70% ya watanzania wanaoishi vijijini huwa hawañunui Vyakula. Tanzania Ugali sio "staple food" katika maeneo yote ya nchi, kwahiyo hata Kama bei ya unga ikipanda, sio tatizo la nchi nzima.
Hivi Sasa huku kijijini ninakoishi, ndoo Moja ya mahindi iliyojaa ambayo ni sawa na 23Kg ni Tshs 16,000. Ukiamua kusaga bila kukoboa utapata 23kg, bei ya kusaga ni 2000.
Kwahiyo utapata 23kg kwa Tshs.18000. Huko mjini lazima bei itaongezeka kutokana na gharama za usafiri na overheads costs zingine.
Sasa Kama 70% ya watanzania wanaoishi vijijini, na kati ya hao wanaoishi vijijini 60% hawategemei kununua mahindi, badala yake hujilimia chakula Chao, kupanda na kushuka kwa bei za Vyakula mijini hakuna athari kubwa kwa watanzania wengi
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app