Hizi sabotage zipo wazi, wanaomiliki malori na vituo vya mafuta tunawajuwa.
Ni wazi reli inarubuniwa, ndiyo maana hata kipande kuungia bandarini, bado kina sua sua, ili biashara za watu ziendelee. Mambo ya hovyo sana.
Uharibifu wa BRT, ni hao hao wamiliki wa boda boda na dala dala, lakini pia kunaweza kuwa na kundi lililotaka kuharibu maandamano ya amani, kuyafanya yaonekane ya vurugu kama walivyofanya kwenye Occupy Wallstreet, miaka michache iliyopita.
Pia uwezekano wa baadhi ya WaKenya kuhusika upo, ila siyo kwa kiwango cha juu kama hawa watu wetu, wenye uchu wa mali.