Na ndio hapo huwa sioni sababu za ATCL kushindwa kutoboa, yaani Bongo ni destination alafu pia ni transit, tukiwa serious kwenye Airline business hata Wahabeshi hawatatufikia. Moja kati ya vitu nitamshukuru Magufuli (RIP) ni kufufua ATCL na kununua ndege na kuboresha miundombinu, kwa hili aliona mbali sana na alilisimamia vilivyo.
Imagine tunaongelea kuwa na Watalii 5M by 2025, unajua ni trip ngapi za ndege hizi? Let’s say ATCL ipate tu 30% ya hizo trips kama direct flight to destination, haijatoboa tu? Tununue ndege za kutosha, hawa jamaa hawana cha kutushinda na ndege zao hizo walizotuibia.