Mkuu nadhani wewe ndo tunaongelea theories , mpaka sasa hakuna hela inayoelelezwa kwa ajili ya ujenzi wa hivyo vipande ulivyosema kwa sababu hela za ujenzi huo tayar zinashatafutwa kwa kutafuta mikopo.
Mkuu hakunaga kuanza serikalini , lazima tujiulize hizo hela zote zinaenda wapi sababu bado tuko kwenye grace period( hatujaanza lipa mkopo wa sgr) kwa hiyo gharama tunayolipa ni kwa ajili ya uendeshaji na opareshen tuu, sidhan kama kuna hata hela inavyoenda serikali kuu
Sijajua inachomaanisha ila chukua mfano tu una kampuni ya mabasi na inafanya usafirishaji wa vifurushi mpaka Dom ila Huna sehemu ya kuhifadhi pale wateja wanapochelewa ila unataka wawekezaji wengine wa kujengee, lazima upotee tu
Tusifagilie private sana , maana hata hao wawekezaji wengi wao ni wageni tuuze hisa ili tupate hata wawekezaji wadogo kutoka ndani ya nchi
Unachosema ni theory huwa wanaformula kwa ajili ya pesa ya mfuko mkuu, maendeleo na uendeshaji. Mimi nipo kwenye pesa ya maendeleo kwa sasa, wangekuwa wanatenga hata 800mil kwa mwezi inayotokana na pesa ya maendeleo kwa ajili ya miundombinu sawa. Leo hii wameshindwa hata kuingiza reli ya pili pale Dodoma terminal kwa kisingizio Cha operation cost.
Tusiwatetee trc ni wazembe tuu
Unaendelezaje hivyo vipande huku watu wanasubiria mwezi mzima kupata behewa la mgr kusafirisha mzigo huku kina mabehewa maelfu yamejazana pale pugu
Hakunaga pesa ndogo ila nia , tukisema ufanyike ukaguzi ambao hauhusishi ofisi ya cag letsay wawe kpmg utakimbia kwa wizi uliopo trc
Tunashindwa kuendelea kwa mentality kama zako kwa kuamini kuwa haiwezekani