwa Richard wa BBA 2 zimetushangaza
Tahariri
Tanzania Daima


TUMESHANGAZWA na kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuibuka haraka haraka kumpongeza mshindi wa shindano la Big Brother 2, Richard Bezuidenhout, ambaye Jumapili iliyopita alijinyakulia kitita cha dola 100,000 za Marekani (zaidi ya sh milioni 100) kutokana na ushindi huo.

Tutangulie kueleza mapema kuwa, mshangao wetu huu haumhusu hata punje Richard, bali unaihusu CCM tu. Haumhusu Richard kwa sababu yeye alikwenda kwenye shindano, haijalishi kama shindano hilo lilikuwa likiendana na mila na desturi za Kitanzania, alichokifuata huko ugenini ni kusaka fedha.

Kamwe hatumshangai kushiriki na kushinda shindano hilo, hata kama alilazimika kufanya vitendo ambavyo haviendani na utamaduni wa Kitanzania na vilivyohatarisha ndoa yake, hayo ni matakwa yake binafsi na familia yake ilimuunga mkono.

Hatumshangai Richard kwa sababu wapo Watanzania wengi wanaotumia staili inayofanana na aliyoitumia yeye ndani ya jumba la Big Brother kusaka fedha, baadhi yao ni dada zetu wanaojihusisha na mambo ya urembo ambao hulazimika kutembea uchi mbele ya kadamnasi, lengo likiwa kusaka fedha.

Watanzania watakubaliana na sisi kuwa mashindano ya urembo ambayo hapo awali warembo walikuwa wakijitokeza mbele ya watu wakiwa na vichupi tu yalikuwa yakipingana na utamaduni wa Kitanzania.

Hili lilipigiwa kelele, likapigwa marufuku, lakini bado dada zetu wanaotuwakilisha katika mashindano makubwa ya urembo duniani, husimama mbele ya kadamnasi wakiwa na vichupi tu, jambo ambalo mbali na kukiuka utamaduni wetu, pia linawadhalilisha wao wenyewe mbele ya jamii ya Watanzania.

Tunaamini kuwa, kama shindano la Big Brother lingekuwa linafanyikia nchini, basi lingekwisha kupigwa marufuku na serikali kwa sababu si utamaduni kuangalia watu wakiwa watupu, wakioga au wakifanya vitendo vya mapenzi.

CCM, chama kinachounda serikali yetu, moja ya mambo ambayo kimekuwa kikihubiri ni kudumisha utamaduni wa Watanzania.

Akiwa ndani ya jumba la Big Brother, Richard, kijana mwenye mke, alikuwa akitazamwa na mamilioni ya watu duniani akioga uchi na akifanya mapenzi na mwanamke ambaye si mkewe.

Vitendo hivi vya Richard vilitosha kabisa kumkera mkewe, ambaye kwa mujibu wa vyombo vya habari, alilazimika kutimkia kwao mara tu aliposhuhudia vitendo hivyo vya mumewe kupitia televisheni.

Hata siku akitazama fainali hizo nyumbani kwa baba mkwe wake, alijikuta akitofautiana naye, baada ya kumsikia Richard akilitaja jina la hawara yake huyo mara tu alipotangazwa mshindi, alimtukana (Richard) akatimka ukweni kwake.

Sisi tulitegemea kuwa, CCM, ambayo serikali yake iko katika mapambano makali ya kupunguza makali ya maambukizi ya ukimwi, kamwe isingeshabikia vitendo vya ngono vilivyokuwa vikifanywa na Richard, mume wa mtu, ndani ya jumba hilo.

Ni jambo la kushangaza kwa taasisi ambayo viongozi wake wanahubiri kupambana na ukimwi, wanapanda majukwaani kupima virusi vya maambukizi ya ukimwi, kushabikia ushindi wa mume wa mtu uliochangiwa na vitendo vya mapenzi.

Tunadhani CCM imepotoka, na tunaamini kuwa tabia hii ya kudandia kila aina ya ushindi au mafanikio wanayopata Watanzania, hata kama yana walakini unaweza kuigharimu.

Turejee nyuma kidogo, tuikumbushe CCM kuwa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ilijitokeza mbele wakati wa mapokezi yake, huku ikijua kuwa Dk. Migiro hakuteuliwa kama kiongozi wa CCM, bali wa Watanzania.

Kwa hili la Richard, CCM imetushangaza, kwa sababu mbali na ukweli kwamba haikupaswa kwa namna yoyote kushabikia ushindi huo ambao umesababisha mfarakano wa ndoa ya Mtanzania mwenzetu huyu, ni serikali ya CCM yenye dhamana ya kulinda utamaduni wa Watanzania na kuhakikisha kuwa wanaishi katika maadili mema.

CCM inapopongeza ushindi uliopatikana kwa kuonyesha uhodari wa kufanya mapenzi, tunadhani inakwenda kinyume cha misingi iliyojiwekea, inapaswa kujiangalia upya.
 
chadema wao kwani walikatazwa kumpongeza ??
masuala ya ccm yanawahusu nini wao ??
tokea lini wapinzani wakawapangia ccm nini cha kufanya, kusema ??

waache zao hao watoto wadogo waache kulialia ! ndio kwanza wameingia kwenye siasa halafu wanataka wajifanye wamekubuhu hapa !
 
De point sio chama gani kutoa pongezi...the point ni chama chenu kujitaftia umaarufu katika kila kitu ambacho chaonekana kinaleta umaarufu kwa wananchi...na pia kusema bwa mdogo kashinda eti kutokana na malezi mema aliyopewa na chama chake...shame on ur chama if u ol support aliyesema dat statement.

Kesho keshokutwa litafanyika shindano la ma*aya mzuri zaidi duniani atashinda mtz..ccm kwa vile mshindi atapata hela nyingi... mtashadadia ushindi ule ni wa ccm kwa ujumla as mmemelea!!!angalieni points za kumake in public sio kufungua vinywa tuu ilimradi mmesema..dats y kiongozi wenu (amepelekwa kupumzika as balozi wetu huko asia)aliwahi shindana na media kwa stupid points na kushow udhaifu wenu.

Else mie sina chama so usije jibu or jibizana kukashifu chama kingine...mie ntacriticise pale palipokosewa na kusifia panafostahili.

Lastly mkikosea step jamani muwe mwakubali au kukaa kimya mkiendelea shadadia au shabikia point hiyo while hata nafsi yako yakusuta abt it mwajiabisha watu wazima.
 
ccm kutafuta umaarufu kwani umesikia ccm ni chama chipukizi kama hivyo vyama vingine ??

ccm inayo umaarufu na ndo maana wapinzani wanadonoa punje punje za umaarufu toka kwa ccm !

case closed !
 
chama-less !

ccm hatuhitaji watu wenye reputation kama zile, alipongezwa kwa kuwa ni mtz !
 
nami nahofu ka waijua vyema..ukumbuke kile ni chama cha mafisadi na minafiki...
n usemavyo ccm haihitaji watu wenye reputation kama zile it means mwakubali fika kuwa kijana hana reputation nzuri due to some of his vitendoz ambavyo mmesimama kusema vitendo hivyo vyake mnavipongeza kwakuwa vimetokana na malezi yenu mazuuuuriii!
kweli aliyeita chama chenu kuwa ni chama cha ma**ya hakukosea na hata wewe naona in one way or another umekubali hilo kwa kusay wat u hav just said
 
kada tena n abt ccm kutafuta umaarufu i think wat he was tryin to mean ni kuwa umaarufu wenu mwema wa kisiasa kwa mambo mema waanza kupotea so once likitokea jambo lolote ambalo litattokea shabikiwa na watz kwa wingi....nanyi mwadandia treni kwa mbelee hamjui mwazidi didimia tuuuu
 
nami nahofu ka waijua vyema..ukumbuke kile ni chama cha mafisadi na minafiki...
n usemavyo ccm haihitaji watu wenye reputation kama zile it means mwakubali fika kuwa kijana hana reputation nzuri due to some of his vitendoz ambavyo mmesimama kusema vitendo hivyo vyake mnavipongeza kwakuwa vimetokana na malezi yenu mazuuuuriii!
kweli aliyeita chama chenu kuwa ni chama cha ma**ya hakukosea na hata wewe naona in one way or another umekubali hilo kwa kusay wat u hav just said

let me sniff the air and come back later !!
 
yah bora muwe mwajibu hivyooo kuliko kushadadia ujinga kwa pints zisizo na maana at the end mwaishia ongea pumba mkizidi didimiza lichama lenu...enjoy ya tym
 
..waungwana!

..hamna haja ya kuelekea kugombana kwa sababu ile issue ilikuwa non starter! watu walikurupuka!
 
thawa thawa mkuu ila lichama hili kidooogo lakera hadi mtu waweza jisikia kinya kwa vitendo na pumpa points zao
 
de point sio chama gani kutoa pongezi...the point ni chama chenu kujitaftia umaarufu katika kila kitu ambacho chaonekana kinaleta umaarufu kwa wananchi...

Mkuu kwa nini haya maneno usiwatumie marais mbali mbali wa Afrika, waliomtumia salaam za hongera rais wetu kutokana na kushinda kwa Richie, badala yake unakuja kulia at the wrong place?

Yaaani I do not get it lichama linakera kuliko pumba zako mkuu?
 
Mkuu kwa nini haya maneno usiwatumie marais mbali mbali wa Afrika, waliomtumia salaam za hongera rais wetu kutokana na kushinda kwa Richie, badala yake unakuja kulia at the wrong place?

Yaaani I do not get it lichama linakera kuliko pumba zako mkuu?

ndio hapo sasa !
 
Mkuu kwa nini haya maneno usiwatumie marais mbali mbali wa Afrika, waliomtumia salaam za hongera rais wetu kutokana na kushinda kwa Richie, badala yake unakuja kulia at the wrong place?

Yaaani I do not get it lichama linakera kuliko pumba zako mkuu?

kuhusu kumpongeza hata mie nampongeza sana tuu!
sijakataaa kushinda kwa mtz mwenzetu wala sijapinga...wat chapingwa hapo ni kauli ya kusema kijana kashinda kwa kutokana na malezi mazuri aliyopewa na ccm......
sijui waona point yangu hapo??
 
yah bora muwe mwajibu hivyooo kuliko kushadadia ujinga kwa pints zisizo na maana at the end mwaishia ongea pumba mkizidi didimiza lichama lenu...enjoy ya tym

hasira za nini tena ?? kapige matofali ngumi kama unaweza !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom