Huko sio kwetu lakini bado ni Kenya. Ni huzuni kuona wanapitia masaibu haya. Nimesema hapa mara nyingi kwamba serikali inastahili kuchimba boreholes kila mahali huko Northern Kenya ili kupunguza athari ya ukame. Kenya ni miongoni mwa nchi ambayo imeendelea sana ukiilinganisha na nchi zingine za Sub saharan Africa lakini kwenye mambo haya ya kuwashughulikia wafugaji wa Northern Kenya huwa tumezembea sana. Huwa nashindwa kwa nini kuna njaa Northern Kenya and yet serikali ya Kenya ina uwezo mkubwa sana wa kifedha kushinda serikali yoyote ukanda huu. KRA ina target ya kukusanya around $20 billion this financial year. Sasa sio kwamba Kenya haina pesa, pengine priorities ndio zipo wrong. Ujue hii njaa inatupea bad press, inafanya watu duniani wafikirie Kenya ni nchi masikini kupindukia na kumbe ni serikali haijali. Pengine rais ajaye atasaidia.