Mkuu. Mimi nimeshaingia kwenye kilimo rasmi,sasa hivi huwezi kuniambia kazi za kajiriwa, sasa hivi mjini nakuja kuosha macho and then narudi zangu shamba ili muda wa kuja kustaafu (60yrs)kwa mtu aliyeajiriwa niwe nimeshatengamaa kiuchumi.
Unamkuta mtu ameajiriwa lakini hawazi maisha ya kustaafu. Miaka 45 anasema bado anaponda maisha. Miaka 2 kabla ndipo anaanza kuwaza ataishije mwishowe anajifia kwa depression.
Tukilima kwa malengo kilimo kinalipa sana. Mtaji ni ardhi tu mengine yanakuja yenyewe.