Sijasahau kazi ya mwamba lahasha
Viapaumbele ya SSH kwa navyoliona game lake ni kama ifuatavyo
1.Afya (kwasasa ruzuku za dawa zinafika kwa wakati,vifaa vya kisasa vinakuja mara kadhaa na kaongeza watumishi )
2.Elimu(kuondoa ada f6,kuongeza budget ya mkopo wanafunzi wa vyuo vikuu,fedha za tafiti nk), kijenga madarasa elimu ya sekondari na kuajiri walimu)
3.Mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji(task force kuondolewa watu wamalipa kodi bila kutumia nguvu kubwa, apa hata revenue imeongezeka)
4.Kilimo..(kupandisha budget ya kilimo×4 na kuanzisha block farms nk)
Yote uliyotaja katika sekta ya Afya na kilimo ni muendelezo ya aliyoanzisha Magufuli, vifaa vyote vikubwa katika Hospital zetu ni kazi ya Magufuli. Mimi nilikua hapo Muhimbili kipindi cha Mwinyi na Mkapa Hadi Kikwete, hali ya Hospital zetu ilianza kubadilika mara tu JPM alipoingia madarakani
1) Alitimua uongozi wa Muhimbili na kuweka uongozi mpya
2)Alibadilisha uongozi wa MSD
3)Alianzisha mfumo wa kununua dawa Moja kwa Moja toka viwandani India badala ya kutumia "middlemen".
4)Alipandisha kiwango cha upatikanaji dawa kutoka wastani wa 22% kabla ya uongozi wake Hadi 90%
5) Alifufua CT scanners na MRI ambazo zilikua hazifanyi kazi kutokana na sababu mbalimbali
6)Alinunua X-ray machines za kisasa na kununua vifaa vipya Kule Ocean road Cancer Institute ikiwemo PET scanner
7)Aliokoa Hospital ya Bugando ambayo ilikua na mgogoro mkubwa wa kiuongozi na kifedha
8)Aliimarisha utendaji wa MSD kiasi cha kufanya ichaguliwe kuwa kinara katika SADC na kuchaguliwa kuwa ndio mnunuzi na msambazaji wa dawa na vifaa tiba wa SADC
9)Alikutana na kushawishi uwekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini, zaidi ya viwanda 5 viko ktk hatua za mwisho
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app