Mimi sijui ile Botanical garden kwa nini imetelekezwa kabisa pamoja na kuwa karibu na ikulu vile.
Kwanza lile eneo lote lilipaswa kuwa la tourism. Kuanzia museum ( waache kutoza laki tano kuchukua video), hiyo ikulu yenyew ingefanywa museum tu.
Mtalii anatembelea city Centre anatembea kuanzia askari monument, anavisit historic Azania front Cathedral, anatembelea st Joseph Cathedral, anaview port ya Dar na german boma, anaingia ndan ya museum ya sasa na hiyo ikulu, anavisit botanical garden ananyoosha mpaka beach. Gymkana inaweza boreshwa nayo, wengine wanaweza tembelea kisutu ile wakafeel old Dar nk.
Hayo majengo ya kizamani yasiyo na watu city Centre mfano yale karibu na mahakama kuu na wizara ya ardhi na mengine mengi yasiyo na watu yangegeuzwa restaurants zenye several dishes including all Tanzanian food, bars, nightclubs, na mengine hostels na Airbnbs.
Wahakikishe eneo lote linakua walkable, zile sidewalks zisambae posta yote na waondoe Boda na bajaji city center
Watu wanaweza tembelea dar kwa hayo tu na tukapata hadi watalii million kwa mwaka kwa kisehemu hiko tu. Utalii si lazima iwe beach au Mbuga za wanyama.
Barcelona inatembelewa na watu million 30+ na sio kwamba wana simba kule ni citu tourism tu. Watu wanatembelea Barca kula tu Spanish food.