Mimi ninsmkubali Sana David Ndii toka zamani bila kujali mrengo wake wa kisiasa, huo upumbavu wa kuegemea mirengo ya kisiasa sisi huku Tanzania sio tatizo kubwa Kama ilivyo huko kwenu, hapa nimezungumzia Rutto na Raila na nimewaweka kundi Moja japo wapo pande mbili tofauti za kisiasa.
Jambo Moja ambalo linanisumbua Sana Kenya ni jinsi ambavyo hamtumii akili zenu katika kufikiria badala yake mnavutwa zaidi na ukabila, ukanda au vyama vya kisiasa. David Ndii ni miongoni mwa watu wenye uwezo mkubwa Sana wa Elimu na akili ya kufikiria mambo, lakini kila anapotoa maoni yake, badala ya kujadili kile alichokisema, ninyi mnapinga kwa misingi ya mirengo ya kisiasa.
Huku Tanzania wakati wa kipindi cha Magufuli, ninyi wakenya mlikua mkisema tulikua tunaunga mkono CCM, Kuna wakenya wapumbavu walikua wakisema wote waliokua wakiunga mkono utawala wa Magufuli ni "CCM die hard". Hivi Sasa walewale waliokua mliokua mkiwaita CCM die hard", wanaipinga CCM mnawaita "Sukuma gang". Hii ni kuonyesha kwamba, Tanzania hatuna huo ujinga wa kufuata mirengo ya kisiasa Kama huko kwenu, tunachofuata ni vitendo na akili ya mtu husika.
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app