Sasa ninaona baada ya kuona Kenya imeshindwa kupambana na Tanzania, umeanza kuhamisha vita unajaribu kutaka kuingiza Botswana, acha sababu za msingi, nani aliyekuambia Tanzania inaizidi Botswana katika vivutio vya utalii?, wewe acha kuhamisha goli, hapa mtinange ni kati ya Tanzania na Kenya, usijaribu kuitoa Kenya katika hii mechi, kama Kenya imeshindwa kupambana na Tanzania inapaswa ukae Kimya, achana na kulinganisha na nchi nyingine, utalii wa Botwsana uliendelea siku nyingi hata kabla ya uhuru kutokana na kuwa karibu na makaburu wa Afrika kusini, Botswana ina population kubwa sana ya wazungu waliowekeza sana katika sector ya utalii, serikali ya Botswana ndiyo nchi pekee hapa Africa ambayo mapato yake ni makubwa kuliko matumizi, hivyo kubaki na pesa ya ziada inayoiwezesha nchi kujenga miundomsingi yote muhimu kwa ajili ya utalii na mambo mengine, bajeti ya wizara ya utalii Botswana ni kubwa kuliko bajeti za utalii za nchi zote za EA combined. Acha kuzungumza vitu usivyovijua, Kenya imezidiwa na Tanzania katika utalii, unajaribu kuhamisha goli.