Kuna tofauti kubwa katika undeshaji wa uchumi wa kenya na uchumi wa tanzania.
Uchumi wa Kenya unaendedhwa kwa front loading economy ( uchumi bandia), ni uchumi unao endeshwa kwa kuchapisha pesa na kidogo kinacho zalishwa na kuki -export kinatumika kama dhamana na kuservice madeni. Kenya haina uwezi wa kujiendesha kama nchi bila kukopa hata kidogo.
Thamani ya uchumi wao (mapato) ukifananisha na deni, wana kosa uwezo hata kulipa mishara ya wafanyakazi wao wa umma.
12 % uzalishaji na akiba - 112% ya uchumi wao wote deni na dhamana walizochukua.
Kenya ni nchi iliyo filisika kwa mizania ya Traditional standards za kiuchumi kama zilivyo Marekani/ Uingereza/Ufaransa/ na karibu nchi zote za ulaya magharibu kutoa nchi chache tuu kama Ujerumani.
Katika bara la ulaya ni nchi tatu ndizo zenye uchumi halisi Germany, Russia na Belarus. Zote zilizo baki zina chapisha pesa kuwawezesha kuendesha uchumi na shuguli za serikali zao.
Na kwa leo hii ni Russia pekee ndio nchi yenye kubaki na bakaa yani wanatumia pesa kwa mahitaji yao yote na pesa inabaki japo inatengeneza chuki na wivu mzito wa kiuchumi na wenzake wa Ulaya wanaochapisha pesa kuendesha chumi zao.
Muda mwingine nitajaribu kufafanua uchumi wa Tanzania ila napata shida sana kwa kutumia lugha yetu kwa maandiko ya kitaalamu, kukiwa na makosa tusameheane. .