Bado nasisitiza uchumi wa Tanzania hautegemei miradi, mradi wa JNHP ni zaidi ya $3B sehemu kubwa ya hizi pesa zinaenda kuagiza mitambo nje ya nchi na kulipa constructors wa nje, excavators, bulldozers, loaders, trucks na mitambo mingi inachukua pesa nyingi sana kwenye miradi na yote hii inatoka nje ya nchi, diesel na petrol, lubricants na oils ni imported goods
Pesa inayobaki Tanzania ni mishahara, cement, nondo, mbao, food supplies na vitu vingine standard vinavyopatikana locally ambapo kwa miradi mingi mambo yote haya huwa ni 20% mpaka 30% ya gharama kuu ya mradi, ni watanzania wangapi wanaoajiriwa kwenye miradi na wenye viwanda vya hizo bidhaa watanufaika na huo mradi mpaka useme uchumi wa nchi nzima unategemea miradi? Labda hata 10k hawafiki directly and indirectly kwa mradi mmoja katika watanzania million zaidi ya 60