Sijauliza kwamba ni constitution au hapana, niliuliza sababu iliyosababisha kutomteua Tena.
Nadhani unajua kwamba CAG alikua na mgogoro mkubwa na bunge, jambo lililosababisha bunge kukataa kushirikiana na CAG.
Kumbuka kazi ya CAG ni kuangalia Kama kweli serikali inatumia pesa na rasilimali za nchi Kama ilivyoelekezwa na bunge, ripoti yake lazima ipelekwe bungeni kufanyiwa kazi na wabunge kwa kufuata maoni na mapendekezo ya CAG. Kama bunge limekataa kufanyakazi na CAG, kweli ni busara huyo CAG kuendelea kuwepo?.
Kwasababu CAG ni mteule wa rais, katika mazingira hayo ya "stalemate", ungemshauri rais afanye nini Ili kazi za kuisimamia serikali ziendelee?.