Hivi kweli Hilo ndio linakufanya uwe unapost kwa shangwe kila tukio Kama Hilo likitokea Kenya?, Sio kweli ninakataa
Wewe kinachokufa uwe "excited" ni sifa kuona maofisi na HQs za kimagharibi zinafunguliwa Kenya bila hata kujali Kama zinawasaidia wakenya.
Hivi kweli kelele zote hizo ni kwasababu ya ajira chini ya watu 300, tena hapo Nairobi wakati hakuna sehemu zingine za Kenya zinazofaidika?.
Sasa mbona Kenya tatizo la ajira linazidi kuongezeka kwa Kasi kuliko nchi zingine hapa EA ambazo hakuna hata ofisi Moja ya UN?.
Kenya mtapata taabu Sana kwasababu hamtaki kujenga uchumi wenu wa ndani badala yake mnategemea Sana watu na Mashirika ya nje kuja kuwajengea uchumi, au kwenda kufanya kazi nje ya nchi yenu ili kutuma pesa Nyumbani, hii ni hatari Sana.
Lazima muwekeze kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii, madini, ujenzi na uzalishaji viwandani ndio ufumbuzi wa ajira, na kumaliza njaa hapo Kenya, hayo ya ofisi za UN na makampuni ya kimataifa yanazidi kufanya maisha kuwa magumu kwa wakenya kwasababu
1)Wafanyakazi wa UN watalipwa pesa nyingi, hivyo watakuja na demand kubwa ya kununua bidhaa za Kenya kwa wingi, hii itaongeza Bei za bidhaa na kusababisha ongezeko la "inflation rate"
2)Kutakua na tofauti kubwa ya kipato Kati ya watu wanayoishi Kenya Kati ya waajiriwa wa UN na HQs ya makampuni ya nje na wale waajiriwa serikalini, hivyo kupunguza mirali ya wafanyakazi na kusababisha rushwa kuongezeka nchini na kupata kwa "crime rate"
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app