Embu uache ubishi we jamaa.
Taratibu za Tanzania afisa tabibu msahara wa kwanza laki nane na nusu za shilingi pamoja na marupurupu.
Daktari wa intern mwenye degree hupewa laki tisa na nusu mpaka milioni moja na laki moja.
Daktari wa degree ambaye ameshaajiriwa mshahara wa kwanza milioni moja na laki nne.
Uwe unaacha ubishi wa kitoto.
NIKUONGOPEE ILI NIPATE FAIDA GANI??
Badilisha hizo fedha kwenda kwenye dola.
Ukisemea hivyo nikianza kutaja Morogoro,Pwani,Tanga,Iringa,Mwanza na kwingineko maisha ni bei rahisi saaanaaaaa kuliko SEHEMU YEYOTE KENYA.
Na Dar es salaam kilicho bei ni masuala ya ujenzi labda na makazi.
Ila kuanzia vyakula mpaka mavazi mpaka matibabu hakujatofautiana na mikoa mengine.
Bado unaendekeza ubishani wa kitoto narudia tena laki nane mpaka laki tisa ya ki-Tanzania ina uwezo kusukuma maisha ya Mtanzania tena akiwa na familia.
Je kes elfu sabini ina uwezo wa kusukuma maisha ya Mkenya mwenye familia??
Nenda rudi mshahara wetu ni toshelezi wala sio umasikini BALI MSHAHARA WETU TOSHELEZI kwa gharama za maisha kitu ambacho Kenya kiko tofauti.
Hapa tutabishana mpaka kesho.