NB: Mipaka ya nchi inapoishia, ushindani wa ndani unapaswa kusimama. Katika diplomasia ya kimataifa, mataifa hayashindani kama vyama vya siasa, bali yanashindani kama dhumuni moja la kitaifa dhidi ya mataifa mengine. Tofauti za ndani hazipaswi kupelekwa nje kwa sababu zinafifisha nguvu ya nchi ya kujadiliana au kujitetea.
Ushindani wa kisiasa, utofauti wa kiitikadi, na mijadala ya ndani ni mambo ya kawaida na ya afya katika demokrasia yoyote. Ndani ya nchi, vyama na makundi yanaruhusiwa kupishana vikali ili kujenga nchi.
Rais anaposafiri nje ya nchi, haendi kama mwenyekiti wa chama fulani cha siasa, bali anaenda kama Mkuu wa Nchi (Head of State).
Anakuwa ndiye nembo, sauti, na uwakilishi wa wananchi wote (ikiwemo wapinzani wake wa ndani).
Kushambulia, Kumdharirisha au kudhoofisha hadhi ya Rais akiwa nje ya nchi kunatafsiriwa kimataifa kama kudhoofisha Taifa lenyewe, jambo linaloweza kupunguza ushawishi wa nchi hiyo kiuchumi, kisiasa au kiusalama.