ichoboy01 uko wapi aisee?
Nashukuru sasa watu wameanza kujadili details.
Kuna watu wengi walikuwa wananiuliza kwanini
Venus Star amebadilika, kipi kimemsibu.
Ndugu zangu napenda kuwaambia mimi nafanya mambo bila kukurupuka huwa nafanya utafiti na kisha nakuja na conclusion
1. Matukio ya
Polepole, mnauhakika kweli huyu Polepole alikuwa upande wa Magufuli? Polepole ameibuka juzi kati na kuanza kutoa maelezo kuhusu Kifo cha Magufuli. Polepole alikuwa Katibu wa Itikati na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi. Yeye na Bashiru walikuwa na ugomvi usioisha ndania ya chama. Bashiru alikuwa Katibu mkuu wa CCM. Hawa watu wawili walimsumbua sana Magu akiwa mwenyekiti maana walikuwa hawaelewani na kusababisha ugomvi wa mara kwa mara ndani ya CCM.
KUHUSU POLEPOLE
Polepole toka akiwa kijana alikuwa kwenye Civil Society na baadaye kuteuliwa kuwa Rais wa Civil Society Tanzania. Baada ya hapo kuna matukio ya Ulimboka na vyama vya madaktali kugoma. Polepole yeye ndiye aliyekuwa akitumwa na Kikwete kwenda kuongea na kundi la Ulimboka ili waache mpango wao.
Siku ya kabla Ulimboka kutekwa alikaa na Polepole pale mlimani city, Polepole akimsihi ulimboka aachane na mpango wake. Walikaa kutoka Saa 12 jioni mpaka zaidi ya saa 5 za usiku. Ulimboka aligoma. Ndio kutekwa na kuteswa kulitokea baadae.
Polepole alimbiwa na Kikwete kuingia kwenye Tume ya Katiba ya Warioba. Kikwete aliwaacha watu wasomi waliokuwa kwenye Civil Society kama akina
Meena akamchukua Polepole. Yalitokea yaliyotokea kila mtu aliona, Polepole alizunguka nchi nzima akiihubiri Rasmu ya katiba iliyoundwa na Warioba huku akimponda Kikwete. He was creating a chaos ili watu wachanganyikiwe. Polepole hakuwahi hata siku moja kufanywa chochote.
Kipindi cha Maazimisho ya siku ya wafanyakazi yalipangwa yafanyike Mwanza. Polepole alipanga kuanzisha Mkutano wake huko Geita ili kuvuruga mkutano wa Kikwete. Kilichotokea, Polepole alifungiwa kwenye hotel tu na Hotel hiyo huko geita kuzungukwa na walinzi. Baada ya mkutano wa Kikwete kuisha aliachiwa na kupewa nauli ya ndege kurudi Dar.
Inabidi sasa tujiulize Polepole alisema yeye yupo na viapo viwili, viapo hivyo ni vipi? I know Polepole Personaly siyo kusimuliwa tu. Baada ya kifo cha Magufuli alikubali kuteuliwa kuwa Mbuge na Rais Samia. Baadae alikubali kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi kisha Balozi wa Cuba. Polepole alianzakuona kabisa Ndoto zake kubwa zinaanza kuziwa taratibu. Polepole alikuwa na uadui mkubwa na Ummy Mwalimu.
Cha kujiuliza zaidi, Kwanini huyu Polepole alikuwa kimya baada ya kifo cha Magufuli mpaka ilipofika muda huu? Hao wa akina Polepole ndio walikuwa washauri na wasaidizi wa Magufuli wa karibu sana, walifanya nini kumlinda Magufuli asiuliwe? Polepole alikuwa anaaminiwa sana na Magufuli. Alifanya nini kumlinda au kutoa ushauri?
Kwenye Comment hii naomba niweke swali hili. Nitaendelea kushusha nondo ili watu wanielewe.
Kwanini niliamua kubadilika