Mkuu upo "biased" Sana, yule mtoto alipigwa risasi na polisi, hilo lilikua ni kosa na polisi mwenyewe amekamatwa yupo ndani, Sasa hapo haki za binadamu zinakujaje wakati ni kosa la jinai na mtenda kosa amekamatwa?.
Hawa waandamanaji hawafanyi maandamano ya amani, wanachoma magari na kufanya uharibifu mkubwa Sana, lakini hakuna hata mmoja aliyepigwa risasi au kuuliwa, ingekua Afrika, Uarabuni, au nchi zingine hivi Sasa zaidi ya waandamanaji 300 wangekua wameuliwa, Kama ilivyotokea huko Iran hivi karibuni.
Kama kawaida Iran ilikua inasingizia nchi za Magharibi kuwa ndio zimechochea maandamano, lakini huko Ufaransa kamwe hawapeleki lawama kwa nchi yoyote, wao wanajua hilo ni tatizo lao na wanalitafutia ufumbuzi wao wenyewe. Ninakuhakikishia ingekua ni Afrika ungesikia "mabeberu hao ndio wanaochochea ghasia, hawa wanaofanya fujo ni vibaraka wa nchi za Magharibi". Juzi tu maandamano kidogo tu ya kupinga DPW wewe binafsi ulishaanza kusema "Ingekua DPW ni wazungu wasingeandamana".
Wiki ijayo Kenya wanaanza maandamano, hata bila kuharibu kitu chochote, watapigwa risasi na polisi hata Kama maandamano yatakuwa ya amani. Mkuu lazima ukubali kwamba wenzetu demokrasia na haki za binadamu wapo mbali Sana, tunapaswa kujifunza toka kwao.
islander M
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app