Hivi naomba kuuliza wazee. Mbona hawa Niger wamewakalia kooni sana kwani ndio nchi ya kwanza au ya pekee kufanya mapindizi ya kijeshi kwa miaka hii??
Mkuu, Umoja wa Afrika miaka 25 iliyopita ulitoa azimio la kutokomeza mapinduzi ya Kijeshi Afrika, na kutotambua utawala wa kijeshi, ndio sababu yakitokea mapinduzi yoyote pale Afrika, hatua ya kwanza ni AU kuitenga na kutotambua utawala wa kijeshi, huku wakitumia mbinu za mazungumzo Ili kuhakikisha utawala wa kiraia unarudishwa haraka Sana.
AU haina jeshi, kwahiyo hawana uwezo wa kuingilia Kijeshi Ili kurudisha utawala wa kiraia, AU hutegemea Sana jumuia za kikanda katika matumizi ya nguvu Kama ECOWAS, SADC na EAC.
ECOWAS imejikuta kwamba imefanya makosa kwa kutoingilia Kijeshi katika nchi za Mali, Chad na Burkina Faso, huko walitumia njia za kuzitenga na kuweka vikwazo(diplomatic &economic means) wakitegemea kwamba zinatosha kurudisha tawala za kiraia.
Baada ya kugundua kwamba njia za kidiplomasia hazizai matunda na mapinduzi yanazidi kushika kasi, Sasa wameamua kutumia njia za Kijeshi, Ili kutoa onyo kwa nchi zingine zenye kufikiria kufanya hivyo, na zile ambazo zimefanya hivyo kuharakisha mchakato wa kurudisha utawala wa kiraia.