Alikuwa na maono mno. Muda unazidi kumprove right.
Katika hii hotuba yake alizungumza kwamba "dhambi ya ubaguzi haiwezi kuisha, lazima itaendelea
Ninalinganisha na kinachoendelea Sudan hivi Sasa. Hawa waarabu walianza kuwatenga watu weusi wa kusini kwa kisingizio kwamba sio waislam. South Sudanese walipoanzisha vita vya kujitenga, raia wa Jimbo la Darfur ambao ni weusi lakini ni waislam, waliungana na waarabu kuwapiga watu wa South Sudan.
Wakati South Sudan wanakaribia kushinda na kupata Uhuru wao, watu wa Darfur nao wakaanza kubaguliwa kwa kigezo Cha rangi zao, Omar Albashir, rais wa Sudan wakati ule, alianzisha kikosi Cha Janjawed, ambacho 90% ni waarabu wanaoishi Darfur Ili kuonyesha Dunia kwamba hana ubaguzi Wala ugomvi na watu wa Darfur. Hawa Janjawed waliua raia wa Darfur weusi zaidi ya laki 3.
Baada ya Dunia kuingilia kati na kupeleka majeshi ya kulinda amani huko Darfur, Janjawed wakaamua kuondaka huko Darfur na kuja Khartoum kuwa kundi maalum la wanamgambo chini ya Albashir, lakini kwa sababu sio wenyeji wa Khartoum, wao wametoka mashambani, wakaanza kubaguliwa na wakuu wa jeshi ambao waliwakuta hapo Khartoum. Wameamua nao kupigana kupinga kubaguliwa.
Conclusion: Dhambi ya ubaguzi ni Kama kula nyama ya mtu, ukishakula nyama ya mtu, utaendelea tu....