Treni ya mizigo toka bandarini haipiti kule kwenye eneo la jengo la stesheni kuu, hata hii narrow gauge ya mizigo iliyopo inapotokea badarini hua haiingii moja kwa moja pale jengoni.
Ili kuondoa usumbufu kwa abria pale stesheni na ucheleweshaji wa mizigo, treni ya mizigo ina-shunt moja kwa moja toka bandarini na ku-bypass stesheni kuu, toleo lake litakua mbele kidogo pale viaduct kubwa ya SGR kuingilia stesheni kuu linapoanzia nadhani ni eneo la Mtaa wa Utete. So gogo la mizigo halitapita juu ya lile viaduct kubwa (the 2 km one).
Kwa ujumla SGR toka Dar es salaam kuanzia steheni kuu na eneo la badarini kuelekea nje ya jiji, design inaonyesha kutajengwa jumla ya viaducts 4, ile kubwa ya urefu wa km 2 pamoja na nyingine ndogo ndogo 3, ya mwisho kabisa itakua na urefu wa kama mita 100 hivi.