Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Kipindi Cha magu kulikuwa na dawa ? Vipi kipindi Cha aliwajali watumishi au aliwahi ajiri maana maendeleo ni pamoja human development .
Mkuuu magu alikuwa jambazi na ufisadi wake upo Kila Kona
Mwaka 2013 Wizara ya Ujenzi ilingia No. AE/006/2012-13/HQ/G/CN-39 tarehe 25th April, 2013 na M/s Johs.Gram-Hanssen Bergensgade 10, DK 2100 Copenhagen Oe Denmark kutengeneza ferry ya abiria ya Bagamoyo-Dar jumla ya USD 4,980,000. Mkataba huu ulitakiwa kuanza 25th April, 2013, na uliongenzwa mda wa kuisha31st October, 2014(Rejea barua No.TMS/F/86/A/22).

Katika ukaguzi tumegundua mambo ya kusikitisha

  • Spidi ya ferry haiendani na ushauri na mahitaji ya wataalam. Wakati wa majaribio spidi ya Ferry ilikuwa mbaya sana, kati ya 19.45knots mpaka 17.25 knots kinyume na spiki iliyokubaliwa kwenye mkataba yaani 20 knots. Pungufu hili kubwa limesababisha ferry ishindwe kufanya kazi na hivyo kukosa thamani ya fedha. Huu ni ufisadi
  • Mkandarasi kushindwa kukabidhi hati Pamoja na kuwa ferry ilikabidhiwa kwa kuchelewa(ilikabidhiwa tarehe 17th November, 2014), ilikabidhiwa bila hati “goods certificate of acceptance’’ kinyume na taratibu za manunuzi, Reg.247 of PPR, 2013. Hata hivyo mpaka ukaguzi unamalizika hati haikuwahi kukabidhiwa na hakuna hatua zozote zilizowahi kuchukuliwa kwa wahusika. Hii imesababisha technical issues kutokurekebishwa kiwango cha kufanya kazi.
S
Sawa mkuu nakubaliana nawewe ila inakuwaje barabara kama ya iyovi- mafinga ambayo ndo barabara inayobeba mzigo kuliko barabara zote nchi hii isiwe na viraka miaka na miaka ila barabara ya songea -masasi isiyo na idadi kubwa ya magari iwahi kuchakaa na kuwa na mahandaki wakati ukiangalia gharama ya ujenzi kwa km karibia zote ziko sawa?
Vipi upana wa barabara ya iyovi- na Ile ya hizo nyingine kama songea - masas unaendana? Iweje zote zijengee kwa gharama zinazokaribiana ila kuwepo na utofauti wa upana?
Mkuu unajua ukipunguza hata nusu MITA kwa km 100 ni mamilion hayo
Mafinga imerudiwa Kaka, hiyo Barabara imejengwa upya. Hata ukienda Leo imepanuliwa na kuwekewa mitaro.
 
S
Mafinga imerudiwa Kaka, hiyo Barabara imejengwa upya. Hata ukienda Leo imepanuliwa na kuwekewa mitaro.
Mkuu imetudiwa lini kwa sababu toka miaka 1990 kulikuwa na barabara .
Serikali ikaingia mkataba 19/03/2008 na AARSLEFF- INTERBETON kuijenga upya . Ile barabara ilifumuliwa upya
 
Mkuu imetudiwa lini kwa sababu toka miaka 1990 kulikuwa na barabara .
Serikali ikaingia mkataba 19/03/2008 na AARSLEFF- INTERBETON kuijenga upya . Ile barabara ilifumuliwa upya
This project is for the rehabilitation of the following roads in Tanzania: Mafinga – Igawa Road Section, Lot 1: Mafinga ...End of the details preview. Please Log in or Subscribe for ALL the information.
 
This project is for the rehabilitation of the following roads in Tanzania: Mafinga – Igawa Road Section, Lot 1: Mafinga ...End of the details preview. Please Log in or Subscribe for ALL the information.
Hata ukigoogle inakuletea mpaka tender. Hii Barabara naijua nimekuwa nikipitisha magari naleta viazi Dar kuuza
 
This project is for the rehabilitation of the following roads in Tanzania: Mafinga – Igawa Road Section, Lot 1: Mafinga ...End of the details preview. Please Log in or Subscribe for ALL the information.
Mkuu ningependa kujielimisha unaweza kunipa link ambayo inasema ilikuwa ni ukarabati wa hiyo barabara maana kabla ya hapo ilikuwa nyembamba ya kikoloni ikaja ikatanuliwa mpaka kufikia ule upana , nisaidie link nifute ukambumbu wangu
 



Mkuu soma hii sijaona sehemu kukarabati labda unioneshe wewe

Rais Magufuli afungua barabara ya Iyovi - Iringa - Mafinga, na afungua kiwanda cha Silverlands

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Mei, 2018 amefungua barabara ya Iyovi – Iringa – Mafinga yenye urefu wa kilometa 218.6 ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Dar es Salaam – Tunduma (TANZAM), inayounganisha Bandari ya Dar es Salaam na nchi jirani za kusini mwa Afrika zikiwemo Zambia, Zimbabwe, Kongo-DRC na Malawi.
Sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo zimefanyika katika eneo la Ihemi, Iringa Vijijini na kuhudhuriwa na Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Naibu Balozi wa Denmark hapa nchini Bi. Camilla Christensen, Wabunge, viongozi wa dini na viongozi wa siasa.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema ujenzi wa barabara hiyo umegharimu Shilingi Bilioni 282 zilizotolewa kwa mkopo nafuu kutoka Serikali ya Denmark kupitia Shirika lake la misaada (DANIDA) na Shilingi Bilioni 1.8 zilizotolewa na Serikali ya Tanzania.​

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa amesema mbali na barabara hiyo Denmark imeshirikiana na Tanzania kukarabati barabara za Ubungo - Mlandizi(kilometa 60.7), Chalinze – Melela (kilometa 129) na Chalinze – Segera – Tanga (kilometa 246.7) na amebainisha kuwa kukamilika kwa barabara hizo kutasaidia kuimarisha usafiri na shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo na biashara.
Naibu Balozi wa Denmark hapa nchini Bi. Camilla Christensen ameelezea kufurahishwa kwake na kukamilika kwa ujenzi huo na amesisitiza kuwa uhusiano wa Tanzania na Denmark ulioanza miaka 50 iliyopita utaendelea kudumishwa hususani katika vipaumbele vinavyohusu uchumi na fedha, afya, ajira na uboreshaji wa biashara.
Mhe. Rais Magufuli ameishukuru Serikali ya Denmark kwa kufadhili miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa barabara ya Iyovi – Iringa – Mafinga ambayo itasaidia kuboresha maisha ya watu kwa kuwarahisishia kupata masoko ya mazao na bidhaa zao pamoja na kukuza uzalishaji mali.
“Ndugu zangu wananchi wa Iringa, barabara hii imekamilika na ni miongoni mwa barabara bora tulizonazo hapa nchini kwetu, natoa wito kwenu mchangamkie fursa, limeni mazao ya kutosha na myasafirishe kwenda kwenye masoko mbalimbali ya ndani na nje ya nchi” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameiomba Denmark kupitia DANIDA kufadhili ujenzi wa barabara ya Igumbiro – Kihesa yenye urefu wa kilometa 11 ambayo itasaidia magari yatokayo kusini mwa Tanzania kwenda Dodoma kutopita katikati ya Mji wa Iringa ili kuepusha msongamano na athari za ajali za magari zinazoweza kutokea.
Mapema asubuhi Mhe. Rais Magufuli amefungua kiwanda cha kutotoresha vifaranga na kuzalisha chakula cha kuku cha Silverlands kilichopo Ihemi, Iringa Vijijini.
Mkurugenzi wa Silverlands Dkt. Ben Moshi amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha vifaranga 150,000 kwa wiki na tani 40 za chakula cha kuku kwa saa, na kwamba mwaka huu kimezalisha vifaranga 7,200,000 ambavyo vimeuzwa ndani ya nchi na nchi nyingine zikiwemo Ethiopia, Kenya, Nigeria na Uganda.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema uwepo wa kiwanda hicho utawasaidia wakulima kupata soko la mazao kwani kinahitaji tani 120,000 za mahindi kwa mwaka na tani 40,000 za soya, na amesisitiza kuwa teknolojia inayotumika inamwezesha mfugaji kuzalisha kuku bora wasiokuzwa kwa kutumia dawa na virutubisho vya kikemikali.
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wawekezaji wa kiwanda cha Silverlands kwa uwekezaji mkubwa wa Dola za Marekani Milioni 71 na kutoa ajira kwa watu 938 lakini amewataka kulipa kodi za Serikali kama inavyopaswa badala ya kusingizia kuwa hawapati faida.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
 
Mkuu ningependa kujielimisha unaweza kunipa link ambayo inasema ilikuwa ni ukarabati wa hiyo barabara maana kabla ya hapo ilikuwa nyembamba ya kikoloni ikaja ikatanuliwa mpaka kufikia ule upana , nisaidie link nifute ukambumbu wangu
Mkuu ningependa kujielimisha unaweza kunipa link ambayo inasema ilikuwa ni ukarabati wa hiyo barabara maana kabla ya hapo ilikuwa nyembamba ya kikoloni ikaja ikatanuliwa mpaka kufikia ule upana , nisaidie link nifute ukambumbu wangu
CONTRACT NO. TRD/HQ/1057/2016/17
BIDDERS
Dr. Geoffrey M. Rowe
Dr. Joseph Anochie – Boateng
Dr. Martin Bizaliele Mgangira
AWARDED Dr. Geoffrey M. Rowe
SIGNING DATE 14/06/2017
CONTRACT AMOUNT USD 54,004.40
CONTRACT DURATION 8 Weeks
 
Several unaziona wewe tuu ,mbona humu hatuoni? 😂😂
Ni nini mnajenga yenye haziko Kenya tofauti na BRT? By the way Tanzania is only trying to do catch up, there is nothing else you do to put Tanzania ahead of Kenya.
 
CONTRACT NO. TRD/HQ/1057/2016/17
BIDDERS
Dr. Geoffrey M. Rowe
Dr. Joseph Anochie – Boateng
Dr. Martin Bizaliele Mgangira
AWARDED Dr. Geoffrey M. Rowe
SIGNING DATE 14/06/2017
CONTRACT AMOUNT USD 54,004.40
CONTRACT DURATION 8 Weeks
Mkuuu ulicholeta ni vitu viwili tofauti
Mkuu hivi unaweza karabati km 200 kwa USD 54,004.4
Screenshot_2024-11-08-14-18-33-46_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Back
Top Bottom