Ninakushukuru sana kwa kuniweka sawa, mimi ni mgeni humu jamvini nimeingia leo, japo huko nyuma nilikua ni kama mtazamaji tu. Lengo langu ni kuwakumbusha ndugu zangu toka Kenya kwamba, hivi sasa inaonekana mpira huu unachezewa nusu uwanja tena upande wa Kenya, kwa sababu kufananisha majengo, barabara, Hoteli na sehemu za kifahari, huo ni uwanja wa Kenya, Tanzania haijawahi kuwa na competative advantage katika eneo hilo, Tanzania eneo lake kubwa ni usawa wa binadamu, maendeleo ya vitu ni sifa ya ubepari.
Kinachoonekana ni kama vile Tanzania imefanikiwa katika hatua ya awali ya ujenzi wa umoja wa kitaifa na usawa miongoni mwa watu wake, sasa imeamua kujenga uchumi ambalo kwa kweli lilikua eneo la Kenya waliloanza nalo, leo kuona Dar inatoa kijasho na Nairobi ni jambo la kujivunia sana kwa watanzania, miaka 15 Iliyopita halikuwa jambo la kufikirika.
Kuna haja ya wakenya kuliona hilo na kujitahidi nao kugeuka kuona kama hayo maendeleo ya vitu waliyoanza nayo tangu Uhuru kama bado yanafaida kwa wananchi walio wengi, au inabidi wajiulize na ikiwezekana wafungue uzi ili tuchangie ni kwa jinsi gani wanaweza kulijenga taifa leo kwa kuwaleta watu wao pamoja kama ilivyo Tanzania, ninahisi inaweza kusaidia wananchi wengi zaidi kuliko hizo malls wanazoshabikia kila kukicha.
Ninaomba kuwakilisha
Sent using
Jamii Forums mobile app