Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Broo ww huelewi tuu we achaa tuu watu wanapiga hela saivi we acha tuu mfano mdogo ni kwenye sensa iliyopita makarani walikua wanapaswa walipewe posho kwa kila kikao wanacho udhuria cha ajabu ni kwamba kuna makarani hawakulipwa na kama walilipwa walipewa nusu ya kile walichostahili kupewa sasa iyo hela yote imeenda mifukoni mwa watu wasiofaa aya mradi mwinginee wa upigaji ni zile pesa za mkopo kwa vijana na wakina mama akifuatilia kwa karibu asilimia kubwa ya mkopo wamepewa watu ambao wako uvccm au CCM kwa ufupi hayo ni baadhi ya mambo tuu ila yapo madudu kibao hususan kwenye haya mavikao na makongomano
 
Kulingana na hiyo picha sababu hamko kwa list ya wanaodefault loans
So unajisifu nchi yako ku default kisa SA, Egypt na Nigeria nazo zime default, nyie Wakenya ni lini mtapata akili? Jirani yako akiwa shoga basi na wewe kuwa shoga itakuwa poa tu si ndiyo?
 
Mkapa alipitisha tu kama raisi ila mambo mengi aliyafanya jpm akiwa kama waziri.
Mawaziri wa sasa hivi no ubunifu wanasubiri maelekezo Toka juu
 
tuusan, nchi lazima iwe na vipaumbele na kuvisimamia kwa nguvu zote. Enzi za Nyerere vipaumbele vilikua ni Elimu, Afya, kilimo na viwanda.
Kwa uwezo wa uchumi wetu wakati ule, hayo yalitosha Sana kukausha pesa ya taifa.

Nyerere alifanikiwa kujenga shule nyingi na kutoa Elimu na Afya Bure, wakulima walipewa pembejeo Bure au kwa malipo kidogo Sana, wakulima hawakukopwa mazao yao. Viwanda vilijengwa na kutapakaa nchi nzima.

Ktk kutimiza vipaumbele hivyo, baadhi ya maeneo yalidumaa kabisa, Barabara na reli vilidumaa, mishahara ya watumishi ilikua midogo Sana, bidhaa muhimu hazikupatikana madukani, zikiwemo nguo, sabuni, sukari na vinginevyo. Watumishi hawakulalamika Sana kwasababu Nyerere alikua alieleza nini anataka kuifanyia nchi.

Magufuli pia alikua na vipaumbele vyake, reli, Barabara, viwanda, Afya na Elimu na ujenzi wa meli na kufufua ATCL, nidhamu na uwajibikaji serikalini, kubana matumizi serikalini


Alikua akisema kwamba, hatoweza kuongeza mishahara hadi atakapokamilisha hiyo miradi, sote tuliona ni kiasi gani hii miradi ambayo watangulizi wake waliogopa hata kuigusa lakini yeye aliamua kuianza.

Kati ya Kikwete ambaye kila mwaka alikua akiongeza mishahara na kusafiri kila wiki lakini alishindwa hata kujenga daraja la Wami, na Magufuli ambaye alikua hasafiri Wala kuongeza mishahara lakini alifanikiwa kukusanya pesa ya kujenga
1)Bwawa la Nyerere $2.9B
2)Daraja la Kigongo busisi Tsh 700B
3)Ndege 11 za ATCL $700M
4)Upabuzi wa Barabara ya Kibaha $60M
5)Daraja la Wami
6)Mali ya MV Mwanza Tsh 90M
7)SGR Dar - Moro $1.9B

Hivi kweli unasahau haya yote eti kwasababu watumishi wa serikali wasiozidi 2M hawajaongezewa mishajara?.

Sasa ukiacha kuongeza mishahara, tena kwa asilimia ndogo ambayo bado haiwatoshi ninyi watumishi hebu tupe vipaumbele vya SSH, ukiacha hiyo miradi aliyoikuta.
 
Benki ya dunia huwa wanatoa Mikopo kwani huwa tunaenda kuwatembelea.
Museveni yuko hapo pamoja na ujinga wake, hatembei na Mikopo anapata, hizi safari ni excuse za watu kupiga pesa na kutalii.
Nasikia symbion nao wamelipwa mabilioni haraka sana.
 
Haya ndio mambo nilikua nataka kuyasikia.
Basi kama ndio ivyo na wahusika bado wapo tu wanaleana vibaya na haifai
 
Sijasahau kazi ya mwamba lahasha

Viapaumbele ya SSH kwa navyoliona game lake ni kama ifuatavyo
1.Afya (kwasasa ruzuku za dawa zinafika kwa wakati,vifaa vya kisasa vinakuja mara kadhaa na kaongeza watumishi )
2.Elimu(kuondoa ada f6,kuongeza budget ya mkopo wanafunzi wa vyuo vikuu,fedha za tafiti nk), kijenga madarasa elimu ya sekondari na kuajiri walimu)
3.Mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji(task force kuondolewa watu wamalipa kodi bila kutumia nguvu kubwa, apa hata revenue imeongezeka)
4.Kilimo..(kupandisha budget ya kilimo×4 na kuanzisha block farms nk)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…